Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maisha ya Chuo

Things I wish every first year student should know (Part 1) | Your Guide to University Life

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


(Mambo ninayotamani kila mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ayafahamu)

Katika kila hatua mpya ya maisha kuna mambo usiyoyajua kwa sehemu, ambayo ukiyajua na kuzingatia kwa asilimia kubwa yatakuwezesha kuwa na matokeo bora ya maisha tofauti na asiyeyajua kabisa.

Katika Makala hii nataka kuzungumza na mwanafunzi mpya wa chuo kikuu na hata wale wanaoendelea na masomo pia watajifunza.

Katika Ujumbe huu nimetumia lugha mbili KISWAHILI na ENGLISH naamini wanafunzi wote kwa level hii mtaelewa.

Katika safari yangu ya kielimu nikiwa chuo kikuu mpaka nilipomaliza, yapo Makosa mengi sana nilifanya, pia yapo mambo mengi sikufanikisha kama nilivyotarajia na yapo mambo mengi niliyafanikisha kama nilivyotarajia na hata zaidi ya matarajio.

Mjumuiko huo wa uzoefu (experience) nilioupata katika maisha yangu binafsi na hata kupitia watu wengine chuoni ulinifundisha mambo haya kadhaa katika mengi ambayo natamani kila mwanachuo ayafahamu mapema aanzapo safari yake ya chuo kikuu.

1 . KILA MATOKEO UYAPATAYO KATIKA KILA SOMO NI YA KUZINGATIA.
(Every Results you get in every Subject/course matters)

Tofauti na ngazi za Primary na secondary ambapo jitihada zote zinalenga kufaulu mitihani ya MWISHO (Annual exams, National exams au International final exams). Huku chuoni kila quiz, tests, assignments, presentations hadi kufikia end of semester Exam vyote kwa pamoja vinachangia matokeo yako ya MWISHO. (Kila matokeo ni ya muhimu).
Kwa kulijua hili ni muhimu kufanya kwa ufanisi kila kazi kwasababu inachangia matokeo yako ya mwisho.

Kule secondary na Primary ilikuwa ukifeli Midterm au weekly test ni rahisi kujipa moyo kuwa unasomea NECTA au utarekebisha kwenye mtihani wa MWISHO.
Na kweli ukifaulu vizuri NECTA ufaulu wote wa mitihani iliyopita hauna madhara tena.

Ila huku chuoni kila unachofeli kinakurudisha nyuma na kila unachofaulu kinakuinua kwasababu matokeo ya MWISHO yanayategemea hadi yale ya mwanzo pia. JIPANGE.

2 . BEING A STUDENT GIVES YOU FAVOUR.
(Uanafunzi ni dhamana)

Ukiwa mwanafunzi na katika jamii ya wasomi wenzako, ni rahisi sana kujichukulia poa, na kujiona wa kawaida kwasababu hauoni utofauti na waliokuzunguka Chuoni.

Lakini kiukweli, ni watu wachache sana kulinganisha na idadi ya mamilioni ya watanzania ndio mmefanikiwa kufika ngazi ya chuo kikuu. Hivyo jamii inawaamini sana wasomi na inatarajia mchango chanya kutoka kwako kwasababu tu ya elimu yako.

-Mwanafunzi ni rahisi kuaminika katika shughuli yoyote kwasababu mwamvuli wa chuo chako unakulinda.
Inaaminika hata likitokea la kutokea pakukupata panajulikana (chuoni).
Hivyo tumia mwamvuli huo kama dhamana ya kufanikisha mambo yote mazuri unayotaka kuyafanya.

Mfano, katika kujifunza.
Kwa kutumia mwamvuli wa uanafunzi, ni rahisi hata kwenda kujifunza jambo kwenye ofisi yoyote ukijitambulisha tu kuwa ni mwanachuo, tayari umefungua mlango wa wewe kusikilizwa, kuelekezwa na kuaminika. Tofauti na mtu wa kawaida kutoka mtaani, kwasababu itahitaji kujiridhisha vizuri kwanza kuhusu nia yake, nk.

Nakumbuka nina rafiki yangu mmoja alikuwa anashughulikia usajili wa kikundi chao flani cha wanafunzi cha ujasiriamali. Alipofika katika mamlaka husika alisaidiwa na kuhudumiwa kwa ukaribu sana kwasababu kila mtu alivutiwa na kuona vijana wadogo wanafanya mambo makubwa. Kwasababu tu ni wanafunzi. (Huenda wapo wanaofanya kama hayo huko mtaani, ila kwao ingeonekana ni kawaida)

Leo hii Kuna activities nyingi na fursa nyingi sana zimeelekezwa kwa wanachuo. Kuna Semina za bure za kujifunza mambo mbalimbali kwa wanachuo, Mitandao ya simu imeweka unafuu wa huduma kwa wanachuo, Bima za Afya zina gharama nafuu kwa wanachuo,nk.

Uanachuo ni dhamana Itumie vizuri. IKIPITA, IMEPITA.

3 . BUDGETING AND SAVING ARE HABITS TO HAVE, FOR A SUCCESSFUL FINANCIAL LIFE IN CAMPUS
(Kuweka AKIBA na kujipangia Bajeti za fedha ni tabia za muhimu sana kuwa nazo uwapo chuoni).

BAJETI.
Ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha katika kipindi fulani ili kuhakikisha mipango inafanikiwa kwa wakati uliotarajiwa.
Huu ni mpango wako wa matumizi ya rasilimali fedha unaokupa Dira na Mipaka yako katika utumiaji wa pesa uwapo chuoni.

Kiukweli watu wengi hawana tabia ya kupanga bajeti. Wanatumia pesa wanavyojisikia katika jambo lolote litakalojitokeza.

Na kiuhalisia kupanga bajeti si jambo lenye raha saana kwasababu unapingana na matakwa yako na inahusisha kujikana mwenyewe kwa kujikosesha unayoyataka ili upate unayoyahitaji.

Hapa unapanga matumizi yako kwa kuzingatia kiasi cha pesa ambacho una uhakika wa kukipata ndani ya muda husika.
Hii itakuepusha na maisha ya kukopa kusiko na ulazima, kukumbwa na Uhitaji bila kutarajia, kushindwa kukabili dharura zinazohitaji pesa na pia itakuwezesha kuishi maisha yenye uhalisia na yasiyo na frustration.

AKIBA
Kwa lugha rahisi akiba ni kitu kilichotengwa kwa ajili ya manufaa ya baadaye.

Hapa tunaongelea akiba ya fedha. Unatenga kiasi fulani cha pesa uliyoipata kwajili ya manufaa ya baadae.

Ni muhimu kujua kuwa hautapata kiasi kile kile cha pesa kila siku uwapo chuoni, hujui kesho itakuja na Uhitaji gani (shida hazigongi Hodi na hazina huruma), pia kuna maisha wakati wa likizo yanayohitaji fedha, na zaidi sana kuna maisha baada ya chuo yanayohitaji fedha pia.
Pia, Uwekaji wa akiba ni Miongoni mwa njia kwajili ya kulimbikiza fedha ili kukuza mtaji wa kufanyia uwekezaji unaoutaka.

-Kuweka akiba itakusaidia kuikabili kesho kwa furaha.
-Hakikisha unajifunza zaidi kuhusu akiba (Makala hii haitoshi).
-Nashauri Tenga angalau 10% au zaidi ya kila kiasi unachoingiza kiwe akiba. Kulingana na lengo, uhitaji na kipato chako.
-Zipo aina nyingi za akiba, na namna nyingi za kuweka akiba kimkakati. Nenda kajifunze zaidi.
(Kupitia watu sahihi, Vitabu, Mitandaoni,Semina,nk)

Japo ni vigumu kufanya haya lakini wepesi wake unaanzia pale utakapoamua kwa dhati kuyafanya.

Upangaji wa Bajeti na uwekaji wa Akiba, ni tabia kama ilivyo tabia nyingine yoyote. Hivyo hata asiye nayo anaweza kujifunza na kuianza hadi ikawa tabia yake kama wengine.

Angalia : Idea za Biashara unazoweza kuzifanya ukiwa chuoni

4 . ALL OPPORTUNITIES PASSING YOUR WAY, WILL RARELY OR NEVER REOCCUR.
(Kila fursa inayopita mbele yako ni vigumu kujirudia au haitojirudia kabisa.)

-Its true that we are not designed to grab every available opportunity. But we are supposed to grab every opportunity that is ours.
( provided it is Aligning with our standards, It doesn’t take us away from focus , it adds something in our life and adds value in what we are doing,etc)

-Tukianza na fursa hiyo kuu ya kusoma unachokisoma sasa. Haitojirudia. Hata ukirudia kwa wakati mwingine bado wakati utakuwa tofauti. Na kila wakati na baraka zake. HIVYO DON’T TAKE IT FOR GRANTED.

-Tukija fursa nje ya masomo pia zipo nyingi. Kuna mambo usipoweza kuyafanya ukiwa mwanafunzi ni vigumu kuyafanya ukiwa mtaani.
Mfano;-
Ukipata nafasi ya kushiriki michezo na unaiweza, shiriki. Ukipata nafasi ya kugombea uongozi na unaweza, gombea. Ukipata nafasi ya kwenda mbuga za wanyama na muda wako na bajeti vinaruhusu, nenda. (Maana gharama zaweza kuzidi ukiamua kwenda mwenyewe baada ya kuhitimu). Ukipata fursa ya kujifunza jambo jipya uwapo chuoni, jifunze.
Hayo na mengine meeengi.
Fahamu,
(Kila fursa nzuri IKIPITA IMEPITA, ILA HAKIKISHA INAPITIA KWAKO)

-Cha msingi hapa ni kuzingatia kutumia fursa zote za kujifunza, za kufanya kitu, za kufika mahala, za Kushiriki kitu,nk ambazo zimekukuta ukiwa chuoni.
Ukishafika mtaani. Maisha yanakutreat tofauti, maisha yanakudai wewe na mchango wa elimu yako.

Itaendelea……

Instagram : Prepare for University

Adam Machalila

Founder – Prepare for University

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

5 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »