Pata majibu ya maswali yako yote kuhusu maisha ya chuoni na changamoto zake

Maisha ya Chuo
Eunice Tossy  

Jinsi ya ku-move on unapoachana na mpenzi wako chuoni

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Kuachana na mpenzi wako ni jambo gumu kulipitia uwapo sehemu yoyote, ila nahisi ukiwa chuo ugumu unaongezeka kwa vile ya ukaribu na kwa vile mnaonana mara kwa mara labda darasa moja au kwa vile chuo ni kimoja basi lazima mtaonana na hio kiaina inakuumiza au kukuchelewesha kupona.

Nakumbuka kuna mahusiano mengine niliyokuwa nayo chuo ambay nilimove on haraka kuliko mengine, hivyo leo naenda kushea namna ya kumove on kwa wale tu ambao wanachukua muda kupona kutokana na umuhimu wa uhusiano ule au kidonda kilichotokana na uhusiano huo. Kama unatamani kupona/ komove on haya ndiyo mambo ya kufanya;

  • Usiingie kwenye mahusiano kutafuta uponyaji

Wengi huwa wanahisi kumove on maana yake kuwa na mtu mwingine, mimi naona ni kumove on ni kutokuumia tena kuhusu yule mtu. Kosa ambalo wengi tunalifanya ni kukimbilia mahusiano mengine chap chap labda tukitafuta uponyaji au ili tu atuone tume ‘ move on’ na hatuumii tena kuhusu yeye. Unaweza fanya uchaguzi mbaya wa huyo mtu mpya kwasababu ya haraka na kuangalia mtu kunakotokana na kuumizwa lakini pia unaweza ongeza maumivu mengine juu ya kidonda ambacho hakijapona.

Pia Soma : Mambo ya kufanya unaposalitiwa na mpenzi wako

  • Kama hauna sonona kutokana na hali hiyo wekeza hiyo nguvu na hasira kwenye masomo

Najua watu tunapitia hali tofauti baada ya kuachana na wapenzi wetu, wengine hupata sonona, na ni sawa kama una hali hiyo, kuachana na mtu siyo jambo jepesi, unaweza angalia hapa kujua jinsi ya kujali afya yako ya akili chuoni.

Ila kama hauna sonon tumia hiyo hasira/ nguvu/ uchungu uliyonao kuuweka kwenye masomo. Unaweza kutumia kuachana kama jambo lililokushtua na kukuamsha na kukuonesha jambo gani ni la msingi na lililokuleta chuo ambalo ni kusoma.

  • Pata mtu wa kuongea naye

Unaweza ongea na washauri wa chuo, mwanafunzi mwenzio au mtu yoyote ambaye anaweza kuwa msaada kwako. Kuongea kunasaidia kutoa uchungu, kuna kusaidia kuangalia hali yako kwa jicho jingine lakini pia kutua mzigo.

  • Usiweke uzito au kufikiria watu wanakufikiriaje

Ubaya wa chuo ni kuwa watu wanapenda drama na kuongelea wengine vibaya, na kwa vile labda watu walikuwa wanajua kuhusu mahusiano mengi ni rahisi sana kuahana kwenu kukawa mada kati ya watu waliokuwa wanajua. Usifikirie watu wanakuonaje, huwa inaumiza lakini pia inakufanya uwe mtumwa wa mawazo yao kila saa unawaza wanakuonaje inachosha na inakuchelewesha kupona. Hawakuwa kwenye mahusiano yenu kwahiyo hawajui ukweli wote lakini pia kama unaona hakuna umuhimu sio lazima ujieleze sana kwao. Maisha ni yako.

  • Punguza kumuona au kufuatilia maisha yake

Ukimfuatilia ukajua kuhusu maisha yake haikusaidii sana zaidi ya kukurudisha chini hatua mbili kwenye ngazi ya uponyaji. Kama unaweza kupunguza kumuona pia itakuwa vizuri, likija swala la kujali moyo wako fanya lile unaloona linakusaidia hata kama ni kumunfollow mitandaoni, kufuta namba, kubadilisha marafiki mliokuwa mnashea nk, lolote linalokusaidia.

  • Jiruhusu kuumia kwa ajili ya kupoteza huo uhusiano

Wengi wetu tunataka kumove on, tusihisi hisia yoyote, ila ukweli ni kuwa unapona kwa kujiruhusu kusikia zile hisia na kuziachilia. Kama unajisikia kulia, chukua muda lia, kama unajisikia kuandika hisia zako chini fanya hivyo, usizikimbie hisia, zitarudi, jiruhusu kuumia kwa muda ili upate uponyaji wa kweli. Lakini pia katika kuumia unaweza kujifunza kuhusu wewe au kuhusu huo uhusiano ulioisha.

Pia Soma : Jinsi ya Kusamehe

  • Tengeneza amani na kilichotokea

Mara nyingi tukiachanaga na watu huwa tunawalaumu kwa kutupotezea muda au kujilaumu kwa kufanya uamuzi wa kijinga, tengeneza amani na kilichotokea, yote yaliyotokea hayakuwa mabaya kuna siku nzuri ambazo mlikuwa nazo kwenye mahusiano yenu, hivyo kuachana kusikufanye usahau furaha au masomo uliyojifunza kwa kuwa na huyo mtu. Tengeneza amani na yaliyopita na maamuzi uliyoyafanya halafu endelea na maisha yako.

  • Fanya mambo yaliyokuwa yanakuletea furaha kabla ya kuwa naye

Mahusiano muda mwingine hufanya tujisahau, tuhisi hatuwezi kuwa na furaha bila ya kuwa na huyu mtu kwenye maisha yetu, moja ya woga au ugumu wa kuachana ni mawazo ya jinsi gani unavyoweza kuwa na furaha wakati huyu mtu hayupo tena kwenye maisha yako. Njia mojawapo ya kulishinda hili ni kujikumbusha na kufanya mambo yaliyokuwa yanakuletea furaha wakati bado haujaingia kwenye huo uhusiano au kutafuta mambo mapya ambayo unapenda kuyafanya yanayokuletea furaha.

Nikuambie tu kuwa moyo wako utakuja kupona, utachukua muda ila hautoumia kama unavyoumia sasa. Uponyaji upo, na unaweza kumove on. Utakuja wakati hautojisikia maumivu kama unayojisikia sasa.

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Muongozo wa Maisha ya Chuo

Je unaenda chuo? Au upo chuo?

Pata majibu ya maswali yako yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuoni hapa, pata dondoo na ushauri kwenye mahusiano, maswala ya pesa na biashara, afya yako chuoni, mitindo, skendo za chuo, kudili na walimu wasumbufu na ada mbalimbali zinazowahusu wanachuo kwenye kitabu hiki

Bonyeza Hapa Kupata Kitabu Hiki
Translate »