Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Mambo 4 ya kuzingatia kwa wanaofanya kazi kutoka nyumbani (work from home)

Toka Corona ianze watu wengi wamelazimika kufanya kazi kutokea nyumbani.

Na kwa vike wote tunajua hali zetu za nyumbani zilivyo, ili swala ni gumu kiaina. Wengine wana watoto, tuna ndugu tunaoishi nao, uvivu, makelele, wageni, majukumu ya nyumbani na vitu kibao vinavyoweza kukuingilia kila unapotaka kufanya kazi.

Na uhakika wengi wamekumbuka kwenda maofisini maana kufanyia nyumbani si utani.

Hata hivyo leo ningependa nikushirikishe tips 4 zitakazokusaidia katika kufanya kazi kwenye ofisi yako hii mpya;

1. Tafuta muda ambao unajua huwa unanguvu ukiwa nyumbani

Muda ambao uko most productive kwako, je ni alfajiri kabla watu hawajaamka? Je ni usiku watu wakienda kulala? Je ni mchana baada ya watoto kulala?

Jua ni kipindi gani mwili wako unakuwa vizuri kufanya kazi lakini pia mazingira yako yanaruhusu.

2. Tengeneza mazingira ya kiofisi kwenye chemba unayotaka kufanyia kazi

Mazingira huwa yana changia katika namna akili yako inavyofikiria, ukitengeneza mazingira ya kiofisi katika chumba kimoja au sehemu ambayo utakuwa unaifanyia kazi kila ukiingia akili yako inatiki kuwa huu ni muda wa kazi.

3. Nyanyuka kitandani

Kuna siku ambazo unaweza kufanya kazi kitandani, sawa.

Kuna siku unajisikia tu kulala.

Kwa siku hizo, amka, fungua madirisha, oga na jiandae kabisa kama unaenda ofisini ili mwili wako nao uchangamke.

Kufanya kazi toka nyumbani sio kazi rahisi maana zamani mwili wako ulizoea kuwa nyumbani ni sehemu ya kupumzika. Hivyo mambo kama haya yanaufanya mwili wako taratibu uachane na hilo wazo.

4. Mwambie kila mtu nyumbani kwako kuhusu muda huo wa kazi

Kama umeshajua muda wako, au kama una simu za ofisi, mwambie kila mtu ajue muda wako, ya kuwa sasa hivi nitakuwa busy na kila mtu aheshimu ratiba yako hiyo.

Ukiwa na chumba cha kwenda ndio vizuri ili kila mtu ajue ukiingia kule unaingia kikazi.

Zaidi ya yote jitahidi tu kufurahia na kujipa neema katika kipindi hiki, hili swala sio rahisi na kila mtu ameguswa hivyo jionyeshe upendo na uvumilivu.

Ni mambo gani yanayokusaidia katika kufanya kazi kutoka nyumbani?

Eunice

2 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป