Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Jinsi ya kujilinda dhidi ya virusi vya Corona

Wakati Coronavirus inaanza sikuwa naogopa sana nikijua kuwa watapata dawa na janga litaisha.

Ila mpaka sasa tulipofika ugonjwa umekuwa mkubwa, na naona nchi nyingi zikiguswa na huu ugonjwa. Kwa kufuatilia tu mitandaoni naona wapo wanaopona na nchi na viongozi wanaweka jitihada sana, madaktari wanaweka nguvu nyingi katika kutoa huduma za afya na wanasayansi katika kutafuta tiba. Haya yote ni mema na yanatupa tumaini, ila pia kuna mambo ambayo wewe mwenyewe unaweza kuyafanya kujilinda ili usiupate, mambo hayo ni;

Kupunguza kukaa kwenye mikusanyiko ya watu wengi

Jambo moja ambalo linaniwazisha kuhusu virusi vya Corona, ni athari yake haswa kwenye sehemu zenye msongamano wa watu. Nawaza kwenye utumiaji wa daladala hasa mimi mkazi wa Mbagala, lakini jambo moja unaloweza kulifanya ni kupunguza safari zisizo za lazima za sehemu zenye msongamano na hata kuacha kupanda mabasi yaliyojaa sana (ngumu ila ndio kujilinda).

Kutoshikana na watu na kutokujishika wewe mwenyewe (kaa mbali na watu)

Kupunguza kushikana mikono na watu na kushika sura yako. Kwa wale tuliozoea kupeana mikono na watu huko duniani sasa hivi wanapeana viwiko au miguu. Kaa mbali na watu kipindi hiki.

Nunua mahitaji ukae nayo ndani

Ili kupunguza safari za sehemu zenye mikusanyiko unaweza kununua vyakula na kukaa navyo ndani ili upunguze safari za sehemu za watu wengi.

Kunawa mikono mara kwa mara

Utashangaa ni vitu vingapi huwa tunavigusa kila siku, sasa kipindi hiki cha virusi hivi ni wangapi pia wameshika unapopashika wewe? ( Mabomba au viti vya daladala).

Jambo rahisi ni kunawa mikono kwa maji mengi kila unapofika nyumbani ili kutoingia na virusi ndani.

Kuziba mdomo unapokohoa au kutokaa karibu na wanaokohoa (na kupiga chafya)

Unapokohoa usizibe mdomo kwa kiganja bali sehemu karibia na kwapa, lakini pia kwa vile wengi hukohoa pia jizibe kwa kutumia mask unapokua sehemu za watu wengi.

Unapopanga kutoka uwe umejipanga tayari kujilinda, vaa nguo za kujilinda, vaa mask na kuwa mwangalifu wakati wote.

Kwasasa haya ndio mambo niliyofanikiwa kuyasoma ya jinsi ya kujilinda. Naamini itakuja kuisha na Mungu atatuvusha salama katika kipindi hiki ambacho dunia inapitia hili.

Unajilindaje dhidi ya virusi vya Corona?

Eunice

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป