Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Budgeting Tips kwa wanachuo wasiokuwa na boom // 16 Tips

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

——

Kwa wale wenye booom na wanatamani kujua jinsi gani walitumie ili likae kwa muda mrefu, maana boom linaishaga haraka??, soma hapa.

Makala hii napenda iwahusu ambao hawajapata boom.

Labda waliomba mkopo ila hawakupata au hata wale ambao hawakuomba mkopo hivyo wanasomeshwa na wazazi au wafadhili.

Likija swala la hela, chuo ni sehemu moja nzuri ya kufanyia mazoezi kujitegemea kwenye maswala ya pesa, ukiingia kazini uwe tayari unajua kutumia vizuri ili uutumie mshahara kwa maendeleo.

Kwa ambao hawana boom hizi hapa njia ambazo unaweza kubudget hela unayoipata ya matumizi:

1. Jua una kiasi gani cha kutumia

Jua una kianzio cha shiling ngapi, uliyotumiwa au uliyopata sehemu.. Usisahau kurekodi kila hela unayoingiza na unayoitoa mfukoni mwako, mimi huwa natumia hii hapa app ya bure kabisa.

2. Jua unataka kutumia kiasi gani

Njia nzuri ya kujua hivi ni kurekodi pia, angalia kwa wiki unatumia sh ngapi, kwenye usafiri, chakula na matumizi mbalimbali unayoyafanya.

Ili hata muda mwingine unajua matumizi yako. Lakini pia usisahau kuweka kiasi akiba. Kujua jinsi ya kuweka akiba, soma hapa.

Akiba itakusaidia hata siku wazazi wameishiwa utakuwa na chakukusogeza. Unaweza kuweka hela kubwa, kwenye mfano airtel money wanaakiba inaitwa Timiza, au chenji zinazobaki ukaziweka kwenye kibubu.

3. Usiigize maisha

Kinachotutia vijana hasara ni kujilinganisha na kutaka kufuatilia kila staili mpya inayokuja. Tunaigiza maisha sana.

Wale ambao wanategemea nyumbani, wafadhali au wafanye kazi ili wajisomeshe, Usione aibu kuishi maisha yako, kuhangaika kutaka kuishi maisha ya watu huleta gharama.

Ukitaka kupika halafu ukibebe uende ukale chuo, beba, ishi maisha yako.

Umeenda chuo pekee yako, usionee aibu kule unakotoka, kukubali maana bila huko ulipotoka usingekuwa hapo ulipo sasa na usingekuwa na akili na mawazo uliyonayo leo.

4. Kuweka bili

Nahisi kitu kinachoweza kukupa mawazo chuo ni chakula na sehemu ya kulala. Mavazi na simu za kijanja ni show off tu.
Ukipata hela kwa kiwango kikubwa unaiwekea bili ya chakula labda ya mwezi au zaidi ili uwe na uhakika wa pakula.

Hata home kukiwa hakupo sawa unajua kula uhakika.

5. Kuscan notes au kutafuta notes za soft copy

Unaweza kuscan notes kwa kutumia hii app, unapiga tu picha halafu zinakuwepo kwenye simu. Au tafuta soft copy ili upunguze gharama za kununua notes.

6. Tumia vitu vinavyopatikana bure chuoni

Mfano internet, sio lazima ujiunge, unaweza kwenda kutumia library / au jiunge bando la chuo

7. Fanya manunuzi kwa kulinganisha bei za sehemu mbalimbali au omba punguzo la bei kabla ya kununua.

8. Kununua vitu kwa wingi

Kwa wale wanaokaa off, nunua vitu kwa jumla. Mfano mchele, unga na maharage na hakikisha unapika ghetto. Punguza kula barabarani kwasababu tayari unavitu vya kupikia nyumbani.

9. Rudia matumizi ya vitu

Mfano sio vibaya kuanza semester mpya na daftari lile lile au peni ile ile.

10. Jua tofauti kati ya unakihitaji kitu (want) na unakitaka (need)

Kukitaka baadae unaweza usikitake tena, ila unakihitaji maana yake mambo mengi yatasimama bila hicho kitu kuwepo.

Hakikisha unafanya manunuzi ya vitu unavyovihitaji. Na sio vibaya kujinunulia vitu vya luxury, ila manunuzi hayo yasiharibu ratiba zako za kifedha.

11. Uza vitu usivyovitumia

12. Angalia chuo kina event gani

Mara nyingi huwa ni bei rahisi sana kwenda na chuo sehemu kuliko kwenda mwenyewe. Kama chuo kimeandaa event jiunge nao upunguze gharama za kula bata kwa gharama.

13. Angalia vitabu library au mitandaoni

Usinunue vitabu vinavyopatikana muda mfupi

14. Unaweza ukafanya biashara ndogo ndogo haswa kwa waliopo off campus.

(Hizi hapa ni biashara mbalimbali unazoweza kuzifanya.)

Unaweza ukapika maandazi ukaenda nayo chuo au chapati za maji au vitafunio vyovyote ukawapelekea in campus wanywe na chai asubuhi, kwa idea zingine mbalimbali, cheki hapa.

15. Usipende kukopa sana

16. Kwa waliopo off campus, panga na marafiki mgawane gharama za kulipa kodi
Ishi na wengine mnaopendana ili kusave hela

Na hizo ndio tips 16 za kubudget kwa wale ambao hawana boom.

Kwa wale ambao waliomba wakakosa, usiogope kuomba tena. Kuna rafiki yangu alipata mwaka wa pili mkopo. Kwahiyo hauwezi jua

(bonyeza hapa kufollow akaunti ya Maisha ya Chuo. Akaunti hii inashare dondoo na ushauri unaowasaidia wanachuo kukabiliana na changamoto za maisha ya chuo)

Eunice

3 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »