Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

calculator and notepad placed over stack of usa dollars
Maswala ya Pesa

Jinsi ya kuwa na nidhamu ya fedha kwenye biashara

Katika kanuni zote za kutengeneza fedha kanuni ya utunzaji ni miongoni mwa kanuni kubwa 3 unazohitaji kuzizingatia ili ufanikiwe kifedha. Kumbuka kanuni hii inatuambia kwamba kila mtu anaweza kufanikiwa kifedha hata wale wenye kipato kidogo kama tu tutajenga utaratibu wa kubana matumizi yasio na ulazima na kutunza fedha tunazozipata na sio kutumia zote kwa maana sio kwa kiwango gani cha fedha tunaingiza ndicho kitachoamua mafanikio yetu bali ni kwa kiwango gani tunatunza.

Pia Soma : Hii ndio sababu mitaji mingi ya biashara hufa mapema

Ni muhimu kujenga nidhamu ya kutunza fedha unazozipata kutoka katika ajira au biashara yako kwa sababu kubwa 4;

  1. Zitusaidie katika kuanzisha biashara mpya, kumbuka kuwa kanuni nyingine ya mafanikio ya kifedha inasema kamwe usitegemee chanzo kimoja cha mapato.

2. Sababu ya pili zitusaidie katika kukuza mtaji wa biashara tunazofanya sasa

3. Zitusaidie katika wakati wa majanga mfano wakati wa Corona, moto nk

4. Zitusaidie miaka ya uzeeni, maana kwa wakati huo hatutakuwa na nguvu za kufanya kazi licha ya kwamba tutakuwa tunatumia fedha tena kwa wingi.

Pia Soma : Jinsi ya kuwa na matumizi mazuri ya hela

Kuwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kutunza fedha kwaajili ya lengo fulani sio kitu rahisi na kama ingelikuwa rahisi kila mtu angeweza kutunza na kufanikiwa kifedha. Inahitaji moyo wa kujitoa na kujibana na nidhamu ili uweze kutunza bila kujali unapata fedha kidogo au unapitia changamoto gani kwa wakati huo.

Njia rahisi ya kujenga nidhamu ya fedha hasa ile ya utunzaji ni kujilipa mwenyewe kwanza yaani ukipata fedha kabla hujafikiria kuitumia anza kwanza kwakutenga 10% au 30% kutegemeana na malengo uliyojiwekea ya utunzaji ndipo baadae uingie katika matumizi mengine.

Watu wengi wanashindwa kutunza fedha kwa sababu wakipata huanza kufikiria matumizi na kudhani itakayobaki ndiyo watatunza kwa bahati mbaya fedha haijawahi kutosha na ndio maana wamekuwa wakishindwa kutunza.

Usiwe miongoni mwa watu wanaofanya kosa hili, kama utahitaji kufanikiwa kifedha na hata kwenye biashara. Kitu kikubwa unachopaswa kuelewa kuhusu utunzaji wa fedha ni kwamba kama hauna sababu ya msingi na yenye mashiko ya kutunza fedha hautafanikiwa katika utunzaji hivyo ni muhimu kuwa na lengo tena si tu lengo bali lengo thabiti la kwanini unataka kutunza maana hili ndio litakuhamasisha kutunza hata kama umepata kidogo au unapitia changamoto kubwa na katika utunzaji wa fedha usiwe na visingizio vyovyote vile.


Imeandikwa na Victor Mwambene, Mshauri wa fedha na biashara.

Share Your Thoughts With Me

Translate »