Mara nyingi huwa tunatamani kujitambua, na tunasikia watu wengi wakituambia umuhimu wa kujitafuta na kujitambua, lakini kama wewe umepitia hali ninayopitia mimi basi umejiuliza sana, nawezaje kujitafuta?

Kama upo kwenye kipindi cha kujiuliza hivyo naomba nikumbe njia kadhaa ambazo zimenisaidia mimi kujitafuta, ambazo na uhakika zinaweza zikakusaidia na wewe pia.

Ila kabla sijaanza naomba niseme kuwa kujitafuta ni kitendo kinachochukua muda, sio jambo la mara moja kwahiyo usijihisi una mapungufu mengi ambayo hauwezi kuyafanyia kazi au usijihisi safari ni ndefu hauna haja ya kuianza, kujijua wewe mwenyewe ndio raha ya maisha maana wewe mwenyewe ndio utaishi maisha yako na wewe kila siku, ni vizuri ukijijua.

Njia nitakazokushirikisha leo ni;


1. Kujisikiliza

Utashangaa ni mara ngapi huwa hatujisikilizi. Ni mara ngapi maamuzi, au maisha tunayoishi tunafanya kwaajili ya wengine. Hata leo tu jiulize umetumia muda gani kutulia na kusikiliza jinsi unavyojisikia au kitu unachokitaka, ni mara ngapi?

Njia rahisi ya kujijua wewe, ni kujisikiliza wewe na pia…

2. Kujiuliza maswali

Maswali magumu, na kukaa chini kusikiliza majibu uliyonayo, na kwanini unayohayo majibu uliyonayo.

Katika maisha ya sasa hivi rahisi kuwa mfuata njia na sio mfikiriaji mwenyewe, ukijiuliza maswali utajijua vizuri, utajua msimamo wako kuhusu mambo fulani nk.

3. Kwa kusoma vitabu

Nakumbuka kuna kitabu kimoja ambacho nilisoma kiliniliza sana na nikagundua kuhusu jambo ninalolipenda kupitia hicho kitabu maana nilikuwa sijui kama moyo wangu unaguswa katika eneo hilo.

Vitabu vinakufungulia dunia na mawazo, na kukufanya uone mbali ya zaidi ulipo, lakini pia kwa kuona mbali, unaona na karibu pia, unajioma ndani ya moyo wako.

4. Kujaribu kufanya vitu vipya mbalimbali

Unapofanya vitu mbalimbali unajifunza na kujijua zaidi, kipi unaweza, kipi hauwezi, kipi unapenda, wapi uko vizuri, kipi kinakukasirisha, kwanini kinakukasirisha nk.

5. Kuwauliza watu kuhusu wewe

Kuwauliza watu wanakuonaje au kukufikiriaje hasa watu unaojua wana nia nzuri na wewe.

Kuna mtu alinifundisha kitu, alisema kuna mambi manne dunia;

– Mambo unayoyajua kuhusu wewe lakini pia watu wanayajua

– Mambo unayoyajua kuhusu wewe ila watu hawajui

– Mambo usiyoyajua kuhusu wewe ila watu wanayajua

– Mambo usiyoyajua kuhusu wewe na watu hawayajui

Kuwauliza watu wanaokujua vizuri wanaweza kukusaidia kujua mambo usiyoyajua kuhusu wewe ambayo wao wanayajua kwa kukuangalia labda au kwa kufahamu na kuona ubora wako.

6. Kujifunza kutoka kwa wengine

Kwa kuwa hakuna jipya chini ya jua, sio vibaya ukipenda kitu kwa mtu ukajifunza kutoka kwake na pia ukakichukua. Hiki pia kinaweza kuwa kipimo cha kujitambua kwako kwa kuangalia mambo unayojifunza kutoka kwa wengine.

7. Kumuomba Mungu

Njia ya muhimu kabisa ni kumuomba Mungu, Yeye aliyekuumba anakujua vizuri. Kwahiyo unapojitafuta ukimuomba na kumsikiliza Yeye ni rahisi sana kujijua. Ni kama kwenye Biblia ambapo Gideon alikuwa anaitwa shujaa na Mungu na yeye anashangaa (Waamuzi 6:12), kumbe Mungu alikuwa anajua amemuumba kuwa shujaa ila yeye alikuwa hajui.


Je, kuna njia nyingine unayoweza kuitumia kujitafuta ambayo sijaitaja?

Niambie kwenye comments

Eunice

You May Also Like

4 thoughts on “Jinsi ya Kujitafuta

 1. Kaijage Leonard

  Nice post, thanks a lot. But explanations aren’t direct to catch up. I feel like I need some more details on each point. All in all work work is amazing.

  1. Eunice Tossy

   Thank you for reading Kaijage.

   Sawa sawa, will work on that. Might even make a video to explain all the points in more details.

 2. Mambo ya kuzingatia unapochagua kozi ya kusoma chuoni – Eunice Tossy

  […] Mimi nilishauriwa tu chagua kozi fulani, chagua chuo fulani ni kizuri. Sikujua nini napenda wakati naenda chuo, ukweli ni kuwa bado nilikuwa sijajitambua. […]

 3. Bonge : Jinsi kuukubali mwili wangu ulivyo kulivyonifanya nijiamini na nijione mrembo – Eunice Tossy

  […] Mimi nimechoka kujibana kwenye maisha wakati naweza nikaenjoy maisha kwa asilimia 100, sijawahi kujaribu diet kwasababu sipendi kuishi maisha yangu nikihesabu kilo ninazokula, nikiangalia kila kitu na kujinyima vitu, nimechoka kuchukia mwili wangu kwa kutokuwa size fulani na kusikia aibu kwenda mitoko na kuenjoy maisha yangu kwavile nasubiria nifike size fulani ambayo inakuja baada ya kujiadhibu, kuadhibu mwili wangu, kujiadhibu mimi. […]

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป