Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

african american male freelancer on laptop in bright room
Guest Post

Jinsi ya kupangilia ratiba yako ya siku

Naomba nikufahamishe kuwa, miongoni mwa sifa zinazotofautisha watu waliofanikiwa kiuchumi na wale wasio fanikiwa kiuchumi ni uwezo wa mtu binafsi kuishi kutokana na ratiba ambayo mtu husika kaipangilia kila siku.

Katika dunia ya sasa si ajabu kukuta mtu hajui kuanzia muda huu mpaka jioni atakuwa amefanya jambo gani na kwa muda gani. Pia hajui jambo analopanga litakuwa lenye tija na manufaa kwa namna ipi. Hii ni hatari.

Pia Soma : Unautumia vipi wakati wako?

Ipo hivi miongoni mwa tabia za watu waliofanikiwa ni uwezo wa kuweka malengo katika kila siku za maisha yao. Huwezi kufanikiwa Kama huna malengo. Na malengo yamegawanyika katika makundi mawili,
aina moja ni malengo ya muda mfupi. Haya ni malengo yanayowekwa ndani ya muda mfupi kama siku, wiki mpaka mwezi, na malengo haya ukiweza kuyatimiza basi utakuwa na msingi mzuri katika malengo ya muda mrefu.

headphones near smartphone and cappuccino on cafe table

Aina ya pili ya malengo ni malengo ya  muda mrefu, haya malengo huanzia miezi sita, mwaka na kuendelea, nakupa siri watu wote waliofanikiwa duniani huwa wanakuwa na malengo ya muda mrefu sana, hivyo anza kufahamu kusudi lako alafu anza utekelezaji taratibu.

Ni ngumu Sana kuwa na malengo ya muda mrefu kama malengo ya muda mfupi huwezi kuyatimiza, kila kitu kinaanza na msingi. Tambua kuwa malengo yako ndio yanaonyesha msingi wa mafanikio yako, hivyo basi kama una malengo ya miaka mitano na kuendelea, anza leo kwa kuanza kutimiza malengo ambayo utakuwa unayatimiza kila siku. Kumbuka akili ya mwanadamu inaenda unavyotaka wewe.

Makala inayoendana na hii : Jinsi ya kufikia malengo / ndoto zako

Ili kuishi kwa ratiba fanya yafuatayo;

01: Anza kutengeneza tabia ya kuweka malengo ya kila siku katika maisha yako.
Hali hii iwe ni tabia yako katika maisha ya kila siku, matokeo mazuri hakika utayaona

Nijaribu kukuuliza leo una malengo gani ambayo unataka kuyatimiza?  
Au mpaka muda huu ulikuwa bado ujaweka malengo? Haujachelewa nafasi bado unayo

Angalia uwezo wako wa kutimiza malengo ya muda mfupi, matokeo yake yatakuwa makubwa katika malengo ya muda mrefu, ila naomba usisahau jambo moja, siri ya kutimiza malengo ni uvumilivu na subira.


Imeandikwa na Mr YAMUNGU, 0763855049

Soma makala nyingine iliyoandikwa na Mr YAMUNGU ; Njia 3 rahisi za kuongeza thamani yako

One Comment

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป