Pata majibu ya maswali yako yote kuhusu maisha ya chuoni na changamoto zake

african american male freelancer on laptop in bright room
Career Guide
Eunice Tossy  

Jinsi ya kuepuka kutapeliwa unapotafuta kazi

Utapeli upo wa aina nyingi sana duniani, kuna biashara ambazo unaweza kujiunga na ukatapeliwa, kuna mambo ya mtandaoni vikundi maarufu kama ‘yahoo boys’ , kuna wale wanaosema nitumie hela mimi fulani kumbe sio na siku hizi kwa wanaotafuta ajira kuna watu mbalimbali ambao wamevamia hilo soko ili kuwatapeli watafuta ajira, kutumia shida yao na uhitaji wao kujipatia kipato. Nakumbuka mara kadhaa ambapo niliwahi kukutana nao na matapeli hawa huja kwa njia mbalimbali;

Pia Soma : Makosa ambayo wahitimu wapya hufanya wapatapo kazi

  • Kuna wale wanaokupigia simu kutoka LinkedIN

Kama kuna mtandao ambao nahisi huwa wanashinda ni LinkedIN, maana nimewahi kupokea simu kadhaa za mtu kutoka kampuni fulani kubwa, ambaye amesoma CV yangu lakini pia amesikia kuna kazi zinatolewa kampuni hiyo aliyopo ila bado hazijatangazwa, hivyo kwa kuwa yeye ni mtu mwema anataka basi aniunganishe mimi ili niombe mapema na kwa vile yeye ndio atakuwa ananiunganishia nipate kiurahisi. Wote tunajua kuwa huko mbeleni kwene mazungumzo yetu kwenye hiyo simu aliyonipigia, lazima aniombe pesa, kama sio leo basi baada ya muda akihakikisha kuwa ameshaniaminisha na mimi hiyo kazi naitaka hivyo niko radhi kutoa gharama zozote kama ni kazi ya uhakika kama anavyosema.

Mara ya kwanza kupokea simu hii nilijua uongo baada ya kuona kuwa alikuwa anatumia muda mwingi sana kunishawishi na alikuwa online muda wote, nilipokataa alitaka niite wengine, kwa mtu mwenye cheo alichotaja yeye, hawezi kuwa online muda wote vile labda kama hii ndio kazi yake lakini pia kwa kuunganishiana kazi anakosema yeye mbona anataka sana watu baki wakati wengi huunganishiana kindugu au kuna hela anaitaka kutoka kwa watu hawa? Lakini pia nilimposti kwenye group la watafuta kazi wengine ndio wakanionya kuwa huyo ni tapeli wa LinkedIN.

Pia Soma : Namna biashara ya Network Marketing ilivyonipeleka polisi

  • Kampuni ambayo inataka unanze kazi Jumatatu ila utume hela ya sare za kazi ambayo watakushonea ukienda Jumatatu kazini utapewa sare yako

Kwenye kampuni hii unapata kazi mapema sana, yani unatuma CV na siku hiyohiyo unapata kazi, interview yao inakuwa kwa simu na baada ya hapo wanakuambia ofisi zao zipo karibu na Mlimani city, Jumatatu uende kuanza kazi ila wana sare hivyo inabidi utume hela wakushonee sare ambazo utapewa Jumatatu hiyohiyo unayoenda kuanza kazi. Kwenye hili nilishangaa kuona mkazo wa hela ulikuwa mkubwa kuliko wa vipimo maana kama ukiwatumia hela, vipimo vyako vya nguo wanavijuaje?

  • Yule anayetangaza kazi anakuambia mfuate inbox, na kwenye tangazo lake anahakikisha kusema kuwa yeye sio tapeli ile kazi aliyoitangaza ni ya kweli. Mtu akitangaza kitu halafu akahakikisha kusema kuwa sio utapeli mara nyingi huwa ni utapeli maana bidhaa za kweli hazina haja ya kusema kuwa sio bidhaa feki. Mara nyingi nilipowafuata na kuwaunganishia watu walinipa mrejesho kuwa hawawaelewi elewi.

