Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Njia 3 rahisi za kuwa na furaha kila siku

Kwenye dunia ya sasa ambapo inaonekana kila siku kuna kitu kipya cha kutuondolea na furaha, ni lazima tutafute namna ya kujipa furaha la sivuo tutajikuta tunaishi siku zetu nyingi kwa hasira, manung’uniko, kwa ukosefu wa amani ya moyo na vilio. Kama unapenda kuwa na furaha, hizi hapa ni njia 3 rahisi kabisa ambazo ninazitumia ili kujipa furaha kila siku;

– Fanya jambo moja unalolipenda au unalojua linakupaga furaha mfano; kula chakula unachokipenda, mpigie unayempenda nk

Vitu kama hivi kwa siku vinakufanya upate muda mchache wa kuwa na furaha. Kwa muda huo unapovifanya unapata furaha.

– Usiingie kwenye kila ugomvi chagua ugomvi unaotaka kuingia

Ujue kuna watu wengine tunagombanaga nao halafu kulikuwa hakuna ulazima wa sisi kugombana nao. Kwa mfano asubuhi asubuhi unaanza kugombana na konda labda au mtu aliyekunyaga kwa kitu ambacho hakikuwa kikubwa kwa ugomvi huo. Jitahidi kupunguza malumbano, watu wengine nafsi zao ziko juu juu tu kila wakati ila kwa vile wewe unatafuta furaha chagua ugomvi unaohisi unafaa wewe kuingia, na mara nyingi unakuta mengi sio ya msingu wewe kugombana na watu kwayo.

Pia Soma : Mambo ya kufanya asubuhi ili uanze siku vizuri

– Tumia muda mchache kwenye mitandao ya kijamii

Kama kuna sehemu ambapo unaweza kuona mabaya na mazuri yanayoendelea duniani kila siku, saa na dakika ni mitandao ya kijamii. Watu waliofanya uchunguzi wamegundua kuwa matumizi ya muda mrefu ya mitandao ya kijamii yanaweza kusababisha hata sonona. Kuona kila siku watu wanavyojisifia na maisha yao, kunaweza kukufanya wewe uwe na huzuni na vile maisha yako yanavyoenda. Ukipunguza muda unaotumia mitandao ya kijamii na kuongeza muda unaotumia kuongea na watu au kwenye uota wa asili inakusaidia sana kukuongezea amani na furaha kwenye maisha.

Hizo ndio njia 3 rahisi zinazonisaidia kuwa na furaha kila siku. Ni njia gani wewe hujipa furaha kwenye maisha? Niambie kwenye comment

Naomba u-subscribe kwenye channel yangu ya YouTube ambapo nitakuwa naweka video zenye dondoo mbalimbali za maisha na kuongelea vitabu, afya, fedha, mahusiano nk

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป