Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

Maisha ya kila siku

Ukiwa busy kuangalia maisha ya wenzako, ya kwako yatakupita

Leo nimekutana na mlinzi wa shule moja hapa mjini, na kwavile nilimsindikiza mentor wangu kuangalia shule ya mwanae, nimekutana na watu wengi na wenye kazi mbalimbali.

Wakati naongea na huyo mlinzi alinisimulia kuhusu kazi anayofanya na vile yeye sio mlinzi tu ila amejiendeleza na kuwa dereva pia. Nilifurahishwa sana na jitihada zake za kujiendeleza, nikamsifia sana.

Ambapo akanijibu, ‘sio kwamba napata kingi sana kwenye maisha yangu, ila hiki ninachopata kimenisaidia kufanya mengi, wanangu wanasoma na nyumbani tunakula, ukiangalia ya wengine utakuta yako vizuri sana na wako mbali tofauti na Mimi, ila kwa hapa nilipo naona Niko vizuri ingawa sio kama wengine’.

Nakumbuka nilimjibu, ‘Nahisi kama kwenye maisha ukiangalia ya wengine, ya kwako yanakupita na unakuwa hauishi ya kwako kwani uko busy kuangalia ya wengine’.

Katika muda huo nikaona nishapata idea ya kuandika blog post, lakini pia niliona nimeongea jambo la maana sana toka wiki ianze????.

Huwa najiuliza Mara nyingi,

Maisha ni nini?

Tunatafuta nini wakati tunaishi?

Kwanini tunafanya tunayoyafanya?

Jambo gani la muhimu kwenye maisha?

Kwanini tupo vile tulivyo?

Sisi ni nani? Na tunaelekea wapi?

Kwanini tunashindana na kutamani kuonekana juu?

Siwezi sema nimepata majibu kuhusu maisha, ila natamani niishi huku nikijaribu kuuliza maswali tu na sio kufuaata mkumbo.

Mfano: Kwanini tunashindana na kutamani kuonekana juu?

Kama umegundua duniani kote, we are searching.

Tunatafuta, kila saa, kila siku.

Tunatafuta furaha, chakula, amani no

We are all searching. Ni kama vile tunahitaji moyoni, ambalo tunatafutia tuba kwenye chochote tunachohisi kinatibu.

Baada ya kuishi, na kuenjoy kwamba uko hai, inaonekana kama vile tunahitaji vya ziada.

Na ukweli ni kwamba hatujawahi ridhika.

Kuna mstari wa Biblia unasema, ‘je, jicho lishawahi kushiba kuona? Na sikio kusikia?’

Jibu ni hapana, kama hatutochagua na kuamua maana ya kufanikiwa ni ipi inayokufaa, dunia itakukumbusha kwamba ulivyonavyo havitoshi.

Na ndiko mashindano yanapokuja, na kujiringanisha na kutamani kuonekana juu ya mwenzio.

Nahisi kama dhambi nyingi zinatokana na watu kutafuta power. Lakini kwanini tunatafuta kuwa na power juu ya mtu mwingine, kwanini tusitafute power juu yetu? Kwanini tusihangaike kujicontrol wenyewe na kuacha kutamani kuwa control wengine?

Kwa vile tuko busy kutafuta namna gani yule amekuzidi kwenye hili na lile, au namna gani umemzidi kwenye hili na lile, tunasahau kuishi.

Tunasahu kuridhika, kufurahia tulivyonavyo, kufurahia mafanikio yetu ambayo sio kama vile jamii ingependa tuwe ila ni yetu, maisha yetu yanatupita.

Tunakuwa busy kushindana ili kupata Yale ambayo hayatuletei furaha au kama yanaleta ni ya muda mfupi, tunawaangalia kwa dharau wengine na kufurahia kuwashusha ambao tunaona wako chini yetu, au hawako kama sisi, tunajisikia wanyonge kama hatujafanikiwa katika level ambayo jamii inaona ndio mafanikio, hatuishi maisha, maisha yetu yanatupita.

Natamani nimwambie yule mlinzi, najivunia maisha yake, yana thamani kwa wanae, yanathamani kwa watu wanaohusika naye kama wanae na mkewe, najivunia kujiendeleza kwake, natumaini anafuraha nakuona vile alivyokuwa wathamani na bora. Popote ulipo kwenye maisha, ishi maisha yako.

Ukiwa busy kuangalia maisha ya wenzako, ya kwako yanakupita.

Eunice

4 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป