rose gold apple watch with pink sport band near eyeglasses

Ukiwa chuo hasa mwisho wa semester unaweza kushtushwa na vile muda ulivyokwenda, kuna vipindi vitatu, kuna kipindi mwanzo wa semester mnapofanya usajili mambo yanakuwa bado hayajachanganya. Huu ndio muda wahadhiri wanapelek vipindi mbele na wewe unalala sana. Kuna kipindi hapo katikati test, assignment na lectures zinachanganya na unakuwa busy kidogo yani mambo yanaanza kasi ya ajabu na kipindi cha mwisho ni pale unakaribia na unaingia UE/SE, yani hapa ndio kipindi unachoshangaa na kuwaza muda ulipotelea wapi.

Mara nyingi hii inatokea kwasababu ulikuwa unaenda tu kama mambo yalivyo haukupata balance maana chuo kina mambo mengi yanaweza kukufanya hata ukashindwa kupata muda wa kujijali mwenyewe. Haina shida, kama ungependa kujua jinsi ya kubalance mambo ya chuo na mambo yao mengine kama biashara nk, hizi ndio dondoo zitakazokusaidia kufanya hivyo;

Soma : Mambo 5 ya kuzingatia unapotaka kuanzisha biashara chuoni

Kila swala lifanye katika muda uliopanga, kama ni masomo, soma kwa wakati uliopanga. Kama ni bata, kula vizuri tu kwenye wakati ulioupanga. Pumzika vizuri ili pia upate nguvu ya kufanya hivyo vitu unavyopanga kwa wakati.

  • Punguza kutumia muda kwenye vitu vinavyokuondolea focus unapofanya mambo unayoyafanya.

Unaweza shangaa ni muda kiasi gani unaupoteza kuangalia umbea wa Instagram muda unaoanza kusoma au kusikiliza stori badala ya kwenda discussion au kwenye mishe hiyo nyingine.

Pia Soma : Mambo ya kufanya yatakayokusaidia kutokupoteza focus unaposoma

  • Omba msaada

Kama una biashara room, ukienda lecture waombe wanaobakia wakuuzie. Kama upo group la discussion na upo kwenye birthday party nyumbani au mbali, omba watu ulionao group moja wakusaidie kujua ni jinsi gani unavyoweza kushiriki hata ukiwa mbali au wakuandike jina kwenye assignment yenu hiyo ili usikose maksi. Usiogope kuomba msaada kama una mambo mengine na uko na watu waelewa.

Pia Soma : Kwanini viongozi wengi wa vikundi vya dini chuoni hufeli?

  • Jitahidi kusoma kwa discussions, kusolve past papers na kuhudhuria lectures ili ukikaa kusoma usiwe unatumia muda mwingi sana ili kuelewa.

Tafuta namna ya kubalance lakini jua katika lolote lile masomo yanakuja kwanza. Ukiwa kiongozi, wewe ni mwanachuo mwenye cheo na dhamana yaa uongozi, ukiwa unafanya biashara jua pia wewe ni mwanachuo mwenye biashara, mambo yote yanakuja baada ya masomo kwahiyo jua pia wapi kwa kuweka uzito zaidi.

Eunice

You May Also Like

Share Your Thoughts With Me

Translate ¬Ľ