Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Dondoo za Maisha

Jinsi ya Kujiamini | 10 tips

Nitakuwa nadanganya nikisema najiamini kila siku, honestly kuna siku sijiamini kabisa… Ila most days najiamini… And I think that’s okay.

Kuna ile woga wa kabla ya kuongea mbele za watu ambao unaupata, na kuna ile kutokujiamini kufanya jambo lolote lile. Niwe mkweli, naenda kushare tips zinazofanya kazi kwangu, nawewe labda ukijaribu zinaweza kukusaidia. Tunahitaji kujiamini kwenye maisha, kujiamini tukiwa tuna present vitu, kujiamini kuingia maofisi ya watu, kwenye interview , kujiamini kwenye maamuzi tunayoyafanya nk.

Kujiamini we we mwenyewe ni jambo la muhimu sana hasa katika hii dunia ambayo vitu vinatuvunja moyo sana.

Inaweza ikaendana kidogo na kujitia moyo, ukijiamini unaweza, unaweza kujitia moyo we we mwenyewe na kufanya jambo fulani unalotaka kulifanya maana utaendelea kujitia moyo.. Tukitegemea kutiwa moyo na watu inaweza kutokea ila sio jambo la kulitegemea maisha yetu yote.

Sasa basi njia /vitu ninavyofanya ili kujiamini:

1- Kujiandaa kiukamilifu
Kama naenda ofisi fulani, najipanga kabisa nitakayoyasema au kujua ofisi kidogo ikoje. Hii inanisaidia hasa kama naenda mwenyewe, nikiwa na mtu ninayemjua nitajiamini kwasababu Niko na yule mtu… Ila nikiwa naenda mwenyewe najiandaa, kama ni presentation naisoma vizuri na kujiandaa nitakalolifanya mwanzo mwisho ili niwe vizuri.

Lakini pia kujiandaa kama ni mavazi na kuwahi, ukiwahi unapunguza kutokujiamini kwasababu unaona kila kitu umekifanya kwa usahihi.

2- Kujiongelesha mwenyewe (maongezi chanya)

Hii ukiwa na kioo ndio inanoga, jiambie mwenyewe kuwa unajiamini, unaweza, unaenda kushinda, wewe ni bora na chohote unachotaka kujiambia ili ujisikie unajiamini.

3- Jitokeze mbele (uwe kimbelembele)

Ukijitokeza kabla haujachaguliwa unapunguza kutokujiamini. Ukisubiri uchaguliwe, mfano darasani unakuwa hauna muda wa kujiandaa. Ila ukiwa kimbelembele unakuwa na muda wa kujiandaa lakini pia kwasababu umejichagua mwenyewe sio rahisi kuaibika. (Wait, hivi kimbelembele inaandikwa na l au r?????, commet please kama unajibu.)

4- Kujua my potential, weakness and strength

Hata katika siku ambayo najiona Niko down, huwa najikumbusha my potential, Mimi ni nani na ubora wangu. Hii inanisaidia kurudi katika mstari na kujiamini tena. Ukijua strength na weakness yako inakusaidia kujiamini hata siku ambazo you feel like hajiamini.

5- Kumuamini Mungu (na kile anachosema kuhusu wewe)

Hii ingekuwa point ya kwanza, ila honestly ukimuamii Mungu kuwa anaweza na wewe ni wake… Ukiamini Yale yote anayosema kwenye Neno lake kuhusu wewe, inakutia moyo na kukufanya ujiamini (kama vile Gideon, Joshua a wengine wengi ambao walifanya makubwa kwa kujiamini kwavile walijua Mungu ni anasema nini juu yao.

6- Kujua kuwa unapendwa na unasupportiwa

Kujua kuwa unapendwa na unasupport ya watu kuna kufanya ujiamini pia, ila hii sio ya kuitegemea sana kwani kuna muda hao hao unaotegemea ndio wawe source ya kujiamini kwako wakaacha kukusupport kwenye swala lingine ambalo we we ulidhani wangekusupport, ikitokea situation kama hiyo basi rudi kwenye point ya 5.

7- Kupata opinion ya watu unaojali opinions zao

Hasa kama unaenda kuongea mbele za watu kwa mfano, ukifanya majaribio kwa kuongea mbele za wat mbao unajua hawawezi kukudanganya lakini pia opinion yao ina maana kwako, basi wafuate wao kwanza kabla ya kwenda kuongea.

8- Kujikumbusha kuwa naishi Mara moja

Hasa kwenye maswala yanayohitaji kutake risk, ninaposhindwa kujiamini, kunajikumbusha kuwa ninaishi mara, na kikubwa kitakachotokea ni kushindwa na hilo sio jambo baya ukilinganisha na majuto. Ni heri uzeeni nijisikie vibaya kwa kushindwa kuliko nijute kwa kutokujaribu na muda wa kujaribu sina tena.

9- Kuacha kuona aibu kwenye kila linalotokea

Aibu sijui niielezeje, ila tu niseme inaturudisha nyuma hasa wasichana. Ndio inayotufanya tuogope kujaribu kwa kujali watatuonaje au kujiweka nyuma nyuma . Kujali watu watakuonaje kusikufanye uache kuishi potential yako, kwasababu mwisho wa siku kutimiza kusudi lako ni jambo litakalo Fanya uone thamani ya maisha yako, na sio vile watu wanavyokuona. Tuache kujiuliza swali la ‘nikishindwa watanionaje?’ Badala yake tujiulize, ‘what if I fly?’. Hata Diamond wakati anaanza hatukumuelewa ila sasa watu wanamuelewa, what if you fly?

10- Kujua Mimi ndio kiongozi wa maisha yangu (kutake responsibility)

Niongezee pia kuwaona watu ( hasa wakubwa zangu mfano; boss, walimu nk) kama watu kama Mimi. Lakini pia kuwa wapo kunisaidia wapo kwaajili yangu. Pia Kujua kuwa this is my life I am responsible for it, imenisaidia Kujua hata kama sijiamini kwenye jambo Fulani inabidi nilifanye, kwani nisipofanya nani atafanya?

Na marafiki zangu nao wanasema:

Personally I always believe in my abilities… so whenever I feel anxious there’s a voice inside of me whispering “you can do it and turn out things for the best” …. that’s actually my mama’s voice, she’s the very first individual to trust in me in so many ways even when I fail.
Therefore, being confident for me it’s a two way game… one for the people who trust me and secondly from accepting the fact that I can do anything in the first place

~Christine

– I talk to myself positively
– I eat?
– Wear my best outfit
– Always feel confident when I’m in jeans and sneakers

Kudzie (Blogger at Kudzie Home)

Hizo ndo tips kumi zinazonifanya niendelee kujiamini (+ bonus kutoka kwa marafiki).

Asante kwa kusoma,

Eunice

9 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป