Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha,  Maisha ya kila siku

Mambo ya kuzingatia unapomfuata mtu inbox

Au kichwa cha makala kingekuwa : Mambo ya kufanya kabla haujaeleza shida yako unapomfuata mtu inbox | Jinsi ya kumshawishi mtu unapomfuata inbox


Unapomfuata mtu inbox iwe WhatsApp, kwa message, au DM jua kuwa unamfuata mtu mwenyewe, kwenye nafasi yake binafsi.

Nakutana na wengi ambao anakuja tu inbox na kunitumia link, au anakuja kunitumia sticker za WhatsApp yenye ujumbe ‘sub for sub’ au anakuja kuniambia ‘save for save’, hakuna ubaya wowote kwenye hizi jumbe ila haujakamata bado umakini wangu kwahiyo siwezi nikakuchukulia serious.

Chukulia kumfuata mtu inbox kama kukutana na mtu kwenye networking event au kukutana naye barabarani.

Hauendi moja kwa moja kama vile yule mtu anawajibu wa kukujibu unaenda kwa kuheshimu muda wake kwanza.

Mambo ya kufanya unapomfuata mtu inbox ni:


1. Usimpigie kama amechelewa kukujibu

Bado hamjuani. Kumpigia mtu simu ni jambo la ukaribu sana muda mwingine, hasa kwa video.

Kama umemfuata inbox na hajakujibu na una haraka kumpigia simu na kuanza kujieleza kuwa wewe ndio ulituma message inaweza isilete ujumbe mzuri kwa yule mtu maana anaweza akaona unampelekesha kusoma message yako, na ikakuharibia mahusiano hata kabla hayajaanza.

Video ndio sio poa kabisa maana hakujui, humjui, kwanini unadhani atapokea akuonyeshe sura yake?

2. Jitambulishe

Usitume moja kwa moja ujumbe ulionao hata kama ni mzuri kiasi gani bila kujitambulisha.

Wewe ni nani, umetoa wapi number, kama kuna mtu anamjua nawewe unamjua nk.

Bado hamjuani hakuna anayependa kujibu watu ambao hawajui. Siku zimebadilika🤣🤣

Usitume tu DM ‘nipe number yako, kwani vibaya kukupigia?’ 🙄🙄 NDIO, SIKUJUI.

3. Onyesha interest na yule uliyemfuata

Kama unamfahamu mwambie unamfahamu vipi, onyesha kuwa una interest naye isiwe tu umemfuata inbox kwa shida zako.

Ila kama haumfahamu, muulize nayeye aongee kuhusu yeye, watu hupenda kuongea kuhusu wao, hii itakufanya umshawishi kiurahisi.

4. Kuwa kiofisi hasa kama haumjui

Nimepata text nyingi kutoka number mpya na mtu ananitext, ‘vp’.

Yani number mpya, ila pia hata sentensi sio kamili, haimshawishi mtu kukuchukulia serious kwa lolote unalotamani kulisema.

Ongea lugha ya kiheshima, na ongea kwaajili ya kueleweka.

5. Acha ego yako nje ya inbox

Ukimfuata mtu inbox usiingie na majivuno, jishushe. Unahitaji kitu, yeye ni mteja wako au lengo lolote ulilonalo la kumfuata inbox..

Nimekutana na mtu unaongea naye na anajivuna na kukudharau hata kabla hajakuambia kwanini amekufuata, au ukimkatalia analolitaka anatoa maneno ya dharau mpaka unajuta kwanini ulimpa muda wako. ‘nilijua tu unadharau’ 🙄🙄 SASA KAMA ULIJUA KWANINI UMENITAFUTA?

Mtu akikupa muda uheshimu, akikujibu, heshimu hilo, na haumdai attention kwahiyo usiidai, akikukatalia pia kumbuka hauumdai ndio. Haumdai chochote.


Ongea na uliyemfuata kwa kumuonesha interest hata kabla haujasema unalolitaka, akiwa huru kihivyo kwako unaweza kumshawishi kwa lolote kiurahisi. Na akikataa pia ni sawa.

Siongelei uwe muongo ufeki urafiki naye ili baadae akupe unachotaka, ila naongelea jinsi ya kukamata attention yake kabla haujaeleza shida yako unapomfuata inbox.


Mambo gani yamekusaidia unapomfuata mtu inbox?

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป