Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

adult african american people black women business
Guest Post,  Maswala ya Pesa

Kauli 6 usizopaswa kumwambia mteja kwenye biashara yako

Kama mfanyabiashara ni lazima kuwa makini sana na unayoyasema kwa wateja kwa kuwa wateja ndio waaoweza kuijenga au kuiharibu biashara yako. Akienda kukutangaza vizuri kwa wengine inakuongezea kujulikana na unapata wateja wengine pia lakini pia kutokana na kauli zako anaweza kwenda kukutangaza vibaya pia.

Kabla ya kufungua kinywa chako jitahidi sana kutafakari hicho unachotaka kukisema mbele ya wateja. Kama kina maana yoyote.

Zifuatazo ni kauli kuu 6 usizopaswa kuzisema mbele ya Mteja..

1. HATA SIELEWI

Badala yake sema hivi, ‘hebu tuone Kama naweza kukusaidia Au Tatizo/Shida yako itapatiwa ufumbuzi, subiri kidogo’. Acha kumfanya mteja apigwe na butwaa kwa kukuona hauna msaada kwake.

Mpaka mteja anaamua kukufuata wewe maana yake ni kwamba ameona wewe una utaalamu katika nyanja hiyo kwahiyo onesha uwezo wako kwa kumpatia taarifa au maelezo yanayojitosheleza.

Pia Soma : Hii ndio sababu mitaji mingi ya biashara mpya hufa


2. HAMNA SHIDA.

Usimpe uhakika, badala yake sema hivi, ‘Pole Sana unataka nikusaidiaje Au Nitazingatia ondoa Shaka’

Usikubali kirahisi, fikiria kwanza kabla ya kusema neno lolote kutoka katika kinywa chako kwasababu mteja huwa anapenda uhakika wa huduma sasa unaposema hamna shida? Je ikitokea shida utafanya nini?


3. SINA CHA KUKUSAIDIA

Badala yake sema hivi, ‘Ni kweli nilitamani kukusaidia ila itakuwa ngumu pole sana Au Unaweza ukajaribu (xxxx) pengine pale utapatiwa msaada’. Usiseme hatuna au hamna cha kusaidia wakati ni WAJIBU wenu kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma sahihi au majibu ya matatizo yao.

Wateja huwa wananunua tiba ya maumivu yao kwahiyo hawezi mtu akanunua simu kwako halafu ikamzimia akarudisha ofisini kwenu mkasema hamna cha kumsaidia lazima ajiskie vibaya na ni WAJIBU wenu kumsaidia kwa namna yeyote ile.


4. HAIWEZEKANI

Badala yake sema hivi, ‘Mimi nitashindwa au siwezi ila wapo wanaoweza kufanya au kukusaidia’ Au sema ‘Itashangaza sana jambo kama hili kushindwa kupatiwa ufumbuzi’, ili kumtia moyo.

Si sahihi kusema haiwezekani sema siwezi au mimi nitashindwa kukusaidia kwasababu wapo wengi wanaoweza Kufanya mambo magumu usiyoweza kufanya.

person using black desk calculator


5. SINA UHAKIKA

Ijue biashara yako.

Badala yake sema hivi, ‘Nalifahamu hili suala japo wapo wanaoshughulika nalo Au jaribu Kufanya kwa njia (hii) nyingine’.

Unaposema hunauhakika maana yake ni kwamba  hauijui vyema biashara yako au huna ratiba maalumu ya huduma yako kwahiyo unapaswa kuwa na uhakika wa huduma unayoitoa au kuwa na mtandao mkubwa wa watoa huduma wenzako ili wakusaidie kupata taarifa za kutosha.

Pia Soma : Namna biashara ya ‘network marketing’ ilivyonipeleka polisi


6. NITAKUTAFUTA BAADAE

Badala yake sema hivi, ‘Nimekuelewa ngoja nitafute majibu halafu nitakupigia au Nitakutaarifu nikupe mrejesho kamili Au Nakuthamini Sana ila namalizia kumhudumia mteja mara moja nitakupigia mimi muda siyo mrefu’.

Ukipigiwa simu na mteja usiikate hata kama upo busy ni heri uache iite na ukipokea usimwambie tu nitakupigia baadae bali msikilize kidogo kisha tumia kauli hizo hapo juu au kama sivyo andika ujumbe wa kumwomba akuvumilie kidogo labda upo kikaoni nk.

Jinsi unavyohusiana na wateja wako ina faida kubwa sana kwenye biashara yako, na moja wapo ya namna ya kuwa na mahusiano mazuri na wateja ni pamoja na maneno unayotumia unapoongea nao, vile unavyowafanya wajisiki wakija kupata huduma kwako. Jitahidi kuwa na kauli nzuri.Imeandikwa na Arafat Msuya

2 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »