(Maisha ya Chuo ni platform ambayo unaweza kupata ushauri, dondoo na msaada utakaokusaidia kurahisisha maisha ya chuoni na kukabiliana na changamoto mbalimbali za chuoni. Unatolewa na waliohitimu vyuo kwenda kwa wanavyuo wa sasa, bonyeza hapa kupata makala mbalimbali zinazohusu maisha ya chuo)


Kama tunakuwa wakweli, kusoma kabla ya test kunakuwaga tofauti na pale test ikitangazwa, lakini pia mwanzo wa semester pia kujisomea kunakuwaga tofauti na semester ikichanganya, ila nashea tips kwa wewe unayependa kujiwekea ratiba natabia ya kujisomea binafsi kwasababu ukweli ni kuwa sasa hivi wote tunajua kuwa chuo sio bata, kwa hivyo msuli wakati wote ni lazima.

Kuandaa ratiba yako ya kujisomea inabidi-

  • Uangalie ratiba ya masomo na mambo yako mengine

Cha kwanza na cha msingi ni kuhudhuria lectures, na hivyo ratiba yako binafsi ni lazima iangalie ratiba ya chuo inaendaje na una uhuru kiasi gani hapo. Ila pia kama una biashara unafanya ambayo sio ya room unatoka kwenda sehemu fulani inabidi pia hilo ulipigie hesabu, cha msingi kukumbuka ni kuwa wewe ni mwanachuo mwenye biashara, sio mfanyabiashara anayesoma chuo, hivyo kujisomea ni muhimu na kunakuja kwanza. Angalia pia ratiba ya mambo ya kijamii unayoyafanya kama michezo, mitoko nk.

  • Jua muda gani unaelewa vizuri

Kila mtu ana muda ambao akisoma anaelewa haraka kuliko muda mwingine labda kama ukiwa kwenye mitihani ndio akili inabeba kila kitu, ila mida mingine kuna muda akili yako inaelewa haraka kuliko muda mwingine. Mimi nikisoma usiku naelewa haraka kuliko asubuhi, labda kipindi cha test, na yenyewe narudia rudia sana ili nikielewe. Jitambue muda wako mzuri wa kusoma, halafu angalia na ratiba ya lectures, upange kwa kuangalia hayo mawili. Lakini pia ukijua wewe huwa unachukua muda gani kuelewa/ kukariri jambo inasaidia sana kujua uanze kusoma mapema kabla test hazijatangazwa au utazima moto.

  • Jua notes zilizopo na muda gani unaweza kutumia kuzielewa

Kuna semester somo moja linaweza hitaji nguvu zaidi ya mengine labda kwa vile notes nyingi au ni gumu au lina credit kubwa, hili nalo ni jambo la msingi kuliangalia unapoandaa ratiba. Simaanishi ukaze kwenye somo moja peke yake, weka uwiano, lakini pia jua wapi kwa kuweka mkazo kwa nguvu kidogo kwa kuangalia vitu kama hivyo.

  • Fuatilia ratiba yako na uiheshimu

Ukiachana na kuwa usiweke ratiba ngumu sana (inayokubana sana) na pia ujue kupumzika kwa ajili ya mwili na afya yako ya akili, ni vizuri kuwa mfuatiliaji wa ratiba utakayoiweka na kuondoa vitu vinavyokutolea focus ukikaa chini kusoma mfano simu, weka mbali (kabatini ukiamua), nenda kasome maktaba nk

crop black student writing report
  • Weka lengo unalotamani kulitimiza kwa kujisomea

Inawezekana ni mimi tu ila nilipokuwa chuo nilikuwa nakosa motisha ya kusoma kama hakuna test labda kama nikiwa na lengo la GPA fulani ndio najisukuma ili nitimize malengo yangu, kuweka malengo kunaweza kukupa motisha ya kusoma lakini pia kukufanya kuona muda ulionao ambao huwa unaupoteza kwa mambo mengine.

  • Jua pia ratiba ya test, assignments na mitihani

Ukijua ratiba utajua unahitaji muda kiasi gani kujiandaa kwa hayo yajayo lakini pia inaweza kukupa motisha ya kuanza kuweka msuli mapema na kuifuata ratiba yako.


Hayo ndio mambo machache yanayoweza kukusaidia kupanga ratiba yako ya kujisomea binafsi chuoni, usiache kusubscribe kwenye channel ya Maisha ya Chuo YouTube ili kupata dondoo za maisha ya chuo kila Jumanne na Alhamisi na pia kufollow Maisha ya Chuo Instagram ili kupata dondoo zinazokurahishisa maisha ya chuo kila siku.

Eunice

You May Also Like

1 Comment

  1. Mambo ya kufanya kama umepoteza mood ya kusoma – Eunice Tossy

    […] Pia Soma : Jinsi ya kuandaa ratiba binafsi ya kujisomea chuoni […]

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป