Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya Chuo

Vitu 9 vya kufanya katika miezi ambayo unasubiria kwenda chuo

(Tembelea maishayachuo.com kupata makala, dondoo na msaada kuhusu chuo kutoka kwa waliomaliza vyuo)


Hongera sana kwa kumaliza form six, ni hatua kubwa sana uliyofikia. Haijalishi umepata matokeo uliyoyategemea au ambayo haukuyategemea, kumaliza form six is an accomplishment in life, hivyo hongera.

Kuna miezi kama mitano mpaka kwenda chuo, yani una muda mrefu sana wa kusubiria chuo kabla ya kwenda chuo ni kabisa.

Kuna wale walioenda jeshi, ambao pia at least wanapata kutumia miezi yao mitatu, Ila Kuna wale ambao hawakuchaguliwa jeshi hivyo wapo muda mrefu nyumbani bila kufanya chochote na unajiuliza naweza kuutumiaje muda wangu huu I got you covered.

Watu wanasema you only live once, na muda ni Mali. Kwa hiyo miezi yote hiyo ni Mali, inaweza kukuongezea kwemye maisha lakini pia inaweza ukaitumia vizuri kabla haujaenda chuo na kuwa busy na hivyo kushindwa kuwa na muda huo tena maishani

You never live the same moment twice, so miezi hii unaweza uka;

1. Utumia kuwa karibu na ndugu zako au familia… Ukishanza chuo utakuwa busy kuwa karibu nao kama ulivyokuwa, na kama ukipata chuo mbali na nyumbani basi hautopata muda was kuwa karibu nao kama ulivyokuwa.

2. Jifunza skills mbali mbali online… Kama unasmartphone, unaweza kujifunza chochote unachotaka kujifunza bure mtandaoni, kwa kutumia YouTube videos ama online platform nyingine zinazofundisha skills kama graphic designing, photography no

3. Jifunza computer na course nyingine za muda mfupi zinazotolewa na vyuo ama sehemu mbali mbali wanazofundisha short course

4. Safiri sehemu mbali mbali ambazo haujawahi kwenda, unaweza ukasafiri kutembelea ndugu na jamaa

5. Soma vitabu na kujifunza kupitia waliokutangulia na kujifunza hekima zao (unaweza kusoma kitabu hiki kinachotoa muongozo wa maisha ya chuo ili ujue na upate majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu jinsi maisha ya chuo yatakavyokuwa, bonyeza hapa kukipata kitabu hicho)

6. Pata tempo sehemu ya kujishikiza au volunteer sehemu.. Hasa ukiomba sehemu zinazoendana na course uliyoomba ili ukapate background ya kitu unachotaka kukisomea. Kufanya tempo inasaidia kujua kama ungependa kusomea unachoenda kusomea au ubadilishe, as well as unaweza ukawa unapata hela Kwenye tempo pia. Ingawa tempo ni ngumu ukapata, but ni vizuri kutafuta pia usivunjike moyo.

7. Kufanya research ya chuo utakachosoma na course.

8. Kupumzika haswa kwasababu umesoma muda mrefu na huu ni muda mchache wa kupumzika ili kwenda kusome tena, so pumzisha akili, enjoy this resting time, while you get ready to go back to studies.

9. Fanya shopping ya vitu utakavyovihitaji ukiwa chuo.

I hope utaweza kutumia muda wako huu vizuri, and I wish you all the best wakati unasubiria kwenda chuo.

Eunice

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)

Share Your Thoughts With Me

Translate »