Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Vitu vya kufanya asubuhi ili uanze siku vizuri

Sijui ni mimi tu au wote, ila naonaga nikianzaga asubuhi vibaya siku nzima inaharibika au inaenda tofauti na nilivyopanga.

Hivyo kuna vitu ambavyo navifanya au sivifanyi ambavyo vinasaidia akili na mwili kuanza siku vizuri.

Vitu hivyo ni:

Kusali

Kabla sijaamka namuomba Mungu aiongoze siku hiyo, na ikawe ya baraka na nzuri kwangu.

Wengine pia hutumia muda huu wa asubuhi kusoma Biblia maana nimegundua nikitumia muda na Mungu asubuhi nakuwa mtu mzuri kuliko nisipoanza na Mungu.

Kutokukurupushwa

Kuweka ratiba ya muda wa kuamka usiku wake ili nisikurupuke tu. Muda mwingine nawekaga ratiba ya vitu vya kufanya ili siku isiende bila kusudi. Lakini pia napenda kuamka mwenyewe, maana nikiamshwa na simu au mtu akinikurupusha huwa sijaamka vizuri.

Kutopeleka mbele alarm

Kuna siku huwa napanga kwenda kukimbia saa 11 alfajiri, ila alarm ikilia naipeleka mbele kwasababu ni asubuhi sana. Huo sio mwanzo mzuri.

Ukiipeleka mbele alarm unaufanya mwili uwe hauna haraka siku hiyo, unakuwa polepole. Ila ukiamka alarm inapoita unachangamka.

Kutoangalia simu kwanza

Najitahidi kwenye hili, ukitaka kulala pia sio muda mzuri wa kuangalia simu, hivyo hata ukiamka kuanza kuangalia mitandao nk sio kitu kizuri sana.

Hata email, hasa kama umeomba kazi.. maana ukiona umepata no furaha ila ukikosa utahuzunika siku nzima.

Au matokeo ya chuo pia. Angalia jioni.

Kutokugombana na watu asubuhi

Kama nina magomvi huwa nahakikisha yanaisha usiku, maana asubuhi ni mwanzo siku mpya. Sasa kuianza na ugomvi, au hasira sio mwanzo mzuri maana siku nzima utaongozwa na hizo hisia. Au utafikiria mambo hayo siku nzima.

Kusalimiana na wengine

Hili ni muhimu pia. Kunakufanya ujisikie upo kwenye jamii hauko peke yako.

Kujiambia maneno mazuri ya shukurani

Kuna mwanamziki, Lira alisemaga akiamka kila siku alikuwa anajisemea manenomazuri kwaajili ya siku hiyo na anajiandaa kuyapokea, anavaa vizuri akisubiria kuyaona.

Ni njia nzuri pia. Kujizungumzia maneno mazuri ya shukurani na ya kuielezea vile siku yako ungependa iwe au wewe pia uwe kwenye siku hiyo husaidia kukuandaa kwa siku hiyo.

Kuwa excited kwa siku mpya
Kila siku mpya ni fursa na nafasi ya mambo mapya na ya tofauti kutokea. Ni siku ambayo haitarudi.

Ni siku ambayo inatupa nafasi ya kuanza tena, kujaribu tena, kujifunza mapya.

Nilipokuwa chuo ndio nilianza tabia ya kuwa excited kwa kila asubuhi mpya inapoanza. Hii inanifanya niamke na furaha na kutamani kujua siku hiyo nitapata kitu gani kwenye maisha au nitatengeneza kumbukumbu ipi kwenye maisha yangu.

Ifurahie asubuhi. Ifurahie siku yako yote.

Asubuhi inatengeneza mood ya siku nzima, ianze vizuri.

Ni vitu gani huwa unafanya asubuhi, ili kuianza siku vizuri?

Eunice

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป