Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Maisha ya Mbeya kwa wanachuo na jinsi ya kufurahia kusoma mkoa huo

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Mimi nimesoma Mbeya University of science and Technology kwa miaka minne.

Kama wanafunzi wengine tunaoamini UDSM ndio kila kitu nilipochaguliwa Mbeya nilihuzunika sana, ila nilijifunza mambo mbalimbali na mpaka nikabadilisha mtazamo, nilipoenda Mbeya kusoma nilitumia muda wangu vizuri kwenye mkoa huo nakuhakikisha nafaulu huku nakula bata kwa ukamilifu, mwisho wa siku mkoa wa Mbeya ni sehemu muhimu sana kwenye maisha na moyo wangu. Ulinibadilisha na kunikuza vizuri.


Hali ya hewa, vyakula na malazi

Mbeya ni mkoa ambao una baridi sana kwahiyo kama unajiandaa kwenda paki vizuri, Mbeya utashuhudia misimu, kuna wa baridi, mvua, vumbi na jua.

Mbeya kuna matunda na vyakula vingi, tena bei rahisi sana. Yani maparachichi, ndizi ndio nyumbani. Kitimoto kwa wale walaji, ndio usiseme.

Kama unapenda kukaa nje ya chuo, malazi Mbeya ni bei ya chini sana, yani sana. Tena nyumba yenye choo na maji ndani, wanapangisha bei rahisi. Kiujumla maisha ya Mbeya si gharama, vyakula kama utaweka bili au utapika sio gharama, usafiri pia nk.

Ni sehemu nzuri ya wewe kuwa mwanachuo kama unaboom au haujapata boom.

Watu wengi wanaogopa au wanadharau maisha ya mkoani ila mikoani ni sehemu nzuri ya kuanzia maisha au kuishi maisha mazuri bila gharama kubwa.

Masomo

Vyuo vingi vilivyopo Mbeya ni vinabana sana kimasomo, kwahiyo ukifika kaza. MUST ni chuo cha mainjinia kwahiyo tulipokuwa pale tulikuwa tuna kaza, kwahiyo jitahidi usipuuzie masomo lakini pia unaweza kula bata kidogo ili kupumzisha akili.

Mkoa wa Mbeya ni mzuri sana kwa kusoma chuo kwavile japokuwa kuna matukio kama Fiesta nk, hauna kelele nyingi kama Dar, hauna vitu vingi vya kukushawishi na kukufanya ushindwe kuweka umakini kwenye masomo.

Kujivinjari

Kuna sehemu nyingi za kutembelea Mbeya, kuna Mbeya Pazuri, kuna Mbeya Hotel kama unapenda kula piza, kuna Ifisi ambayo pia ina sehemu ya kuona wanyama, kuna ziwa Nyasa – Matema beach, kuna maji moto, kimondo cha Mbozi, kuna kupanda milima Mbeya kama unapenda kupanda milima, Ziwa Ngosi, daraja la Mungu, kuna boda ya Tanzania na Zambia, na Tanzania na Malawi yani kuna sehemu nyingi za kufanya utalii wa ndani na kujivinjari Mbeya (ulizia waliokutangulia au zurula).

Hata kama unaenda na hauna mtu unayemjua, usiogope utakutana na watu, watakuwa marafiki zako na Mbeya utaiona kama nyumbani kwasababu unawatu unaowafahamu hapo. Wengi utakutana nao pia hawana mtu wanayemjua hivyo mtakuwa pamoja.

Soma Makala Hii : Njia 6 za kupata marafiki

Ni matumaini yangu kuwa ukienda Mbeya utafanikiwa kusoma na kufaulu na kuzurula mkoa huo na kuufurahia kama mimi nilivyofanya. Usiogope


Kama unaswali lolote kuhusu maisha ya Mbeya kama mwanachuo usisite kuuliza nitafurahi kukujibu, usiache kufollow @maishayachuo Instagram, ambapo nashea dondoo zinazowasaidia wanachuo kukabiliana na jambo lolote chuoni, uisache pia kunitumia DM kama unalolote la kuniambia.

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate »