Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Imani

Apps 2 za simu janja zenye msaada kwako kiroho

 
Mtu wa kawaida anayetumia simu hushika simu yake mara 2617 kwa siku kutokana na uchunguzi uliofanywa na Dscout research.
 
Heri ya sikukuu ya pasaka.

Mara nyingi ikiwa kipindi cha sikukuu kama hivi huwa nina weka malengo ya jinsi gani ninaweza kujiendeleza au kubadilisha jinsi ninavyoishi maisha yangu. Haya malengo huwa natamani yaguse kila kinachohusiana na maisha yangu. Na haswa leo tunapokumbuka kufufuka kwa Bwana na mwokozi wa maisha yetu nimejiwekea malengo ya jinsi ninavyotaka kukua kiroho. Naomba Mungu niyatimize malengo yangu.

Kama watumiaji wengine wa smartphone mimi pia huwa naiwaza, naishika muda mwingi na ninaitumia sana. Na hivi karibuni nimepata kuwaza kuwa kifaa kama hicho ambacho kiko karibu yangu kwa muda mwingi labda kuna njia ya kukitumia vizuri kwa ajili ya kiroho changu tofauti na kunipotezea tu muda, labda kinaweza kunisaidia kukua kiroho.
 
Na muda mwingi ninapoitumia huwa nafungua applications, kama kipindi ambacho nilikuwa natumia mitandao ya kijamii basi nilikuwa nafungua facebook na instagram kwa sana, katika kunisaidia kukua kiroho pia nataka nitumie applications vilevile.
 
Kwa hiyo leo natamani nikushirikishe applications za simu ambazo nazitumia au nimeona wengi wakizitumia au kuzishauri kuzitumia ambazo zinaweza kukusaidia kukua kiroho. Application zote zinapatikana kwenye simu zote za Android na iOS.
 
 
Nimeanza na hii makusudi kwa sababu ninaitumia mara nyingi lakini pia ni muhimu kwa mkristo kusoma Biblia kama nilivyoelezea umuhimu wake hapa. Hii application ya Biblia ni tofauti na nyingine kwa sababu hii haina tu Bibia ila ina Bible plans, ambazo ni devotions za kila siku za mambo mbalimbali kama ni mahusiano, uongozi, ndoa, maisha ya Kikristo,wanawake na kadharika jinsi utakavyopenda wewe kusoma devotion ya aina yoyote, ina vitu vingi vya kusoma na kujifunza kwa Mkristo.

Pia unaweza kujiunganisha na marafiki zako nao ukasoma nao, lakini pia unapata mistari ya Biblia ya kila siku yenye picha ambazo unaweza ukawatumia marafiki zako. Pia unaweza kusoma Biblia kwa mwaka mzima kwani kuna masomo, mistari na alarm ya kukumbusha katika jambo hilo la kusoma Biblia kwa mwaka mzima. Zaidi ya haya yote mazuri kuna tafsiri mbalimbali za Biblia,unachagua ipi unayotaka kuisoma na ipi kwako ni rahisi.Kuna NIV,Swahili Bible, Amplified na nyingine nyingi. Kwasasa mimi natumia Good News Bible Translation.

 
 
Hii ni app nzuri ambayo ninaitumia kila siku, inakusaidia kuomba kwaajili ya nchi na watu wanaopata shida kwa ajili ya imani yao kwa Kristo lakini pia inakupa shuhuda za wale ambao wamepitia shida mbalimbali ambazo unaweza ukawa haujawahi kusikia kwasababu ni mambo ambayo hatukutani nayo sana wakristo wengine.

Kwahiyo hii app inatuonyesha kwa ukaribu gharama na shida wanazopitia wakristo wenzetu kwenye mataifa mbalibali. Kila siku wanaweka nchi ya kuiombea, wanaielezea, lakini pia wanaweka ushuhuda wa kututia moyo kiimani kutokana na mambo ya kishujaa ambayo wakristo hao wamefanya hata katika mateso yao, lakini pia wanaweka interview (podcast) na watu hao au viongozi mbalimbali wa umisheni na wanaeleza mambo wanayokutana nayo.

Hiyo ndio zawadi yangu kwako ya Pasaka, Mungu akubariki sana na ukapate kufurahia kutumia hizi app na zikakusaidie kukua kiroho kama vile nilivyokusudia na ninavyoomba zinisaidie mimi.

 
Eunice
 
 

6 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »