Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha,  Maisha ya kila siku

Jinsi ya kuinyamazisha sauti hasi iliyo ndani yako

Toka nigundue kuwa kwa siku tunajiongelesha wenyewe ndani kwa ndani mara nyingi kuliko tunavyoongea na wengine nimekuwa nikifuatilia maneno ninayoyasena, hivi unajua kuwa huwa tunajiambia maneno makali ambayo katika hali hiyohiyo hatuwezi kuwaambia marafiki zetu.. Yani ukikutana na rafiki yako halafu akakosa jambo fulani hauwezi kumwambia maneno makali kama unayojiambia wewe mwenyewe ukiwa katika hali ile ile. Sauti zetu za ndani ni kali mno na mara nyingi ni hasi.

Haya hapa ni maneno machache ambayo sauti yangu ya ndani huniambia kwa siku ambazo sijisikii vizuri au hata siku ninazojisikia vizuri :

Wewe sio mzuri’

‘Hakuna anayekupenda’

‘Kila unalogusa kulifanya linaharibika’

‘Wewe ni mbinafsi’

‘Haupendi watu’

‘Umefeli kwenye maisha’

‘Haujui unachokifanya na hautofanikiwa’

‘Yanickila siku wewe ndio unakosea, watu wanakuona mjinga’

‘Hautokuja kubadilika, hizi tabia zako mbaya ni zako milele’

Hayo na mengine mengi ni maneno ambayo sauti yangu ya ndani hunikumbusha, huyacheza na kuyarudia kwenye nafsi yangu kama nyimbo niliyoipenda baada ya kuisikia, tofauti ni kuwa maneno haya siyapendi na huniumiza. Baada ya kusoma na kufuatilia hii mada nimegundua kuwa hizi sauti za ndani mara nyingi ni sauti za watu wengine, ni mambo ambayo wengine hutuambia kuhusu sisi halafu sisi kuyachukua na kuyafanya yetu, watu hushauri uwe mpole unapokuza mtoto kwasababu sauti yake ya ndani akija kuwa mtu mzima huja kuwa maneno yale uliyokuwa ukimwambia utotoni, kwahiyo labda njia ya kwanza ya kunyamazisha sauti zetu za ndani ni kufuatilia zinatoka wapi, nini chanzo cha hayo maneno makali na hasi tunayojiambia.

Unaweza kufanya hili kwa kujiuliza maswali kila ukisikia sauti yako ya ndani inajiambia maneno hayo hasi, kila unaposikia labda ‘wewe sio mzuri’ au ‘wewe ni mtu mbaya’ jiulize kwanini unajisemea hivyo, je inatokana na neno ulilowahi ambiwa au kwanini unajiambia hivyo na kujisikia hivyo nk nk

2. Andika maneno chanya yabandike mahali

Ni muhimu kujikumbusha au kujiambia maneno chanya kwa kukataa yale hasi kila yanapokuja, unaweza kufanya hivi kwa kubadilisha hayo maneno hapohapo unaposikia neno hasi au kubandika maneno chanya mahali ili uyaone kila unapoendelea na mambo yako katika siku.

3. Amini maneno chanya watu wanayokuambia

Kwa watu ambao tunajiongelea maneno hasi sana ni vigumu sana kuamini au kupokea maneno chanya au sifa pale unaposifiwa na watu. Jifundishe kukubali na kupokea na kuyaweka moyoni maneno chanya unayoambiwa, jifundishe kukubali kuwa wewe sio tu mambo hasi, wewe ni mambo chanya pia unayoambiwa au unayojiambia. Naamini ukiwa na mambo chanya mengi unayoamini kuhusu wewe kuliko hasi hata kujiamini kunaongezeka.

Na hizo ndio njia tatu zinazonisaidia mimi kunyamazisha sauti hasi iliyomo ndani yangu, je njia zipi zinakusaidia wewe? Niambie kwenye comment

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate »