Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Hisia 2 utakazozisikia unapoenda kuanza chuo mwaka wa kwanza

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Bado nakumbuka siku nilipofika Mbeya tayari kuanza mwaka wangu wa kwanza.

Nakumbuka nilivyoamka asubuhi baada ya kuingia Mbeya usiku sana na kulisikia lile baridi ambalo ndio litakuwa part ya maisha yangu kwa miaka minne ijayo.

Bado nakumbuka nilivyokuwa napelekwa chuo, na tukapita barabara kuelekea geti kuu la chuo cha Mbeya University of science and technology, harufu nilizozisikia, vile nilivyojisikia na vitu nilivyoviona.

Siku ile ilikuwa moja ya siku nzuri na ya kukumbukwa kwenye maisha yangu.

Mwezi huu unapokaribia kwenda chuo kwa Mara yako ya kwanza na tayari kuanza maisha mapya kwa miaka mitatu/minne/ mitano ijayo, natamani nikushirikishe hisia ambazo unaweza kuzisikia unapoenda chuo kwa Mara ya kwanza:

1: Excitement

Unakuwa excited, maisha mapya unaenda kuyaanza. Ambayo yatakubadilisha sasa unakaribia kuwa adult. Unaendea experience mpya. Siunajua vile tukiwa vidato vya chini tunalenga kwenda chuo, na sasa ndo unaelekea huko tulipokuwa tunadream kwenda – chuoni. Excitement, huwezi kuicontain. Lazima utafeel excited.

2 : Fear of the Unknown

Haujawahi kuishi hayo maisha hapo kabla, ndio Mara ya kwanza unaenda chuo, kuwa huru, kumake new friends na kusoma masomo mapya na course ambayo inaweza ikadirect maisha yako yajayo, of course unaogopa. Unaogopa kwamba labda unaweza ukafeli, unaogopa labda yatakushinda, yatakuwa magumu, peer pressure, unaogopa, unaogopa mengi ambayo unayawaza sasa hivi.

Hivi ndo natamani Eunice aliyekuwa anaenda chuoni mwaka 2014 angejua – ‘you will be okay, yes, mambo ni magumu au yatakuwa magumu lakini you are a conqueror, you will make it through”.

Na hicho ndicho ninachokuambia Leo wewe.

Usiogope kwamba haujui hiyo miaka mitatu au zaidi ijayo itakuwaje, usianze kuogopa. Labda kutokujua ni jambo zuri, kwasababu katika kutokujua Kuna mema. What if usichokijua ni chema na sio kile unachofikiria kuwa kibaya? Kwa vile hujui that means Kuna possibility. Kuna possibility ya mambo mema kutokea, what if you fly??

(Kuna watu wengi mnaniuliza maswali mbalimbali kuhusu maisha ya chuo, mkiwaza mtadeal vipi na peer pressure na mambo mbalimbali kuhusu maisha ya chuo, usiogope, unaweza subscribe kwenye channel yangu ya maisha ya chuo kwani ninashare tips, ushauri na kujibu maswali mbalimbali kuhusu maisha ya chuo na kukusaidia ili wewe pia ufaulu na kuenjoy maisha yako ya chuo kama vile Mimi nilivyoyafurahia yangu – Subscribe hapa )

Instagram @maishayachuo

Kama unaswali lolote kuhusu maisha ya chuo usisahau kuniuliza kwenye email – (hie@abiblegirl.com), au comment hapa.

Eunice

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Share Your Thoughts With Me

Translate »