Download Mwanachuo planner ili uandike malengo yako ya chuo sasa

Your Guide To University Life / Maisha ya Chuo

Jambo la kuzingatia unapochagua sehemu ya kufanyia field

Reading Time: < 1 minute

Kuna wale wanaofanya field kwasababu ni sehemu ya somo na inakupa maksi, na kuna wale wanaotilia mkazo na kuona umuhimu wake.

Kuna watu waliotengeneza connections za kazi field na wengine walijifunza mambo mazuri tu mpaka wakazawadiwa vyeti sehemu walizofanya field.

Anyways, kama unafikiria kufanya field, hili hapa ni jambo la kulizingatia;

Unatamani kujifunza nini ambacho kitakusaidia hapo mbeleni?

Siamini kama kwenye kozi umefurahia masomo yote kwenye semester, lazima kuna eneo ambalo unalipenda zaidi, kwasababu yoyote ile. Je, ungependa kufanyia field hilo ili ukuze ujuzi zaidi? Na ni sehemu gani unaweza pata ujuzi huo?

Kumbuka pia kuna CV baada ya chuo hivyo mambo unayojifunza field ndiyo utakayoandika kama ujuzi wako wa kuanzia hivyo hakikisha unaenda sehemu ambako utapata ujuzi ule unaotamani ujulikane unao mtaani.

Eunice

One Comment

Share Your Thoughts With Me