Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Afya

Mabadiliko 5 unayoweza kuyafanya kila siku ili uwe na afya njema

Maisha yana siri moja tu kubwa, bila kuwa na afya njema mengine yote yanasimama. Yani afya tu, unaweza kuwa mwimbaji mzuri sana ila afya yako ikiwa namna gani vipi siku hiyo hatutokusikia, unaweza kuwa mwamafunzi, afya yako ikiwa namna gani vipi pia hauwezi kusoma. Kuishi maisha kwa kujijali na kujiangalia afya yako ni jambo la muhimu na hivyo kwenye makala hii naenda kuelezea mambo 5 unahoweza kuyaongezea kwenye maisha yako yanayoweza kukusaidia kuendelea kuwa na afya bora..

1. Kuusikiliza mwili wako

Hivi kwanini tukipiga miayo huwa tunajia kuwa tumechoka? Kwasababu miili yetu ina namna mbalimbali za kuwasiliana na sisi pale hali inapokuwa namna gani vipi. Sisi sio mashine lakini hata mashine pia hutoa taarifa kwa namna zake. Sikiliza mwili wako. Ukiona kipele sehemu ambayo hakuna kipele, kifuatilie usidharau. Ukiona ukila kitu fulani unapata matokeo haya fuatilia ili uyaepishe au uache kula kitu kile.

2. Fanya mazoezi

Mazoezi husaidia sana kuukumbusha mwili kuwa bado uko hai, viumbe vyote hutembea, hujongea. Ni vizuri kuufanyisha mazoezi mwili unafanya sehemu mbalimbali za mwili zikae sawa. Tafuta zoezi unalopenda kufanya, fanya.

3. Jitahidi kula vyakula asili kwa wingi na maji

Kama ni unga jaribu kula ule ambao hauna matengenezo mengi, kama ni nyama, zile ambazo si mpaka zimepitishwa viwandani nk. Kula vitu vikiwa na uasili wake ndio hata madaktari ushauri kuliko vyakula vingi vyenue kemikali na matengenezo mengi ya viwandani. Na maji, yani miili yetu asilimia kubwa ni maji, jitahidi kunywa maji mengi.

4. Kuwa na muda wa kulala na kuamka ule ule kila siku

Hili hata mimi bado sinaliwezea ndio maana makala hii inaandikwa usiku hivi, ila kuwa na muda ule ule wa kulala na kuamka kunausaidia mwili sana na kuna saidia hata mmeng’enyo wa chakula. Nilisoma kitabu fulani na walielezea kuwa hili pia linasaidia hata kwenye kuepusha sonona na kukusaidia hata kwenye kupungua uzito.

5. Fanya kitu kinachokuletea furaha kila siku

Kama unapenda kusoma vitabu, kuangalia machweo na mawio au kuongea na marafiki, jitahidi kufanya hivyo hata mara moja kwa siku hili linakuletea furaha na faraja. Hili pia linakusaidia kwenye afya ya akili.


Kama ungependa kujiunga group langu la WhatsApp ambalo natuma makala hizi moja kwa moja, BONYEZA HAPA.

Na pia kama unapenda kusapoti uendeshwaji wa blogu hii kifedha, unaweza nisapoti kwa kutuma kiwango chochote utakachopenda kwenda namba hii 0627975502. Fedha hizi zinanisaidia kulipia hosting ya blogu hii.

Share Your Thoughts With Me

Translate »