Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Mahusiano

Soma hii kama unahisi hauna bahati kwenye mapenzi

Dunia ya sasa imebadilika sana, au labda hivi ndivyo watu walivyokuwaga toka zamani sema unapokuwa mtu mzima hayo mambo unayapitia kwa ukaribu zaidi kuliko ulivyokuwa mtoto. Usaliti, kuachwa, kunyanyasika katika mapenzi, yote ni mambo yanayoweza kukufanya ufikie hatua ya kuamini kiwa hauna bahati kwenye mapenzi. Hayo kutokea lakini pia mara ngapi yamekutokea ndio kabisa inaweza kukufanya uamue kutoingia tena kwenye mahusiano au kutoamini tena kitu kinachoitwa mapenzi.

Bonyeza hapa kusoma mambo ya kufanya unaposalitiwa na mpenzi wako

Kama unahisi hauna bahati kwenye mapenzi, napenda ujue kuwa naelewa. Najua umeumizwa sana mpaka umefikia hatua ya kuamini hivyo. Unajua kila unayempata alikusaliti, kila uliyewahi kuwa naye alikuumiza, hakuwa furaha yako, hukuona tamu ya mapenzi. Inaeleweka kwanini unaamini hauna bahati ya mapenzi, naelewa kwanini upo hapo, inaweza kuonekana kama ni hali isiyoweza kubadilishwa kwasababu mahusiano yanahitaji watu wawili ila kabla haujaangalia mtu mwingine ajaye kwenye maisha yako, ni muhimu kuangalia ni watu gani huwa unawaruhusu kuingia kwenye maisha yako.

Kuna zoezi nililifanya wakati nimeachana na watu kadhaa na nilitaka kupata mpenzi wa tofauti na wale nilioachana nao, nilichofanya ni kuchunguza vitu gani vilinivutia kwa wale nilioachana nao, na ni vitu gani si vizuri kwao ambavyo niliviona ila nilivipuuzia. Unaweza pia kuangalia ni vitu gani wanafanana, tabia, mienendo, mawazo ya maisha nk. Hii inakusaidia kuona kuwa watu wa aina fulani, au tabia fulani ni nzuri kuziepuka kwa mtu unayemleta kwenye maisha yako kama mpenzi. Ukikosea unajifunza kutokana na makosa, ili usirudie kuendelea kuwa kwenye mahusiano na watu tofauti ila tabia na mienendo ile ile ambayo haikukufikisha mbali na wale uliokuwa nao hapo mwanzo.

Pia kuongezea kwenye hili jaribu kutoka na watu ambao haujawahi kufikiria kutoka nao, hapa namaanisha kama umezoea kuwa na wanaume au wanawake wa namna fulani na tabia fulani, mara nyingi kubali kuwa na wa aina tofauti. Inawezekana labda sio kwamba hauna bahati, ila upo na watu ambao sio sahihi kwako, hamuendani. Na kwa vile unaendelea kutafuta hao hao, na mnashindwana basi unahisi hauna bahati badala ya kubadilisha watu na tabia zile unazoona wewe zinakupendeza kwa juju juu. Mambo ya msingi sana kuzingatia unapotafuta mpenzi ni kuendana kwa mambo mnayoyathamini, namna mnavyoiona dunia na mitindo ya jinsi mnavyotaka kuishi maisha pamoja na mbeleni.. mkishindwa kuwa na vitu vingi mnavyothamini vinavyofanana inakuwa ngumu kidogo labda angalia na hilo, usikute unaingia kwenye mahusiano na wengi kwa nia ya kuwabadilisha ili muendane na ukishindwa unajihisi hauna bahati…

Jambo lingine la msingi ni kuwa ukianza kutafuta mwenza ingia kama haujawahi kuumizwa, usiingie na mtazamo wa kuwa hauna bahati, hautobahatika. Jaribu kupenda tena, jitoe hauwezi jua lini kwako itakuwa njema. Samehe kabisa, usichukue maumivu yaliyopita ukayaingiza kwenye mahusiano mapya, pona. Muone huyu mtu kama moya wakuanza naye ukurasa mpya, usimuone kama muendelezo wa ule ukurasa ulioisha, hii itakupa nafasi ya kumsoma na kumjua yeye kama yeye na kujua jinsi ya kumfurahisha na kuishi naye. Ni muhimu kubadilisha mtazamo, vile unavyokiri ndivyo itakavyokuwa, basi kwa vile bado unaishi kuna mambo mawili matatu ya kubadilisha lakini bado unaweza kubahatika kwenye mahusiano.

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป