Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Matumizi mazuri ya boom yatakayolifanya likae kwa muda mrefu

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Shida ya hela ni kuwa ukianza kuitumia inaenda haraka sana.

Haswa boom, yani linaisha hata lingine bado haujasign na unaanza kuomba hela nyumbani Muda sio mrefu.

Katika matumizi yangu ya hela hizi hapa njia nilizoona ni rahisi za kulitumia boom kwa umakini ili lidumu kwa Muda kidogo.

1. Kuweka akiba

Kuna migawanyo mbalimbali ya hela ambayo watu huifanya, na wengi hushauri uwe kiwango fulani constant ambacho unakiwekea akiba. Hiko kiwango unakuwa haukigusi kabisa, mpaka utakapohitaji kweli kutumia hela yako ya akiba. Naasume ndio huo Muda utakaofulia.

2. Kufanya meal planning

Mimi nilikuwa napanga nakula nini kwa wiki na najua matumizi ya wiki nzima kwenye chakula itanigharimu shilingi ngapi. Meal planning inakusaidia pia kutokutumia hela tu kwasababu ya tamaa au kwavile unaona chakula, ila kutumia kwa kwa kufuata mpango fulani. Je, ungependa niandike kujua kwa undani kuhusu meal planning?

3. Kuigawanya kwa wiki

Usiitoe hela yote benki, toa kiwango kidogo tu. Lakini pia mkononi uwe na kiwango unachokitumia kwa wiki, ukiwa na kiwango kikubwa kinatamanisha kuendelea kukitumia. Hivyo kwa wiki inasaidia maana haikutii majaribuni. Kiwango hicho unaweza kukipanga baada ya kujua utakula nini wiki hiyo na labda kuweka nyingine ya matumizi mengine kama nauli, maji na dharura.

Angalia Video : Matumizi mabaya ya boom niliyoyafanya nikiwa chuo

4. Kufanya shopping ya vitu vya jumla

Nimegundua vitu vingi vinavyouzwa kwa jumla huwa vinapungua bei kidogo kuliko kwa rejareja. Je, na we we umeona hili?

Moja ya vitu vilivyonisaidia kudumu na boom wakati nasubiria lingine ni kununua vitu vya jumla. Mfano, toilet paper, pad au maji (kama unanunua).

Vitu vya jumla vinadumu Muda mrefu lakini pia unakuwa umesave hela kwa kununua kwa bei ya chini kidogo.

5. Ukienda kununua kitu nenda na hela kamili

Hapa sina maneno mengi, ila ukitoka, usitoke na hela nyingi. Ukienda dukani au shopping, nenda na hela kamili inayotosha kununulia unachotaka ili usijaribiwe.

6. Itengenezee mpango kabla haujaipata

Si unajua unapokea shilingi ngapi? Iwe na mpango kabla haijaja. Hela ikiwa haina mpango, inapotea haraka. Hivyo kabla haujaipata, uwe umeshapanga matumizi au vitu unavyotamani kuifanyia. Ili ukiipata tayari una bajeti na unaifanyia tu matumizi.

Ikiwa ukawa hauna bajeti unaweza kuitumia tu hovyohovyo ikaisha bila we we kuona ulichoifanyia.

7. Ishi ndani ya uwezo wako (live within your means) ila pia jua jinsi ya kuwa na matumizi mazuri ya hela

Kuishi ndani ya uwezo wako kwangu Mimi naichukulia kama kuishi kwa kiwango na uamuzi wako, kuna wengi ambao hupenda kufuata watu wanakula nini au wanaenda wapi na wao kufanya bila kujali uwezo wao unaruhusu ama la! Ishi ndani ya mipango na uwezo wako.

Lakini pia kuweza kujua jinsi ya kuwa na matumizi mazuri ya hela, soma makala hii nyingine niliyoandika kwaajili ya hilo pekee. Kuisoma makala hiyo,bonyeza hapa.

(Bonyeza hapa kufollow akaunti ya Maisha ya Chuo Instagram, akaunti hii inashare dondoo na ushauri unaowasaidia wanachuo kukabiliana na changamoto za maisha ya chuo)

Eunice

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »