Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Random

Kimoyomoyo tunajali jinsi watu wanavyotufikiria

Watu wengi ni wepesi sana kusema kuwa sijali watu wananionaje au wananifikiriaje, lakini ukweli ni kuwa kuna asilimia chache za kujali ndani ya kila mmoja.

Tuanze na majirani zetu. Wengine wanatuona na wengine tumejenga ukuta hawatuoni ila tukikutana nao tunajali wanatufikiriaje

Je wanafikiria maisha yetu ni mazuri, je wanafikiria ni magumu, je wanafikiria tuna upendo nk

Kama vile tulivyokuwa busy kuangalia maisha ya wengine, wengine nao wako busy kuangalia maisha yetu.

Lakini ukweli ni kuwa kama vile tulivyokuwa busy kufikiria majirani zetu wanatufikiriaje, wao pia wako busy kufikiria sisi tunawafikiriaje.

Kwahiyo labda yale tunayodhani wanatufikiria, ni sisi ndio tunayafikiria kuhusu sisi, ni mambo ambayo ni mapungufu yetu wenyewe tunayojikosoa na sio wao.

Nimejikuta hivi karibuni nikijikataza kufanya mambo kichwani, au nikijikosoa mimi kwa kusema kuwa, ‘watu watakuwa wanasema mimi ni ….’ au ‘watu watafikiria hili na lile’

Mambo mengi najikataza kwa kufikiria vile watu watakavyonifikiria.

Ila pia nimejikuta muda mwingine nikijisemesha, ‘ni nani aliyekuambia kuwa watu wanafikiria hivyo’?

Kama si mimi ninayefikiria hivyo?

Je, ningeacha kuwaza watu wananifikiriaje, ningeishi maisha huru kiasi gani?

Ningefanya maamuzi gani?

Ningeacha kujikosoa kiasi gani?

Nawaza tu labda nikiacha kujikosoa mimi kwa kuwaza watu wananifikiriaje, labda nitaacha kujali watu wanafikiriaje.

Labda nikiweka kujali Mungu ananifikiriaje kuwa muhimu kuliko watu wanavyonifikiria labda hiyo itanipunguzia mawazo, kujikosoa na kujaribu kujibadilisha badilisha na kuwa vile nahisi watu watapendezwa na mimi.

Labda.

Labda watu wananifikiriaje niibadilishe na mimi najifikiriaje… Mimi najionaje, mimi natakaje?

Labda nitafanya maamuzi mazuri kwaajili yangu mwenyewe na sio ambayo nadhani yataniweka kwenye kufikiriwa vizuri na watu.

Je, watu wanavyonifikiria inaniongezea nini?

Eunice

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป