Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Guest Post,  Maswala ya Pesa

Jinsi ya kumsaidia mjasiriamali mdogo kukuza biashara yake mtandaoni

Hakuna mtu ambaye anaweweza kufanikisha jambo bila msaada wa mtu au watu wengine. Tunaishi kwa kutegemeana. Unachokitafuta wewe kipo kwa mtu mwingine.

Katika dunia yetu ya kidigitali, ni rahisi kuwa sehemu ya msaada mkubwa kwa wajasiriamali wanaotafuta kukuza biashara mtandaoni. Unaweza kufanya hivyo bila hata ya kutumia pesa.

Jinsi ya kusaidia kukuza biashara ya mjasiriamali mtandaoni

1. Follow page yake ya biashara. Inaweza kuwa ni instagram, twitter au facebook – popote unapoona unaweza kumfollow fanya hivyo. Hii haigarimu pesa yoyote.

2. Toa Comment , Like au Share post za bidhaa zake ili zipate kuonekana kwa wengi. Kumbuka wewe binafsi una followers ambao nao wana followers, hivyo ukishare au kucomment kweny post ya mjasiriamali huyu, unaipa nafasi post yake kufika mbali zaidi. Hii nayo haikugarimu hela.

3. Toa maoni, reviews au ratings kuhusu huduma yake kwenye page yake Google My Business, kwenye App yake playstore, au kwenye listing directories zingine.

Lakini pia ukitumia bidhaa yake ukaipenda unaweza iweka hata WhatsApp status au kuiposti na kutag pages zake mitandaoni.

4. Weka picha ya eneo au bidhaa yake na shiriki kuhakiki (verify) taarifa zake kwenye ramani za google. Pia unaweza posti picha yako pia ukiwa eneo la biashara yake ukaweka google map.

5. Pia wajuze marafiki zako juu ya bidhaa zake.

Pia Soma : Hii ndio sababu mitaji mingi ya biashara mpya hufa

6. Cha mwisho, acha kuponda biashara ya mtu mtandaoni. Kama kuna kitu unaona anakosea ni busara kumtumia ujumbe inbox na kumweleza.

Ukifanya yote haya, utakuwa hujatumia kiasi chochote cha pesa, lakini utakua umemwezesha mtafutaji mwenzako kufikisha bidhaa kwa wateja hivyo kujipatia kipato cha kuendesha maisha yake.

Kama umeelewa somo, nenda kafanye hivyo kwenye biashara ya mjasiriamali unayemjua. Kugusa maisha ya watu wengine si lazima uwe mtu mwenye pesa nyingi sana. Kusaidia kukuza online visibility ya biashara ya mtu ni aina nyingine ya utoaji. Tuendelee kuinuana.


Imeandikwa na Shukuru Amos

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป