Pata majibu ya maswali yako yote kuhusu maisha ya chuoni na changamoto zake

woman in black jacket and black pants sitting on white staircase
Afya
Eunice Tossy  

Hatua 5 za maombolezo unazozipitia unapokuwa na majonzi

Unapopitia jambo linalokupa majonzi kama vile kuachwa, kufiwa na mtu wako wa karibu, kupata ajali, kufeli, kufukuzwa kazi, biashara kupata hasara nk, wanasaikolojia wanasema kuna hatua 5 unazipitia za maombolezo ambazo nitazielezea hapa chini.

Ningeenda kusema kwanza kama unapitia jambo gumu sasa hivi, au umempoteza mtu kwenye maisha yako, pole sana, huwa sio kitu rahisi kupitia jambo kama hilo, dunia yako yote hubadilika, hivyo nakuombea uponyaji wa moyo, utulivu wa nafsi na mwangaza kwenye kipindi hiki.

Pia soma : Mambo ya kufanya unapopitia kipindi kigumu

Hizi hapa ni hatua tano za maombolezo / 5 stages of grief ;

Kukataa / denial
Unachukua muda kukubali kuwa lile jambo ni kweli limetokea, kuwa lile jambo limekutokea, au huyo mtu kafa, hauamini, haukubali kuwa umeachwa nk. Kwenye hii hatua unachanganyikiwa kidogo na akili inakuwa haijatulia kutaakari hilo unalolipitia/ liona/ au ulilolosikia. Unakuwa na uoga na mshtuko muda mwingine.

Hasira / anger
Unakuwa na hasira moyoni ya kilichotokea, aliyesababisha kitokee au ambaye haelewi unalopitia. Unaweza kuwa na hasira na aliyekuacha au hata aliyekufa ya kuwa kwanini amekuacha au amekufa

Kujadiliana ili kufikia muafaka / bargaining
Kwenye hii hatua unajitahidi hata kujadiliana kichwani kwako na yule aliyekuacha au kufa, unahisi kama hali ingekuwa abc basi kifo kisingetokea, angefanya moja mbili tatu basi msingeachana bado mngekuwa pazuri nk. Katika hatua hii unajaribu kuelewa au kupata maana ya kitu kilivyotokea, kujaribu kuelewa kusudi nk. Unaweza ukatafuta msaadakwa watu na katika hatua hii unakuwa na uwezo wa kuelezea kilichotokea kwa watu.

Pia soma : Mambo ya kufanya unaposalitiwa na mpenzi wako

Sonona / depression
Kutokana na mawazo mengi na hali hii kuathiri hisia zako kwa muda unapata sonona. Sonona inayotokana na kupitia jambo gumu ni ya kawaida kabisa kuipitia ni hali ya binadamu kurespond kwa yale yanayomkuta. Katika hatua hii unajisikia hauna msaada, unajisikia vitu ni vingi sana na vizito sana unavyovipitia.

Kukubali / acceptance
Hatua ya mwisho ni kukubali kilichotokea na kuendelea na maisha. Haimaanishi utakuwa hauumii ila utakuwa tu umekubali lililotokea. Kwenye hatua hii unaweza kuangalia kama una jambo lingine la kufanya mfano kama umeachwa basi unajitia moyo kuwa utapata mwingine na unakuwa na matumaini ya kuendelea mbele baada ya kukutana na hali hiyo uliyokutana nayo.


Wanasaikolojia wanasema sio lazima upitie kama nilivyozieleza ila unazipitia kivyovyote vile kwa kuanza na lolote, lengo kuu likiwa ni kufikia kukubaliana na hali au ukweli wa hilo linalokukumba.

Pia soma : Mambo yanayokusaidia kuwa chanya kipindi unapopitia mambo magumu

Hatua hizi zote ni sahihi na za muhimu kuzipitia kikamilifu ili upate uponyaji wa moyo na kuachilia, kwahiyo usihisi haupo sawa kisaikolojia unapopitia hizi hatua wanasaikolojia husema ndio njia sahihi ya kuomboleza / kuhuzunika

* Mimi sio mtaalamu wa afya kwa hiyo nimeelezea kwa uelewa wangu

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Muongozo wa Maisha ya Chuo

Je unaenda chuo? Au upo chuo?

Pata majibu ya maswali yako yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuoni hapa, pata dondoo na ushauri kwenye mahusiano, maswala ya pesa na biashara, afya yako chuoni, mitindo, skendo za chuo, kudili na walimu wasumbufu na ada mbalimbali zinazowahusu wanachuo kwenye kitabu hiki

Bonyeza Hapa Kupata Kitabu Hiki
Translate »