Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maoni

Jinsi ya kujua kama biashara unayotaka kujiunga ni ya utapeli / network marketing

Nimejitahidi sana kuweka makala zinazohusu utapeli kwenye blogu hii, makala ambazo na uhakika zinaweza kukusaidia kuepuka kuingia mtegoni mwa hili mfano :


Biashara za network marketing zipo nyingi sana, makampuni haya yapo mengi sio tu Tanzania, duniani kote. Wanashawishi watu watafutaji, wenye nia ya kufanikiwa kwenye maisha kujiunga na hivyo wao kuwatapeli kwa kutumia nia njema za hawa watu na tamaa yao ya kufanikiwa. Wote tunatafuta, watu wa network marketing wanalijua hilo na wameamua kulitumia hilo dhidi yako, hawajali kama ni maskini au unashida ngapi kwenye maisha yako, watakutapeli tu pesa na kukupotezea muda.

Kama kweli ungekuwa unatajirika kupitia hizi biashara, kwa asili ya watu jinsi tulivyo unafikiri ungeitwa na kuelekezwa jinsi ya kutajirika? Kama sio wewe ndio unayehitajika ili kumtajirisha mtu?

Network marketing huahidi kipato, kujitegemea, utajiri, mafanikio na mahusiano (familia), ni rahisi kwa wengi kuingia kwasababu ni kama ajira, kuna ahadi ya kipato kwa hiyo kuna kuwa kama kujiajiri fulani hivi.

Ni baadae sana baada ya kununua bidhaa na kuona huwezi kuziuza, marafiki zako wanakukimbia au hawapokei simu zako kwa vile stori yako ni bidhaa zako na kuwaita wajiunge kwenye kampuni na baada ya kupoteza muda na pesa na kuona namna walivyokuambia utafanikiwa haikutokea ndipo wengi huelewa kama wameibiwa, ila hapa naenda kushea dalili chache za kujua kama hiyo biashara inaweza kuwa utapeli / network marketing mapema, nazo ni;

 • Mtu anayekukaribisha hawezi kuiongelea kwa simu mpaka uende kwenye kikao chao
 • inaleta mashaka kuiamini kama ni kweli unaweza fanikiwa kwa kuamini au kufanya hayo tu uliyoambiwa (too good to be true)
 • kuna hamasa nyingi sana kuliko hatua za kweli za kufanya (yani unapewa maneno ya hamasa ya kukufanya uamini utakuwa bilionea hata kabla hauja uza bidhaa)
 • ‘good morning’ nyingi
 • Kuna kiingilio kidogo cha kujiunga kwenye hiyo biashara yao na ununuzi wa bidhaa unafuata au unatakiwa kuhimiza watu unaowajua wajiunge (pyramid scheme)
 • Unalipia packages za kujiunga, iwe educational packages au packages tu wakati wa kujiunga au ili upande level zao
 • Hauelewi kitu unachofanya au kazi haswa itakayokupa hela kwenye hilo jukwaa, ila unaahidiwa kupata hela baada ya kujiunga muda mwingine kwa kufanya kitu ambacho kikawaida unajua hauwezi pata hela mfano kujifunza au kuangalia video
 • Wanavyoongea inaonekana kama hela yao inapatikana kirahisi sana na kwa haraka sana au matangazo yao yanaonesha hilo
 • Unanunua bidhaa kiasi fulani na kuna vyeo vya kupanda kwenye kamuni na vyeo vinavyozidi kupanda ndio mafanikio au kiasi unacholipwa inavyozidi kupanda
 • Unapanda cheo ila pesa zako zinakuwa zipo kwenye akaunti yako iliyopo mtandaoni kwenye tovuti ya kampuni, kiasi fulani ambacho hauwezi kukitoa mpaka zifike kiasi fulani au umuuzie mtu coins.
 • Inabidi uandike majina ya watu 100 unaowafahamu, waambie kuhusu hii biashara, wao wawaambie wengine (washawishi ndugu na marafiki watapeliwe kirahisi)
 • Mtu anakufuata inbox kwenye mitandao ya kijamii ujiunge kwenye biashara yenye faida, kuhusu mambo ya afya, masoko nk ila hauambiwi bidhaa utakayoiuza ni ipi ila tu kuna fursa
 • Bidhaa zao ni za gharama sana, dawa ya mswaki 15000
 • Unatakiwa ulete watu ili uone faida ya biashara hiyo, kwahiyo unaishia kuamini kuwa watu kutokuja ndio kumekukosesha utajiri.
 • Vikao mahotelini na mashughuli makubwa makubwa
 • Kuna kuwa na uharaka yani kama vile ukikosa kujiunga kwenye hiyo fursa kwa wakati huo utakuwa maskini na utajutia maisha yako yote kwanini haukujiunga
 • Kuna picha za wenye magari nyumba na wanaosafiri kwa jina la hiyo biashara, hii inakupatumaini kuwa siku moja wewe ndio utakayefanya hayo
 • Wanaongelea mindset kupita kiasi, ‘mindset yako, mtazamo wako ndio unakufanya uwe maskini’
 • Inaendeshwa kwa hype sana bila kuwa na uhalisia
 • Mtu anayekushawishi kuwa utatajirika ukimwangalia unaona kuwa na yeye ana ndoto tu ya kutajirika, utajiri haujawa uhalisia kwake

Kwavile inabidi ununue bidhaa kwenye hiyo kampuni ili kuziuza au kuzitumia, jua tu sehemu yoyote unaponunua bidhaa wewe ni mteja wao, kwahiyo hata kwenye hayo makampuni wewe ni mteja unayeleta faida kwa kununua bidhaa zao hata kama usipoleta watu.

Watu wengi wanaoacha kufanya network marketing huwa wanaonekana wamefeli, wao ndio wameshindwa kupambana maana mafanikio yapo ila wao hawakutumia nguvu kuyatafuta, ukweli ni kuwa biashara hizi zimetengenezwa kukufanya ufeli, wa juu wafanikiwe, sio makosa yako lakini pia kwa vile mafanikio yako yanategemea kuttapeli wengine, wengine huchagua kuacha baada ya kujua mchezo ulivyo.

Ukiona dalili hizi na bado ukakaribishwa, Mtu akikuambia jiunge uwe tajiri mwambie tajirika kwanza wewe halafu nitakuja. Na zaidi ya waanzilishi na wale waliopo juu juu wa kwanza kujiunga, sijawahi msikia mtu aliyetajirika kupitia network marketing/ pyramid schemes/ MLM, wao huwatajirisha waanzilishi.

Je ni dalili zipi za biashara ya network marketing ambazo sijazitaja hapa?

Eunice

2 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป