UDSM ni chuo kizuri sana.

Kina kozi nyingi.

Kipo mjini.

Kuna fursa nyingi.

Unanikumbusha nilivyomaliza kidato cha sita nilikuwa nataka nisome UDSM, kozi yoyote ile ili mradi tu niwe UDSM. Kwahiyo nikaapply kozi tatu tofauti katika nafasi zangu tano, zote niliapply UDSM, mbili zilizobaki, nikajaza UDOM na ya mwisho nikajaza Mbeya University of Science and Technology (MUST).

Nikachaguliwa MUST.

Niliumia sana. Yani nimejitoa nafasi tatu zote lakini sijachaguliwa??

Yani nimeweka kozi tofauti tofauti japokuwa nilikuwa sizipendi lakini bado?

Niliumia sana.

Ila nilipata nafasi ya kufikiria, hivi kwanini wengi tunapenda kusoma UDSM?

Je, ni kwasababu kipo Dar?

Kuna fursa nyingi? Au ni chuo bora na maarufu kwahiyo kusoma hapo kunakupa heshima?

Nilifundishwaga kuwa ukitaka kuchagua chuo, chagua chuo ambacho kimejikita kwenye jambo unalotaka kusoma, kwahiyo kwa mfano mambo ya biashara, ni vizuri ukisoma IFM kuliko UDSM, sio kwamba UDSM ni kibaya ila IFM ni chuo maarufu kwaajili ya biashara hivyo wanaujuzi na wamejikita eneo hilo sana.

Mambo ya sayansi na engineering, MUST na DIT vinaweza kuwa bomba zaidi, sio kwasababu UDSM hakifanyi vizuri eneo hili ila hivi vimejikita kwenye hili eneo pekee hivyo hata mazingira yanakuwa mazuri kwa wewe ukisoma engineering vyuo hivyo.

(Soma : Mambo 5 ya kuzingatia unapochagua chuo)

Kwahiyo jiulize kwanini unapenda UDSM, je ni jina tu na mjini au kweli kozi unayoipenda pale ndio itakufungulia milango zaidi…

Wakati naenda MUST sikuwa na furaha kwasababu ndio nilikuwa nasafiri nje ya mkoa kimasomo kwa mara ya kwanza lakini pia sikuwa naenda UDSM kama nilivyotamani, lakini nilijifunza kuwa inaweza kuwa adventure ya kujua mkoa mwingine lakini pia kuna vyuo vingine ambavyo ni vizuri pia, hasa kwa kozi niliyokuwa naisoma – Mechanical Engineering.

Hivyo kwa wewe unayependa kusoma UDSM, ni kwanini unapenda kusoma hapo? Na ukikosa, je ukowazi kuamini kuwa vyuo vingine pia vinaweza kukupa experience nzuri ya chuo ambayo uliidhani ungeipata UDSM? Unaweza kuenjoy sehemu nyingine au ndio utaishi kwa maumivu, kujuta na kunun’gunika ukichaguliwa chuo kingine?

Ukikosa kuchaguliwa UDSM haimaanishi hauna akili au umeshindwa, utakuwa umepata chuo kingine, furahia umepata chuo.

Na ukichaguliwa UDSM sio kwamba ambao hawajachaguliwa hapo hawana akili au wewe ni bora zaidi ya wao, ni chuo kama vyuo vingine, thamani yako ni zaidi ya chuo unachosoma.

Follow @maishayachuo Instagram ili kupata dondoo za maisha ya chuo.

Eunice

(Soma : Mambo ya kuzingatia unapochagua kozi ya kusoma chuoni)

(Angalia Kozi unazoweza kuzisoma kwa combi yoyote uliyoisoma)

You May Also Like

1 Comment

  1. Maisha ya Mbeya kwa wanachuo na jinsi ya kufurahia kusoma mkoa huo – Eunice Tossy

    […] Kama wanafunzi wengine tunaoamini UDSM ndio kila kitu nilipochaguliwa Mbeya nilihuzunika sana, ila n… nilipoenda Mbeya kusoma nilitumia muda wangu vizuri kwenye mkoa huo nakuhakikisha nafaulu huku nakula bata kwa ukamilifu, mwisho wa siku mkoa wa Mbeya ni sehemu muhimu sana kwenye maisha na moyo wangu. Ulinibadilisha na kunikuza vizuri. […]

Share Your Thoughts With Me

Translate Ā»