Pia Soma : 12 digital skills itakazokusaidia kujiajiri

Najua mifano yangu niliyoitoa ni michache na ningependa kusikia kwenye comment njia nyingine ambazo ushawahi kukutana na matapeli katika harakati zako za kutafuta kazi. Tukishea njia mbalimbali zitasaidia wasomaji wengine wa sasa au hata miaka ijayo ili waepuke kutapeliwa kwa njia ambazo sisi tumeponea chupuchupu au hata tulitapeliwa. Kwa mimi hizi hapa ni njia zilizonisaidia kuepuka kutapeliwa;

  • Kufuata sauti yangu ya ndani iliyoniambia kuwa kuna jambo halipo sawa

Kuna muda mwingine mambo huwa yanang’aa sana na yanaonekana kama ni mepesi sana kwa hayo mambo kuwa kweli, basi ukijisikia hivyo mara nyingi huwa ni kweli kuwa umepitia mteremko sana kuna jambo haliko sawa. Sikiliza sauti ya ndani, swali kama ‘ mbona hawaniulizi vipimo?’ linaweza kuwa dogo unapoambiwa tuma pesa haraka haraka ila ni la muhimu sana kujiuliza. Tulia na pitia kila jambo kwa jicho la utulivu. Utapeli mara nyingi hufanikiwa kwasababu watafutaji huwa tunapaniki na kutaka kufanikiwa haraka kwenye hili kiasi kuwa huwa tunaamini lolote ili mradi tu tuape kazi, na mtu anapokupa presha ya jambo unakuwa hauna muda wa kufikiria kwa utulivu, kwahiyo tulia na fikiria vizuri, sikiliza sauti yako ya ndani.

  • Ulizia na fanya utafiti

Hakuna jambo la muhimu kama kufuatilia kampuni au sehemu watu husema wanatoka, ni mara kadhaa nimeenda kwenye usahili na wasahili wakanisifia kwa kufanya utafiti wa kampuni yao kabla ya kwenda kwenye usahili. Kama yule mfano wangu wa kwanza yani nilikuwa tayari kuwapa namba za watu wanaoniamini kabisa ila nilipouliza ndio nikajua kuwa ni utapeli. Uliza, watu wameona mengi sana. Najua unahisi ukiuliza itachukuliwa lakini mimi huamini kama yako ni yako tu. Mara zote nilizouliza ilinisaidia kuepuka kuibiwa. Fanya utafiti mitandaoni, Google, uliza wawili watatu, mfuatilie huyo aliyekutafuta hata jina alilosajiri namba yake nk

  • Usiendeshwe na presha au hisia

Kama nilivyosema kukupa presha ndio kunawasaidia wao kukufanya ufane wanalolitaka, ukiona mambo yanapelekwa haraka sana, tuliza akili kwa muda. Usiendeshwe na hisia, muda mwingine inafika kipindi unachoka kutafuta ajira na hiyo inaeleweka na inaweza kukufanya ukipata chochote uwe tayari kufanya chochote ili uipate tu hiyo kazi iliyojitokeza, lakini ni muhimu pia kuchunguza jambo kwa undani, usiende tu kwa hisia. Ni muhimu pia kutoamini kila simu unayopokea au kila email kuwa ni kweli hao watu ni kampuni halali.

Pia Soma : Mambo ya msingi kwa waajiriwa wapya kuyajua

Cha mwisho ambacho ningependa niseme ni usitoe rushwa ya ngono au ya pesa ili kupata kazi, kuwa na subira, yako itakuja. Najua unapoona kuwa hio ndio tabia na watu wengine wanafanya ili kupata unaweza kuhisi hauna jinsi ila tabia inaendelea kwasababu wanaoiendeleza wanaendelea kushiriki, ukikataa wewe kushiriki unaweza kuwa umeharibu mzunguko wa tabia hiyo na kuendelea kwake. Kila mtu ana wajibu binafsi na uchaguzi wa kuamua kushiriki au kutoshiriki kwenye tabia fulani.

Usiache kuniambia aina mbalimbali za utapeli ulizowahi kukutana nazo kwenye kutafuta ajira kwenye comments!

Share Your Thoughts With Me

Muongozo wa Maisha ya Chuo

Je unaenda chuo? Au upo chuo?

Pata majibu ya maswali yako yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuoni hapa, pata dondoo na ushauri kwenye mahusiano, maswala ya pesa na biashara, afya yako chuoni, mitindo, skendo za chuo, kudili na walimu wasumbufu na ada mbalimbali zinazowahusu wanachuo kwenye kitabu hiki

Bonyeza Hapa Kupata Kitabu Hiki
Translate »