Pata majibu ya maswali yako yote kuhusu maisha ya chuoni na changamoto zake

birthday wallpaper
Maisha ya Chuo
Eunice Tossy  

Jinsi ya kuenjoy birthday yako unapokuwa chuoni

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Miaka inaenda unapokuwa chuo na hivyo umri wako pia unabadilika. Japokuwa uko mbali na nyumbani (kama uko mbali na nyumbani) una haki ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yako ya kuzaliwa hata kama upo chuo au umebanwa na masomo nk. Inaweza kuwa uko mazingira mapya au una marafiki mapya ila hii haimaanishi usisherehekee na kuenjoy siku yako hii muhimu. Kama unapenda kusherehekea birthday yako unapokuwa chuoni na unatafuta ideas za mambo ya kufanya kusherehekea birthday yako hizi hapa ni ideas za namna mbalimbali unazoweza kusherehekea birthday yako unapokuwa chuo;

  • Unaweza kufanya party ndogo room

Unaweza nunua keki, ukakata na wana room na majirani na mkacheza mziki. Hapo baada ya kuwa umemwagiwa maji asubuhi yake lakini.

  • Unaweza kwenda out na marafiki zako kula mahali (chakula cha mchana au cha usiku)

Sehemu ya kujilipua inapendeza zaidi siku kama hii, ila unaweza pia kufanya hivi kwa bajeti usijilipue ukafa bure. Unaweza tuma tu hiyo siku kusherehekea pamoja na marafiki wanaokusherehekea kwenye siku yako hiyo.

Pia Soma : Budgeting tips kwa wanachuo wasio na boom/ 16 tips

  • Unaweza kuandaa party na marafiki zako wachache off campus
  • Unaweza kukata keki na kula na classmates zako
  • Tembela kivutio au sehemu ya starehe iliyopo mkoa unaosoma
  • Wengine hupendelea kusherehekea birthdays zao kwenye vituo vya watoto yatima au vya watu wenye ulemavu (na kupeleka misaada kwa watu hawa kwenye kumbukumbu ya siku yao ya kuzaliwa)
  • Sherehekea na ndugu zako waliopo karibu na wewe kwenye mkoa/sehemu uliyopo chuo
  • Tumia siku hiyo kufurahia na kupumzika usijihusishe na mambo ya kusoma nk. Hili linawezekana kiurahisi kama birthday yako imeangukia siku ambayo haina mitihani na ni wikiendi.
  • Chukua muda huo kufikiria kuhusu mwaka mpya na yale unayojifunza kuhusu maisha, jiandikie barua na malengo ya maisha yako, nenda dance, katengeneze kucha, kapate massage, nenda hiking, nenda movies nk
  • Kwa wale walio kwenye mahusiano unaweza ukaplan kitu na mpenzi wako for our birthday, picnic na vitu kama hizo zinaweza kuwa simple and enjoyable

(Kama utapenda kumpa rafiki yako kadi ya birthday, pata kadi zenye design nzuri na maneno matamu HAPA)

Kuna idea gani nyingine unayo ya jinsi unavyoweza sherehekea birthday chuoni?

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Muongozo wa Maisha ya Chuo

Je unaenda chuo? Au upo chuo?

Pata majibu ya maswali yako yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuoni hapa, pata dondoo na ushauri kwenye mahusiano, maswala ya pesa na biashara, afya yako chuoni, mitindo, skendo za chuo, kudili na walimu wasumbufu na ada mbalimbali zinazowahusu wanachuo kwenye kitabu hiki

Bonyeza Hapa Kupata Kitabu Hiki
Translate »