Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

serious ethnic young woman using laptop at home
Maisha ya Chuo

Kwa anayefikiria kuacha chuo…

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Bado nakumbuka mara ya kwanza nilipojisikia na kuanza kuwaza kuhusu kuacha chuo, na hiyo mara ya kwanza haikuwa ya mwisho, kutoka mwaka 2014 mpaka mwaka 2018 kipindi nasoma Mbeya University of Science and Technology kuna mara kadhaa ambapo mawazo ya kuacha chuo yalinijia na yalikuwa yanakuja kwasababu mbalimbali.

Kuna muda nilifikiria kuacha chuo kwa kuwa masomo yalikuwa magumu sana, semster niliona siwezi toboa, kuna muda nilifikiria kwa kuwa nilikuwa na changamoto ya kiuchumi, muda mwingine changamoto nyumbani mzazi alikuwa anaumwa, na muda mwingine nilifikiria kuacha chuo kwa vile nilikuwa na kesi na mwalimu (hii stori nitasimulia siku nyingine).

Pia Soma : Mambo ya kufanya kama umepoteza mood ya kusoma

Kwasasa nilipomaliza chuo nashukuru kwa kuwa sikufanyia kazi mawazo yangu, naelewa kuna wengine wanakuwa kwenye hali ambazo inabidi kweli waache chuo, mfano labda wamepata kazi na hawana muda au sababu yoyote ile ambayo inawafanya waache, napenda kusema kuwa naelewa na sipo hapa kuhukumu uamuzi wa mtu kuhusu maisha yake ila kama unafikiria kuacha chuo ningependa ujue hili;

  • Kama ni kwasababu ya changamoto, jikaze. Tafuta msaada wa kupata suluhisho ya changamoto zako, changamoto zipo kwenye maisha na unapozipitia chuo zinakufundisha hata jinsi ya kukutana nazo mtaani, chuoni kugumu lakini na wewe pia unaweza kustahimili huo ugumu mpaka mwisho. Jaribu kujiuliza kama wazo la kuacha chuo linakuja kama njia ya kukimbia tatizo au kweli ni jambo linalohitajika kufanywa? Na kama ni njia ya kukimbia tatizo basi, tafuta namna ya kupata suluhisho la tatizo.
  • Kuna muda ukifika unaweza pata shida ya kuona umuhimu wa elimu unayoisoma mtaani, hivyo unaweza fikiria kuacha, nakumbuka mwaka wa tatu mimi nilipata mawazo ya kuacha chuo kwasababu hii. Nikushauri tu jikaze, nikushauri tu elimu inafungua mawazo, nikushauri tu kuwa ukiacha sasa unakuwa umepoteza miaka yako ya nyuma, kama hauna kitu cha tofauti unachofikiria kukifanya kwa wakati huu ni mawazo tu ndio unayo basi malizia tu huo muda uliobakia huku ukifikiria kuhusu mambo ya kufanya tofauti na elimu yako au jinsi ya kuitumia elimu uliyonayo kujiajiri kitaa.
  • Kuna muda ni woga, wa maisha ya chuo, wa masomo, wa kufeli. Kuna muda unaona bora ulipotoka vidato kuliko huku unapokwenda, inaeleweka kwa vile masomo ni mapya, inaeleweka kwa vile wahadhiri wanakutisha nk. Ila usiache chuo kwasababu hii, pambana, soma, discuss na wengine, solve past papers, ongeza juhudi. Unachokifikiria kinaongezeka ukubwa na ugumu akilini mwako, unapoendelea kufikiria kuacha chuo kwasababu ya chuo kilivyo unashindwa kutumia nguvu hivyo kwenye masomo, kwenye kusoma ili ukutane na changamoto za chuoni. Usiogope, uzuri wa chuo, semester ijayo itakuja na changamoto nyingine, tofauti na hii, pambana, kaza.

Ni hali ya kawaida kujisikia hivyo, huwa inatokea kujisikia kuacha chuo, hauko peke yako. Jitie moyo ili uendelee na safari, ni kweli safari ni ngumu, changamoto ni nyingi ila wewe pia unaweza kuimaliza, unaweza kufika mwisho.

Usiachie katikati, wewe pia ni mgumu unaweza kumaliza safari. Usiangalie nyuma na kutamani kurudi ulipotoka, angalia mbele na utengeneze mipango ya jinsi ya kupanda mlima huo. Unaweza kumaliza, utamaliza. Jikaze umalize, upate cheti, umalizane na deni lililokupeleka chuo.

Eunice

Pia Soma : Kwa anayeona chuo kigumu, hizi hapa namna ya kusurvive

Share Your Thoughts With Me

Translate »