Random

Maswali 10 ya kujiuliza tunapoelekea mwisho wa mwaka | 2019 Reflection

Reading Time: < 1 minute

Nimepata hii idea kutoka kwa Jessica, na alikuwa anaposti kwenye status yake, nikaona ni kitu kizuri sana namimi niandikie blog post.

2019 hiyo inaisha, naona kama mwaka ulianza juzi tu lakini tayari ni November, na 2020 ndo inakaribia mlangoni ikiwa tayari kuingia.

Nimefikiria tujiulize maswali ili tuangalie tumeishije 2019, eneo gani tuongeze bidii 2020, eneo gani tumejivunia sana jinsi tulivyoishi 2019 nk.

Maswali yenyewe ni:

1. Kitu gani umejifunza kuhusu maisha katika mwaka huu?

2. Kitu gani umejifunza kuhusu wewe ndani ya mwaka huu?

3. Ni mpango gani uliouweka katika mwanzo wa mwaka na haujautimiza?

4. Mipango ipi umeitimiza?

5. Vitu gani ungetamani ubadilishe kuhusu jinsi ulivyoishi mwaka huu?

6. Kitu/vitu gani vimekufanya ushindwe kutimiza malengo uliyopanga?

7.Na umejiandaaje kuvikabili katika mwaka 2020?

8. Umejifunza skill gani mpya mwaka huu?

9. Ongelea ukuaji wako katika mwaka huu kama binadamu.. Katika maeneo ya hisia, uchumi, elimu, physical, spiritual nk.

10. Ukiambiwa uelezee mwaka 2019 ulivyokuwa kwako kwa neno moja, utasema ni lipi?

La nyongeza…

11. Kitu/ vitu gani umetimiza katika mwaka huu ambavyo vinakufanya ujivunie?

Eunice

2 Comments

Share Your Thoughts With Me