Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Mambo ya kuzingatia unapochagua kozi ya kusoma chuoni

(Bonyeza Hapa kusoma makala mbalimbali zitakazokuongoza kwenye mambo yanayohusu chuo)

(Bonyeza hapa kupata mchanganuo wa kozi mbalimbali unazoweza kuzisoma kutokana na kombi uliyoisoma)


Kuchagua kozi utakayoisoma chuo ni moja ya maamuzi makubwa sana unayoweza kuyafanya kwaajili ya maisha yako. Maana yanaathiri utakachosoma kwa miaka yako utakayokuwa chuo na utakachofanya baada ya chuo na pengine maisha yako yote.

Mimi nilishauriwa tu chagua kozi fulani, chagua chuo fulani ni kizuri. Sikujua nini napenda wakati naenda chuo, ukweli ni kuwa bado nilikuwa sijajitambua.

Sikuchukua muda kujouliza maswali muhimu, sikuchukua muda kufikiria kwa mbaki na kwa vile nilikuwa bado sijajitambua nilikubali tu wazo lolote nililopewa ili mradi niende tu chuo, nipate boom nimalize.

Hauna haja ya kufanya kama nilivyofanya mimi, haya hapa ni mambo ya kuzingatia unapochagua chuo;

Angalia kombi uliyosomea na kazi ya ndoto yako

Kombi uliyosomea inakupelekea kujua kozi gani unaweza soma chuoni.

Lakini pia ni kazi gani ambayo toka zamani ulikuwa unatamani kuifanya? Na je kozi hiyo inakupelekea kuifanya hiyo kazi?

Angalia Passion yako

Nikuambie siri, ukianza kazi unaweza kufanya muda mrefu sana katika hilo eneo ambalo unakuwa umesomea kutokana na kozi hiyo.

• Je, una passion na hayo mambo?

• Je, unaweza kuona miaka yako yote au mingi baada ya chuo ukifanyia kazi hicho kitu unachotaka kukisomea au kukaa kwenye eneo hilo la kazi/career?

Vitu gani vinakufanya upate furaha ya kuishi? Na hivyo vitu vinaingiaje kwenye kazi utakayoipata kwenye hii kozi unayotaka kuisoma?

• Ujuzi utakaoupata ndio utakaokusaidia kwenye kazi unayoitaka?

Jiulize kwanini unataka kusoma kozi hiyo

Mimi nilisoma kozi hiyo kwasababu nilishauriwa na jamii na pia nilikuwa bado sijatambua passion yangu ni ipi na nilikuwa naogopa kuwa passion yangu inaweza isiwe na soko lakini pia nilikuwa nataka nipate ajira nilikubali kwa vile niliambiwa kuna ajira nyingi kwenye kozi hiyo.

Sababu zako ni zipi?

• Upatikanaji wa ajira?

• Gharama za kujisomesha kozi hiyo unazimudu?

• Kozi hiyo unapata boom 100%

Sababu zako ni zipi? Jiulize na ujijibu kwa ukweli.

Hayo ni mambo matatu ambayo naona ni ya muhimu sana kuyafikiria unapochagua kozi, naamini kozi nzuri ni ile utakayochagua kwa kubalance haya mambo. Lakini kumbuka kwenye maisha furaha yako na amani ni jambo la muhimu sana.

Usiwe na presha sana hata ukichagua kozi ambayo baadae ukaona hauitaki, unaweza kubadilisha. Wewe bado ni mdogo sana hata ukiwa na miaka 30,40 unaweza kubadilisha kazi. Maisha ni safari. Usiwe na stress.

Eunice


(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomaliza chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Pia unaweza soma : Vitu vya kuzingatia unapochagua chuo

Na Kwa waliochaguliwa kozi ambayo hawaipendi

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate »