Hakuna kitu ambacho hautakisikia kuhusu hatua yoyote unayoiendea maishani, na hivyo pia hata ukiwa unaenda chuo au ukiwa chuo, utasikia maneno mbalimbali. Mengi yatakuwa ya ukweli lakini pia mengine yatakuwa ya uongo, na leo nitaongelea machache ya uongo ambayo niliambiwa.

-Chuoni bata

AH, hili linaongelewa sana, na utaambiwa sana au hata umeanza kuamini hili. Ukibalance muda wako unaweza ukaenjoy maisha ya chuo kwasababu ya uhuru utakaokuwa nao, ila sio bata kwamba maisha ya chuo ni rahisi, sio rahisi. Kiukweli maisha ya chuo yanastress sana, hasa mahitaji yake yanavyokuwa nyingi, kwahiyo jua kubalance muda wako. Na utapata muda wa kula bata ila sio kwamba maisha yako yatakuwa bata muda wote.

-Kila somo liwe na daftari lake

Stori ya kweli, nahisi nimemaliza chuo na makaunti manne kama sio matatu. Nilinunua kaunta moja ambalo lilikaa semester mbili na kila mwaka nilikuwa naongeza ili kujisikia kwamba nimebadilika mwaka wa chuo ila yalikuwa hayajajaa. Kutokana na soft copies ambazo unaweza kuzisoma kwenye smarhone ama laptop, muda mwingi unajikuta unatumia soft copy kuliko kuandika. (Ila usiwaambie malecturer kwamba umeona nimeandika hivi).

-Bila laptop, chuoni hauwezi soma

Labda niseme hivi, kuna matumizi mengi ambayo kuwa na laptop yangekusaidia, lakini asilimia 80 ya jinsi tunavyotumia laptop chuo ni kwaajili ya movie. Wengi tulikuwa tunaitumia hivyo. Kama kweli kusoma hata smartphone unaweza kusomea na nina mifano mingi ya wanafunzi ambao walitumia smartphone tu kusomea na tumemaliza nao. Kwahiyo isikupe presha sana kama hauna uwezo wa kununua sasa, utanunua tu utakapofanikiwa kiuchumi au utakapoona umuhimu wake, usijipe presha kwasababu ya laptop, smartphone inatosha.

serious ethnic young woman using laptop at home

Usipopata mchumba/ mume/ mke chuoni huwezipata tena

Ni hivi, unaenda chuo kusoma, sio kutafuta mke/mume, ukimpata tunamshukuru Mungu na usipompata sawa, na statistics zinaonyesha ni asilimia chache sana ya mahusiano ya chuo ndio hufikia mpaka ndoa, na hata hivyo watu hukutana sehemu mbalimbali sio lazima iwe chuoni,usiwe na papara na kwenda kutafuta yasiyokupeleka.

(Unaweza pata ushauri wa mahusiano kwa wadada waliopo chuo)

-Chuoni hakuna kufeli

Okay, najua huku shuleni tulikuwa ukifeli ndio inaonekana kama mwisho wa dunia na ndio maana supp, carry na disco havionekani kama vikubwa kwasababu havioneshi kukunyima nafasi nyingine tena kama mitihani ya NECTA. Ila usichezee elimu ya chuo lwasababu ‘kufeli’ kwake hakufanani na ulikokuzoea.

Na hayo ndio mambo niliyoambiwa kuhusu maisha ya chuo, ambayo niliyaprove kuwa ya uongo.

Niambie na wewe, ni mambo gani umeambiwa ambayo ni ya uongo kuhusu maisha ya chuo.

Eunice

You May Also Like

13 thoughts on “Mambo matano ya uongo, utakayoyasikia kuhusu maisha ya chuo.

 1. Jessy

  Bora uuwaambie

  1. Eunice Tossy

   ??????? watag wanaohusika???

 2. Praygod

  I’m glad you wrote this article, I just hope the target group will read it?

  1. Eunice Tossy

   Thank you PG! ???

 3. A letter to a depressed recent graduate (part 2) - Eunice Tossy

  […] Also Read: Maisha ya Chuo […]

 4. 10 ways to have fun in university | Your Guide to University Life - Eunice Tossy

  […] Soma : Chuoni bata na mambo mengine ya uongo utakayoyasikia kuhusu chuo […]

 5. Makosa niliyoyafanya nilipokuwa chuo | Your Guide to University Life - Eunice Tossy

  […] ni kati ya wale waliokuwa wanajua chuo ni bata, na of course nilienjoy na nimefaulu vizuri, ila sikuweka effort kama niliyokuwaga nayo nilipokuwa […]

 6. Kwa anayeona chuo kigumu, hauko peke yako, hizi hapa tips za namna ya kusurvive - Eunice Tossy

  […] Ukweli ni kuwa tofauti na tunavyoambiwa Mara nyingi, chuoni sio bata. […]

 7. 10 ways to have fun in university | Your Guide to University Life – Eunice Tossy

  […] Soma : Chuoni bata na mambo mengine ya uongo utakayoyasikia kuhusu chuo […]

 8. Kwa anayeona chuo kigumu, hauko peke yako, hizi hapa tips za namna ya kusurvive – Eunice Tossy

  […] Ukweli ni kuwa tofauti na tunavyoambiwa Mara nyingi, chuoni sio bata. […]

 9. Makosa niliyoyafanya nilipokuwa chuo | Your Guide to University Life – Eunice Tossy

  […] ni kati ya wale waliokuwa wanajua chuo ni bata, na of course nilienjoy na nimefaulu vizuri, ila sikuweka effort kama niliyokuwaga nayo nilipokuwa […]

 10. A letter to a depressed recent graduate (part 2) – Eunice Tossy

  […] Also Read: Maisha ya Chuo […]

 11. Jinsi ya kuandaa ratiba binafsi ya kujisomea chuoni – Eunice Tossy

  […] tips kwa wewe unayependa kujiwekea ratiba natabia ya kujisomea binafsi kwasababu ukweli ni kuwa sasa hivi wote tunajua kuwa chuo sio bata, kwa hivyo msuli wakati wote ni […]

Share Your Thoughts With Me

Translate »