Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Imani

Kwa wanafunzi wakikristo waliopo vyuoni..

Mpaka Mara ya kwanza naenda chuo, sikuwahi kwenda kanisani kwa maamuzi yangu..

Yani kwamba niweke uamuzi na nia ya kwenda, nilikuwa naenda kwasababu ni jumapili, mama anaenda na Mimi niende.

Mara nyingi ukiwa mbali na nyumbani ukaanza kujitegemea, kama vile ukiwa chuo, ndio muda mzuri wa kujua nini unaamini na kwanini unaamini. Na muda wa chuo kwangu ulikuwa kipindi cha ukuaji sana katika imani yangu, na kumjua Mungu Mimi mwenyewe bila kushurutishwa.

Kutokana na peer pressure, na umri huu kuwa wa muhimu sana katika kujitambua, watu wengi huacha kumtafuta Mungu wakiwa chuo.

Kwa upande wangu naona kama ni kipindi nilikuwa karibu sana na Mungu (nilikuwa najishughulisha na mambo yanayomuhusu Mungu), nilikuwa napata muda wa kusoma Neno mwenyewe, nilishiriki mashindano ya Biblia, nilikuwa mwalimu wa watoto kanisani, na Mara kadhaa nilikuwa nikiimba timu ya kusifu na kuabudu ya chapel yetu.

Nimetamani kuwaandikia wanafunzi waliopo chuo, ambao ni wakristo, kwasababu natamani kuwashirikisha machache niliyojifunza kwa kuwa mkristo chuoni, japokuwa siwezi sema nilikuwa mtakatifu sana, lakini nilikuwa natafuta kukua katika mahusiano yangu na Mungu.


Muda huu ni mzuri kumjua Mungu mwenyewe

Mara nyingi tunamjua Mungu kama familia, lakini sasa hivi kwavile upo mbali na nyumbani ni muda wa kukua kiroho mwenyewe kumjua Mungu vyema. Nakumbuka mwanzoni nilipofika chuo nilihangaika kupata kanisa ambalo ningependa kuwa nasali kwa miaka yangu yote, na nilipolipata nikawa committed hapo, ni vizuri ukipata sehemu ya kusali, kushiriki na wenzio pia ni vyema, lakini muhimu ni kuwa na effort personally za kukua katika mahusiano yako na Mungu.


Kujifunza kufanya maamuzi yako mwenyewe

Peer pressure ina nguvu sana pale ambapo hatuna maamuzi yetu wenyewe. Ukiwa chuo ni vizuri kuwa na mipaka, na kujua mambo ambayo unaweza kuyafanya na Yale ambayo huwezi kuyafanya.. Kuwa na maamuzi yako mwenyewe na vile unapenda kuishi maisha yako.

Jitahidi kumuwakilisha Kristo kwa kila unalolifanya. Kuna kuigizia kwenye mtihani, kiukweli naamini hata Neno linasema tiini sheria zilizowekwa, kucheat kwenye mtihani sio vizuri, kudanganya, na mammambo mbalimbali ambayo yanaonekana sio makosa mbele ya wenzio haimaanishi sio makosa kwako kuyafanya. Msikilize Roho Mtakatifu.

Muombe Mungu akulinde na dhambi zituangushazo vijana kwa wepesi

Chuoni watu wengi huamgalia picha za ngono, na hufanya kuwa tabia hii sio tagizo kwasababu tuko chuo. Ulevi, kuishi pamoja nk, yote yanaonekana sawa kwasababu sasa hivi upo chuo. Lakini nirudie tena, sio kila lililosawa kwa watu, ni lazima liwe sawa kwako, muombe Mungu akulinde, ukue katika kumjua Yeye na kukuepusha na mambo yanayotusumbua vijana.

Kutafuta balance kati ya kufanya kazi ya Mungu na masomo

Upo chuoni kutafuta maarifa, yatafute haswa. Kwa kusoma vitabu, kuangalia documentary nk, tumia muda uliopo chuo kujifunza pia kuhusu dunia inayokuzunguka.

Katika unafanya kazi za Mungu ukiwa chuo, kumbuka kuwa, unazifanya kazi hizi chuoni kwasababu we we ni mwanafunzi wa hicho chuo, tafuta balance katika kusoma kwako na kumtumikia Mungu ili usije ukafeli ( ukasupp au ukadisco), kitu ambacho kitakupa shida kwenye utumishi pia.


Wewe ni nuru, ni chumvi, ni muwakilishi wa Yesu hapo ulipo.. Simama kwenye nafasi yako ipasavyo.

Eunice

Makala nilizoona zinaweza kukusaidia pia :

1. Three lessons for Christians to learn in college

2. Christians in College

3. Why students lose their faith in college

4. Lies that Christians in college believe

One Comment

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป