Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Kwa waliochaguliwa course ambayo hawaipendi

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Wakati naapply vyuo, sikujua nataka nisome course gani..

Nakumbuka nilikuwa jeshini.

Nikapiga simu nyumbani kwa mama, alikuwa kazini, mfanyakazi mwenzie akatoa ushauri wa chuo niapply.. Nikakijaza.. Nakumbuka alisema,’ kuna chuo Mbeya, jaza hata Mechanical ina market sana’. Nikajaza.

Nilisoma PCM.

Ila nilipenda kusomea psychology.

Nikajaza UDOM nk..

Na mechanical nikawa nimeijaza ya mwisho.Nikiwa sina uhakika wa kupata.

Nikiwa nimejaza ili tu nijaze sehemu tano za fomu ya kuapply.

Majibu yakatoka nikawa nimechaguliwa Mechanical Engineering.

Mara ya kwanza nilifurahi, kwasababu nilipata chuo.

At least nimepata chuo.

Nikawaza nikasema niende TCU kubadilisha, na nakumbuka nilifika hadi TCU. Ila nilipofika nakuona process ni ndefu, lakini pia nilikuwa sijui nahitaji nini kwenye maisha nikaona labda nitaipenda hii course na labda hii ndio njia ambayo nilipangiwa kwaajili ya maisha yangu.

Nikajitia moyo na kukubali course niliyochaguliwa.

Nikafika chuo, nikiwa na rafiki ambaye nilisoma naye high school nikijua kuwa tupo course moja.. Alikuwa akinipitia twende darasani, nikafurahia kampani.

Baada ya wiki chache akaniambia anahama course kwenda Civil Engineering.

Nikabakia peke yangu Mechanical.

Nikapata marafiki wapya, nikaenjoy Mbeya, nika make memories, nika have fun, nikasafiri, nikafaulu darasani, nikawa na maisha kwa miaka yote minne niliyokuwa chuo…

Lakini miezi ilikuwa haipiti bila kujiuliza kwanini nasoma Mechanical?

Bila kuwaambia marafiki zangu vile hii sio njia ya maisha yangu, vile natamani kufanya mambo mengine na maisha yangu..

Bila kusafiri na kufanya kazi za jamii ambazo nazipenda. Nakumbuka mwaka wa tatu nilijitolea na organization ambayo nilikuwa inafanya kazi za social work.. Kitu ambacho ndio nikagundua ni passion yangu.

Nimemaliza chuo, miezi ya mwanzo ya kumaliza chuo nilikuwa najilaumu kwanini nilisoma Mechanical, kwanini nisingechukua hata mwaka mmoja wa kufikiria kitu gani napenda, au hata kubadilisha course nakusoma course ninayoipenda..

Au kwanini sikujua kitu ninachokipenda mapema?

Nimefaulu vizuri, ila kwa degree ambayo sipendi kuifanyia kazi…

Kwa degree ambayo sipendi sana kujitambulisha niliisomea maana natamani watu wanijue kwa mambo ninayoyapenda.

Na kuwa Mechanical engineer ni achievement kubwa sana, watu wengi hushangaa na kushtuka wakijua kuwa Mimi ni Engineer, lakini kwangu naona cha kawaida kwasababu sikuwa na moyo nayo, kwasababu nilikuwa navumilia niimalize, niendelee na mambo ninayoyapenda.

Na sasa sijui kama nitasomea mambo ninayoyapenda masters au nitaendelea kufanya kazi za jamii ninazozifanya bila vyeti mpaka nitakapozeeka.

Ananiinspire master Jay, alisoma Electrical Engineering, Ila anajulikana kwa kufanya kitu kingine kabisa. Maybe nami nitakuwa hivyo ama sivyo…

Ila kwa uliechaguliwa course ambayo hauipendi..

—Inawezekana njia yako ni kama ya Master Jay.. Au yangu.. Kwamba utagundua unachopenda au unachopaswa kufanya baadae…

—Au njia yako ni kupumzika mwaka mmoja (gap year) ili usipoteze miaka minne wakati ushajitambua..

—Au njia yako ni kubadilisha course, kutokuifanya kwasababu unadhani inalipa, kutokuifanya kwasababu unaona process ya kubadilisha ni ndefu..

Kwa lolote utakaloamua, I hope utafanya uamuzi mzuri kwaajili ya maisha yako.


(Naomba niseme kuwa hii ni stori ya maisha yangu na sio kwamba ndio majibu ya wote waliochaguliwa course ambayo hawaipendi, ningependa tu kushare stori yangu)

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate »