Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maisha ya Chuo

Mambo 5 ya kuzingatia unapochagua chuo | Your Guide to University Life

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Ni jambo moja kuamua usomee nini, na ni jambo la pili kuamua ukasomee wapi.

Nisikilize,

Tanzania Kuna vyuo vikuu zaidi ya 70, (vyuo 72 ndivyo vitadahili wanafunzi kwa ngazi ya degree kwa mwaka huu 2019) vinavyoweza kuhudumia zaidi ya wanafunzi 60,000 katika TAALUMA mbalimbali.
Lakini utalazimika kuchagua kimoja tu katika hivyo vingi ili uweze kusomea unachotaka kusomea.
Hivyo ni muhimu sana kuwa na sababu ya kwanini unachagua chuo fulani na si chuo kingine…

Wapo wanaochagua chuo kwasababu mbalimbali zisizojitosheleza kiumuhimu, kama vile kwasababu marafiki zao wanasoma hapo, au kwasababu ndicho pekee wanachokijua, kwasababu wamelazimishwa kusoma hapo na walezi, wazazi, ndugu,nk. Na wengine wapo tayari tu kusoma kitu chochote katika chuo chochote ilimradi wapate chuo..

Mimi nashauri uchague chuo ukiwa na sababu ya msingi kwanini unachagua hapo na siyo chuo kingine.
__________________________

Yafwatayo ni baadhi ya Mambo ya kuzingatia unapochagua chuo cha kwenda kusoma;-

1. Uwepo wa Taaluma unayoitaka kuisoma.

Kwa kuzingatia malengo yako , TAALUMA unayoitaka kusomea ndiyo itakayokuongoza, maana itakulazimu kuchagua chuo ambacho wanafundisha Taaluma unayoitaka.
Hivyo,jambo la kwanza baada ya kujua ni Taaluma gani unahitaji, Angalia ni vyuo gani vinaifundisha ili katika orodha hiyo uamue ni chuo kipi uchague.
(Kama TAALUMA unayotaka inapatikana katika vyuo zaidi ya kimoja, Nashauri uapply zaidi ya chuo kimoja ili kuwa na wigo mpana wa kuchaguliwa kwasababu ya ushindani unaoweza kuwepo).

2. Zingatia Vigezo vya udahili. (Entry qualifications)

Vipo vigezo vya jumla vya kuanzia (“minimum qualifications” kulingana na MWONGOZO wa TCU, ambapo ni kwanzia Cut off points ya 6 kwa TAALUMA za Afya na 4 kwa taaluma zisizo za Afya) ili uweze kudahiliwa chuo kikuu katika Taaluma Yoyote.
Lakini kila chuo kina vigezo vyake ili wakudahili katika Taaluma husika . Hivyo ni muhimu kuzingatia hilo kwa kulinganisha na matokeo yako.

Ni vyema kufahamu kuwa Vigezo vya kudahiliwa kusomea TAALUMA hiyo hiyo katika chuo fulani vinaweza kuwa tofauti katika chuo kingine.

3. Vigezo vya kifedha. ( Financial reasons.)

ADA NA MALIPO MENGINE.
-Vyuo vinatofautiana Ada kulingana na Taaluma husika, (japo vipo vinavyofanana ada.)
Pia kuna malipo mengine kama vile malazi (hostels), nk.

GHARAMA ZA MAISHA UWAPO CHUONI.
-Ukiwa chuoni utakula, utasafiri, utanunua vitu mbalimbali kwa matumizi binafsi, Makazi kwa watakaoishi off campus,nk. Gharama za maisha hutofautiana katika vyuo (ndani ya chuo na hata mazingira ambapo chuo kipo). Kuna mahala ambapo vitu bei ziko juu sana, Kuna mahala huduma nyingi hazipo hivyo utalazimika kuzitafuta mbali.

Haya yote ni ya kuzingatia pia unapoamua kuchagua Chuo gani ukasome.
Chagua chuo ambacho unaweza kumudu gharama za kifedha.

4. Mahala chuo kilipo (Geographical Location ).
-Ni muhimu pia kuzingatia Mahali chuo kilipo, kwa kuzingatia hali yako, Mahitaji yako, malengo yako na hata mazingira rafiki kwako kitaaluma na kuishi.

Maeneo yanatofautiana katika Hali ya hewa, upatikanaji wa huduma , umbali na kufikia,nk.
Kuliko kuishi mahali usipopapenda ni heri kuchagua mahali ambapo utaridhia kuishi kwa kipindi chote uwapo chuoni.

Makala inayoendana na hii: Mambo 3 ya kuzingatia unapochagua course

5. Zingatia mifumo na taratibu za kitaaluma katika chuo husika.

Fuatilia kujua ratiba za chuo husika zipoje.
(Kuna vyuo ambavyo vinashift ya ratiba kwa masomo ya day time na evening, kuna vyenye shift za semester kutofautiana kulingana na miaka ya masomo.,nk.

Fuatilia kujua Taratibu za kimasomo zipoje katika chuo husika, ikiwemo mifumo yao ya kupima wanafunzi katika mitihani, misimamo (standards) zao katika Taaluma.

Pia Mifumo na taratibu za chuo husika katika kusupport ubunifu na initiative za wanafunzi.
Fursa za kitaaluma na kijamii zilizopo katika chuo husika.
(Mfano kuna vyuo ambavyo mbali na kufundisha taaluma mbalimbali, lakini pia wana shughuli mbalimbali za kuendeleza wanafunzi wake kitaaluma. Kama vile kutoa motisha kwa wanaofanya vizuri kimasomo, kuwasafirisha nchi za nje ili kujiendeleza kitaaluma,nk)

KWA KUONGEZEA:

-Hayo ni baadhi tu ya mambo ya kuzingatia, unaweza ukawa na vigezo vingine zaidi.

-Kwa wale wa ngazi ya diploma, mambo hayo hayo pia waweza kuzingatia katika kuchagua ukasomee wapi.

-Kuna kitu kinaitwa PROSPECTUS. Ni kijitabu Chenye taarifa zote A-Z kuhusu chuo husika. Kila taarifa unayohitaji kufahamu juu ya chuo fulani, ipo humo.
(Tafuta PROSPECTUS ya chuo husika kwenye Website za chuo au moja kwa moja chuoni , ili uweze kukifahamu chuo na mambo yake yote kwa urahisi).

-Waweza pata taarifa za chuo pia kupitia wanafunzi wa chuo husika au kwa urasmi zaidi katika tovuti za chuo husika.

-Kuna mambo mengine katika hayo yaliyoelezewa huenda kukawa na changamoto ambayo yaweza kuvumilika, hivyo Jipime na kama utaweza basi usiache kuapply.

-Unaweza usipate kabisa unapopataka kwasababu mbalimbali ikiwemo ushindani. (Isikushangaze)

Ikitokea hivyo, basi usikate tamaa. Chagua ambapo angalau panaweza kukufikisha unapotaka kufika kitaaluma, huku ukifikiria namna gani utazikabili changamoto zilizopo.

Mfano : ninafahamu wanafunzi ambao ,kwasababu za kifedha walitamani vyuo vyenye gharama nafuu ili waweze kumudu, lakini ushindani uliwakosesha na wakalazimika kuapply vyuo vyenye gharama kubwa sana. Changamoto Hii haikuwakwamisha badala yake walitafuta njia mbadala ya kutafuta wadhamini kwajili ya kupata msaada wa kifedha katika masomo yao.

(Huo ni mfano tuu. Changamoto zinatofautiana, hivyo tafuta pia njia mbadala kuikabili changamoto inayokugusa wewe).

Kwa kuhitimisha, nakutakia kila la heri katika mchakato huu wa kuapply vyuo na kuelekea kutimiza malengo yenu kitaaluma..

Adam Machalila
@prepare_for_university (Instagram page)

3 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป