Kwa vile ugonjwa huu bado mpya, ingawa sio sana, kuna vitu vinaendelea kugunduliwa kuuhusu. Kwahivyo hata dalili nitakazoziorodhesha zitakuwa zile ambazo tumekuwa tunazisikia mara kwa mara mpaka sasa.

Mpaka sasa kuna wale ambao wanaweza kuupata na wasioneshe dalili yoyote ile, na kuna wale ambao wanaonesha dalili.

Kwasasa cha muhimu ni kujiangalia kama una dalili hizi na kujipeleka kwenye vituo vya afya, kujilinda kwa kukaa mbali na wenye dalili hizi lakini pia kuwaripoti kwenye vituo vya afya watu unaowadhania wana maambukizi.

Dalili zenyewe za kujua kama una maambukizi ya virusi vya Corona ni:

– Homa

Kikohozi

Kupata shida kupumua (pumzi)

Dalili nyingine ni;

Nimonia

Figo kufeli

Kwasasa hizo ndio dalili nilizopata kuzijua kuhusu Corona. Kwa vile wataalamu wanaendelea kuusoma tutazidi kujua zaidi ila kwasasa chukua hatua hizi kujilinda dhidi ya virusi vya Corona.

Eunice

You May Also Like

Share Your Thoughts With Me

Translate »