Najua wengi ndio ndoto yetu, na ndio njia ya wengi..

Kupata kazi

Kukopa mkopo wa gari

Kununua gari

Mshahara utalipia deni taratibu.

Hata mimi ndio nilikuwa nafikiria kufanya hili hili, lakini siku zinavyozidi kwenda naanza kupata mawazo mengine.

Najua kwanini tunanunua gari kwanza
Ni alama ya mafanikio, na nani hapendi kuonekana ameshafanikiwa?

Ni njia rahisi ya usafiri, na nani hapendi usafiri wake mwenyewe aende popote anapotaka na kurudi kwa wakati wake?

Ni formula ya maisha, ukipata kazi nunua gari, gari linaonyesha kuwa una kazi, kuwa umeshafika na gari ni hatua moja wapo ambayo unatakiwa utick kwenye mambo yako ya kufanya maishani.

Lakini kuchukua mkopo ili kutimiza haya haswa baada tu ya kupata kazi inakuingiza kwenye madeni wakati bado haujajua system ya kazi ipoje, inakuingiza kwenye madeni yatakayokufanya uendelee kubaki kazini hata hauipendi kazi ili kuyalipa kwa muda.

Ndio, inaweza ikatokea kazi hauipendi, inaweza ikatokea ukawa sehemu yenye stress, inaweza ikatokea ukafukuzwa,ukaona uhame, ujiajiri au uache kazi.

Gari linahitaji matengenezo, linahitaji mafuta, linahitaji uangalifu.

Mkopo utalipia gari, na mshahara utalipia mafuta na matengenezo ya gari na kulipa deni.

Mimi ni kati ya watu wanaoogopa sana mikopo.. hasa ambayo inakuingiza kwenye system ya kuwa mlipaji kwa muda mrefu na haijakuletea faida yoyote.

Lakini kama unataka kukopa, kwanini usinunue ardhi?

Kwanini usianze kujenga mapema, hata nyumba kwaajili ya kupangisha?

Kama unatamani usafiri kwanini usifikirie pikipiki kwanza kwa mfano, ambao ni bei ya chini kidogo kuliko gari?

Au kwanini usianzishe biashara ambayo itakuzalishia hela ya kulipia mkopo na ukalipia na deni ulilokopa?

Kwanini gari liwe cha kwanza?

Unaweza na unaruhusiwa kununua hata baadae, hakuna limit ya muda.

Eunice


(Siko against kuwa na gari, nipo against kuwa na gari kwaajili ya kujionesha umefanikiwa kwa watu, ambao kwa wengi wanaopata kazi hiyo ndio motivator ya kwanza ya kununua gari lakini tunasingizia ni kwaajili ya usafiri)

You May Also Like

8 thoughts on “Ukipata kazi, usinunue gari kwanza

 1. Victor Habadasha

  Ahsante kwa elimu

  1. Eunice Tossy

   Karibu Victor, asante pia kwa kusoma

 2. Mustapher

  Nice my qafeer, well said my mate

  1. Eunice Tossy

   Thank you so much qafeer. Thank you for reading

   1. Jackson

    Asante Eaunice, God bless u

    1. Eunice Tossy

     Amen. Asante pia kwa kusoma Jackson

 3. Faida na Hasara za kuishi nje ya mji – Eunice Tossy

  […] Watu wanaweza wakawa bado hawajaamia, watu wako radhi wakae ‘mjini’ na joto lote hilo ku… […]

 4. Jinsi kutegemea wengine wakupende kunavyokukosesha furaha kwenye maisha – Eunice Tossy

  […] wengi hawajui namna furaha inavyoathiri sehemu zote za maisha yao. Wengine husema watafurahi wakipata kazi, wengine husema watafurahi wakipata watoto, wengine husema watafurahi wakimaliza masomo, wengine […]

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป