Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya kila siku,  Random

Ukipata kazi, usinunue gari kwanza

Najua wengi ndio ndoto yetu, na ndio njia ya wengi..

Kupata kazi

Kukopa mkopo wa gari

Kununua gari

Mshahara utalipia deni taratibu.

Hata mimi ndio nilikuwa nafikiria kufanya hili hili, lakini siku zinavyozidi kwenda naanza kupata mawazo mengine.

Najua kwanini tunanunua gari kwanza
Ni alama ya mafanikio, na nani hapendi kuonekana ameshafanikiwa?

Ni njia rahisi ya usafiri, na nani hapendi usafiri wake mwenyewe aende popote anapotaka na kurudi kwa wakati wake?

Ni formula ya maisha, ukipata kazi nunua gari, gari linaonyesha kuwa una kazi, kuwa umeshafika na gari ni hatua moja wapo ambayo unatakiwa utick kwenye mambo yako ya kufanya maishani.

Lakini kuchukua mkopo ili kutimiza haya haswa baada tu ya kupata kazi inakuingiza kwenye madeni wakati bado haujajua system ya kazi ipoje, inakuingiza kwenye madeni yatakayokufanya uendelee kubaki kazini hata hauipendi kazi ili kuyalipa kwa muda.

Ndio, inaweza ikatokea kazi hauipendi, inaweza ikatokea ukawa sehemu yenye stress, inaweza ikatokea ukafukuzwa,ukaona uhame, ujiajiri au uache kazi.

Gari linahitaji matengenezo, linahitaji mafuta, linahitaji uangalifu.

Mkopo utalipia gari, na mshahara utalipia mafuta na matengenezo ya gari na kulipa deni.

Mimi ni kati ya watu wanaoogopa sana mikopo.. hasa ambayo inakuingiza kwenye system ya kuwa mlipaji kwa muda mrefu na haijakuletea faida yoyote.

Lakini kama unataka kukopa, kwanini usinunue ardhi?

Kwanini usianze kujenga mapema, hata nyumba kwaajili ya kupangisha?

Kama unatamani usafiri kwanini usifikirie pikipiki kwanza kwa mfano, ambao ni bei ya chini kidogo kuliko gari?

Au kwanini usianzishe biashara ambayo itakuzalishia hela ya kulipia mkopo na ukalipia na deni ulilokopa?

Kwanini gari liwe cha kwanza?

Unaweza na unaruhusiwa kununua hata baadae, hakuna limit ya muda.

Eunice


(Siko against kuwa na gari, nipo against kuwa na gari kwaajili ya kujionesha umefanikiwa kwa watu, ambao kwa wengi wanaopata kazi hiyo ndio motivator ya kwanza ya kununua gari lakini tunasingizia ni kwaajili ya usafiri)

8 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป