Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya kila siku

Faida na Hasara za kuishi katikati ya mji

Hivi karibuni haswa kumekuwa na watu wengi wanaohamia sehemu za mbali kidogo na mji, kwasababu mbalimbali.. Ila pia haimaanishi kuwa hakuna wengine pia wanaohamia mijini, kwa vile bado sijapata tafiti inayochunguza uhamiaji ni ngumu kujua ni asilimia ngapi wanahamia mijini, asilimia ngapi wanajisogeza kando na mbali na miji.

Kama utapenda kujua kwanini watu wengi wanahamia / au kujenga mbali na mji, bonyeza hapa kusoma makala niliyoelezea faida na hasara za kukaa nje ya mji ila kwenye makala hii ningependa nishee faida na hasara za kuishi katikati ya mji kwasababu nimeishi katikati ya mji kwa miaka mingi kabla ya kuhamia mbali na mji.. na hizi hapa ni faida za kuishi katika ya mji.

Faida za kuishi katikati ya mji

1. Upatikanaji wa huduma za kijamii kwa haraka na urahisi.. Huduma za kijamii kama vile ofisi nyingi, hospitali nzuri nk zinapatikana haraka ukiishi mjini lakini pia zinafikika kwa haraka tofauti na ukikaa nje ya mji.

2. Kuna bidhaa ambazo unazinunua kwa gharama nafuu zaidi maeneo haya. Kuna bidhaa kama vile mboga za majani, zinakuwa gharama nafuu nje ya mji kwasababu ya uwezekano wa kuwa zinalimwa huko, ila bidhaa nyingine inakuwa rahisi ukizipata mjini kuliko nje ya mji maana wauzaji hupandisha bei ya hiyo bidhaa ili kulipia gharama za nauli za kuisafirisha bidhaa hiyo mfano vitu vya kielectroniki au vinavyotengenezwa kwenye viwanda vilivyopo mjini.

3. Miundo mbinu ipo vizuri, kama ni barabara nk viko vizuri na vimetumika kwa muda mrefu tofauti na ukiishi nje ya mji

4. Kuna kuwa kumechangamka, maswala ya sherehe, sehemu za starehe nk nyingi ziko maeneo ya mijini na zimechangamka. Ukitaka wikiendi uende sehemu zipo nyingi tu, tofauti na nje ya mji ambapo kuna kuwa kumetulia kidogo hakuna fujo nyingi za mji ambao unachelewa kulala.

Hasara za kuishi katikati ya mji

1. Hali ya hewa inakuwa joto kidogo, hivi ni mimi tu au nje ya mji kuna upepo mwanana?

2. Kelele, yani fikiria kuishi Kariakoo, halafu fikiria kuishi Chanika.. kelele zinazopatikana sehemu hizi mbili ni tofauti.

3. Gharama za vyumba/ nyumba zinakuwa juu. Ukipanga chumba sehemu kama Vikindu, na ukapanga sehemu kama Mwenge gharama zao ni tofauti sana. Gharama za kukaa katikati ya mji ni kubwa sana, kwa chakula, , vyumba na usafiri. Kwenye usafiri, liangalie kwa jicho hili; ukipanda bodaboda maeneo ya Posta na Vikindu, Vikindu gharama itakuwa ya chini kwa umbali mrefu, tofauti na Posta..

Na hizo ndio faida na hasara ninazoziona kwenye kuishi katikati ya mji.. Je kuna zipi unazozifahamu na sijazitaja kwenye makala hii? Niambie kwenye comment.

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป