Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Jinsi ya kulinda afya yako ya akili kipindi hiki cha virusi vya Corona

Mwaka 2020 umeanza na mambo mengi. Ukiachana na yanayoendelea kwenye maisha yetu, pia kuna Coronavirus.

Baada ya virusi hivi kusambaa na mambo yote yanayoendelea duniani, ni muhimu kulinda afya zetu za akili na hisia ili tujue hata jinsi ya kujiangalia afya ya mwili kwa maana kimoja kikiharibika kinaweza kuharibu vyote.

Hizi hapa ni namna unazoweza kujali afya yako ya akili kipindi hiki;

Usipaniki

Kuna watu wengi waliopona kuliko waliokufa kwa virusi hivi.

Inasemekana hadi tarehe 15 mwezi huu, walioambukizwa ni 156,000 kwenye nchi 80. Waliokufa ni 5800, na zaidi ya watu 730,000 walipona virusi hivyo.
Kwahiyo usipaniki, vinaambukizika ila pia uwezekano wa kupona ni mkubwa kuliko wa kufa.

Usitumie muda mwingi mitandao ya kijamii

Haswa Twitter, naona kule ndio kuna habari za uongo na kweli kuhusu Coronavirus. Na ubaya wa hizi habari ni zinazidi kukutisha unaweza kufa kwa presha au kujawa na chuki/ubaguzi kwasababu ya habari kama hizi. Hakikisha unachuja habari nyingi kuhusu virusi hivi unazozipata mtandaoni.

Uwe na sehemu chache unazopata habari ambazo unaziamini

Unaweza kusoma na kusikiliza kuhusu Coronavirus, ila sio kila sehemu iwe chanzo chako cha habari. Ukipata habari nyingi pia unashindwa kufanya maamuzi, kwahiyo ni heri ukapata chache ambazo utazidadavua mwenyewe na kujipanga vizuri kuliko kusikia maoni ha sauti nyingi kuhusu hili swala. Tafuta habari kwaajili ya kujilinda na kujua hatua za kuchukua dhidi ya virusi hivi.

Weka vitu ndani kwaajili ya matumizi

Ili usiwaze kama umeambukizwa au la kila unapotoka kununua vitu, basi uweke vitu stoo ndani kwaajili ya matumizi.

Endelea kuwasiliana na watu kwa simu

Kwasababu ya kujitenga unakotakiwa ukufanye, unaweza ukajisikia mpweke mara nyingi au ukawa na mawazo yanayohusiana na ugonjwa huu muda wote. Usiache kuwasiliana na wengine kwa kuwapigia simu, kuongea nao kujua hali yao na wewe pia kuwaeleza unavyoendelea.

Amini kuwa wapo wanaojitahidi kutafuta suluhisho

Hii inakuondolea mzigo wa kuwaza sana kuhusu huu ugonjwa na kukufanya uweke nguvu zako kwenye kujilinda. Lakini pia inakuondolea mawazo ambayo hayaongezi chochote kwenye kutafuta tiba. Wataalamu wapo wanafanyia kazi na serikali nyingi pia zinatilia mkazo kwa namna moja au nyingine kulinda raia wake.

Fanya mazoezi na mambo mbalimbali unayoyapenda

Muombe Mungu atulinde na atuondolee huu ugonjwa (naamini ukiomba unapata amani, tumaini, unatua mzigo ila pia unapata sehemu ya kulia na kuondoa uchungu, na pia Mungu anaweza kutuondolea hili janga), na pia fanya mazoezi, kula vizuri ili uwe na nguvu (usije ukafa kwa mengine), soma vitabu, maisha hayajasimama kwasababu ya hili, mambo mengine yanaendelea.

Hizo ndio njia chache ninazoona zinaweza kukusaidia kulinda afya yako ya akili na hisia katika haya yanayoendelea.

Unajilindaje na virusi vya Corona?

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป