white paper with heart print

(Maisha ya Chuo ni jukwaa linalokurahisishia maisha ya chuo kwa kushea dondoo, ushauri na kukupa msaada wa karibu uwapo chuo, bonyeza hapa kutufollow Instagram, Subscribe YouTube na soma makala nyingine nyingi zinazohusu wanachuo)


Hili ni jambo ambalo wengi huwa hatuliongelei ila huwa linatokea.

Ni swali ambalo wengi wetu tunalo na kimya kimya tunajiuliza maana dini ni kitu ambacho ni nyeti kidogo kwahiyo kuongelea hadharani mambo kama haya labda inaweza ikaonekana ni kama kudhalilisha dini. Lakini ukweli ni kuwa hili jambo linatokeaga.

Inaweza kuwa muda mwingine dini inachukua muda mwingi wa maisha ya viongozi wa dini, kwahiyo unakuta wanashindwa kuwa na uwiano kati ya dini na masomo yao.

Nahisi sababu kuu ni hiyo, kwahiyo unakuta wanakosa kupumzika, wanakosa kuhudhulia masomo, wanakosa kupata muda labda wa kusoma na wengine nk. Uongozi ni dhamana alisema hayati Magufuli, kwahiyo inaeleweka kuwa kazi inaweza kuwazidia kwenye eneo hilo la dini.

Pia Soma : Jinsi ya kupanga ratiba yako ya siku

Nilipokuwa chuo nilikuwa naona viongozi wa dini wanavyochelewa kulala, muda mwingine hawali na hata kushindwa kuhudhulia lectures kwa vile majukumu ya dini ni mengi.

Imani ni nzuri, ila ni muhimu kujua kuwa unapokua chuo wewe ni mwanachuo unayesali sio mhubiri unayesoma. Ni muhimu kuwekeza nguvu kwenye masomo cha Kaisari mpe Kaisari kwa moyo wote.

Ni muhimu kujua staili yako ya usomaji, kujua uelewa wako na kujua kumeneji muda vizuri ili uwe unapata pia na muda wa kusoma.

Kama unaona unahitaji nguvu sana kuelewa na unaona muda unakubana ni heri uache uongozi uweke nguvu kwenye masomo maana ukifeli chuo hauwezi tena kuwa kiongozi, wewe ni kiongozi wa dini chuoni kwa vile ni mwanachuo, ukiwa sio mwanachuo hauwezi kuwa kiongozi wa kikundi cha dini cha chuo.

Pia Soma : Kwa wanafunzi wa Kikristo waliopo vyuoni

Cha Kaisari mpe Kaisari kwa moyo wote, ishike elimu vizuri kwa vile umepata fursa ya kufika hatua hiyo.

Pia Soma : Kwa anayefikiria kuacha chuo

Eunice

You May Also Like

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป