Kama mwanachuo kuna mambo mengi ambayo yanaweza yakakfanya upate magonjwa ya akili, kuna stress za masomo, mambo a kiuchumi, familia, mapenzi, marafiki wa uongo, kuigiza maisha, mawazo ya maisha nk, yote haya yanaweza kukupa msongo wa mawazo unaoweza kusumbua afya yako ya akili.

Wataalamu wanasema kuwa kuna magonjwa matano ya afya ya akili ambayo wanachuo wengi yanawasumbua nayo ni;

 • Sonona (Depression)
 • Magonjwa ya kula (Eating Disorders)
 • Waiwasi (Anxiety)
 • Addiction
 • Suicide

Vitu vya kufanya ili kujali afya yako ya akili unapokuwa chuo ni:

 • Kupumzika (pumzika akili, Chukua mapumziko ya mitandao ya kijamii nk )
 • Kula vizuri na kunywa maji
 • Lala vizuri
 • Fanya mazoezi
 • Kutana na marafiki – uwe na maisha tofauti na masomo
 • Usifanye kila kitu wewe – usibebe mzigo wa darasa au kikundi chako cha assignment peke yaki kila siku.
 • Tembelea ofisi ya mshauri wa chuo kama unahitaji msaada zaidi (counselor)
 • Jaribu kuwa na muda wa kufanya vitu vinavyokuletea furaha
 • Usitumie sana vilevi na madawa 
 • Jifanyie vitu vyema / Jipongeze (ukifaulu jitoe out kula chakula, au jinunulie kitu

Bonyeza hapa kufollow @maishayachuo Instagram kupata dondoo na msaada wa karibu kuhusu maisha ya chuo

Eunice

You May Also Like

Share Your Thoughts With Me

Translate »