Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Random

Ideas za zawadi za mahafali | Graduation gift ideas

Unawaza nini cha kumpelekea / au kumpa ndugu yako/mwanao/rafiki ambaye anagraduate/ amegraduate?

Usiwaze tena.

Hizi Ni idea chache nilizonazo za vitu unavyoweza kumpa mpendwa wako:

Vitabu

Nimeandika list ya vitabu ambavyo natamani kila anayegraduate avisome. Unaweza chagua kimija wapo tu, na uhakika kitamtia moyo na kitamuondolea woga wa maisha ya mtaani… Kuiona list ya vitabu hivyo, bonyeza hapa.

– Card

Unaweza kumpelekea card iliyoandikwa maneno special kwaajili yake yatakayomfanya ajisikie vizuri kwenye siku yake. Bonyeza hapa nikutengeneze kadi kwaajili ya mpendwa wako anayehitimu

– Picha za frame /za kuchora

Nahisi kila nyumba inapicha ya mtoto wao alivyograduate ikiwa kwenye frame, sebuleni. Kuwa wa kwanza kumpatia picha hiyo itakayokuwa ndio kivutio sebuleni kwao, na hivyo kila akiiona atakukumbuka.. Unaweza kuzinunua sehemu za wapiga picha, nje ya ukumbi, Mara nyingi huwa zinakuwepo hapo.

-Accessories

Kutoa hela kwa watu wanaograduate ni kitu kizuri, lakini Mara nyingi nashauri utoe zawadi yenye thamani ya ile hela, kwasababu hela ataitumia atakusahau, ila zawadi itaendelea kuwepo physically, kwa muda kidogo.

Unaweza kumnunulia cheni, Saa, wallet, vitenge, bracelet, perfume, viatu, lotion,mashuka ya kuanzia maisha, headphones/ speaker, nguo nk.

Vitu ambavyo kila akivitumia/ akivaa anakumbuka siku yake na we we pia.

– Outing

Unaweza ukawasurprise na mtoko mmoja wa sehemu ambayo hawajawahi kwenda, ili tu wakapumzike baada ya masomo.

– Chocolate

– Kitu chochote ambacho walikuwa wanakitaja kwa muda mrefu

Muda mwingine kujua zawadi ya kumpa mtu, inatokana sana na kumsikiliza anachokisema Mara nyingi, labda hicho ndicho anachohitaji.

Link ya makala nilizoziandika kwaajili ya wanaograduate

Pia unaweza kuwatumia makala mbalimbali nilizoziandika kwaajili ya wanaograduate.. Zitawatia moyo, zitawapa muongozo, kuwafariji na kuwaondolea woga. Unaweza kuzipata hapa


Je, umegraduate? Hongera sana.. Umeletewa zawadi gani?

Na je, una mtu ambaye amegraduate? Umempelekea zawadi gani?

Share kwenye comment!

Eunice

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป