Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

black student listening to music using smartphone in park
Maisha ya Chuo,  Vitabu

Majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuoni

Bado nakumbuka kipindi kile naenda chuo, nakumbuka ule woga niliokuwa nao, maswali ya kuwaza maisha ya chuo yatakuwaje lakini pia ile furaha ya kwenda kuanza maisha yangu mapya ya chuoni.

Nakumbuka nilipokuwa chuo nilikuwa napitia nyakati mbalimbali ambazo nilikuwa natamani nimuulize mtu aliyepita chuo ili anipe moyo, nilikuwa na maswali mengi kwenye maswala ya mahusiano, tulipoamua kugoma na wenzangu darasani nilikuwa natamani kusikia stori za waliotutangulia kuhusu hilo swala, na nilipomaliza chuo niliwaza kwanini sikujiandaa na maisha ya kitaa miaka yote minne niliyokuwa chuo na mpaka nikapitia msongo wa mawazo baada ya kuhitimu.

Ndio maana niliamua kuanzisha Maisha ya Chuo, jukwaa ambalo linawaunganisha wanachuo, lakini pia linashea dondoo na msaada unaowasaidia chuoni na katika changamoto yoyote ile, mwaka huu niliamua kuungana na wahitimu wengine na wanachuo wa miaka ya mwishoni kuandaa huu muongozo kuhusu maisha ya chuo ili kushea ujuzi wetu, dondoo na ushauri pia. Kitabu hiki ni cha Kiswahili, na kimeanza kupatikana sasa.

Kwenye kitabu hiki utakutana na mada mbalimbali kama vile mahusiano na urafiki chuoni, maswala ya pesa na biashara chuoni, mambo ya kufanya ukipata skendo chuoni, afya ya akili chuoni, kukaa off campus na on campus na changamoto zake, jinsi ya kujiandaa na maisha ya kitaa ukiwa chuo, fursa zilizopo chuoni ambazo zinaweza kukusaidia mwanafunzi, ujuzi ambao unaweza kuupata chuo ili ukihitimu usiwe tu na cheti ila uwe na ujuzi mwingine utakaokusaidia hata kujiajiri, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, migomo, mambo ya supp, carry na disco na mada nyingine kibao zinazowahusu wanachuo.

Unaweza kukipata kitabu hiki sasa kwa gharama ya Tsh 5000/= tu kwenda namba 0627975502 au 0683687524 (Jina ni Eunice Tossy Jonassy), na hapo hapo nitakutumia kitabu hiki.

Kama una maswali zaidi kuhusu process za kutuma pesa na kukipata kitabu hiki, wasiliana nami kwa number hii 0627975502.

Eunice

8 Comments

  • Gachewa

    Nimekipitia kitabu hiki toka mwanzoni hadi tamati, na kwa kweli kina ujumbe muhimu hususan kwa wanachuo wapya. Ingawaje hata youth yeyote yule atapata mengi kutoka hapo. Kiko poa cha kujiandaa kwa maisha ya chuo, na kujipanga ili wakati utakaokuwa chuoni uweze kufanikisha mengi. Zaidi ya hayo kitakuandaa pia kwa maisha ya hapo baadaye, mambo kama kazi, hela, biashara za kando na kadhalika. Asante sana Eunice.

    • Moureen

      Actually I read the book in one day,and i think it’s very thoughtful of you to write such a masterpiece,kiukweli kitabu ni kizuri hasa kwa sisi tunaotarajia kuanza chuo mwaka wa kwanza, ni kitabu ambacho mtu unakisoma na unataman hata kisiishe yan kiwe endless,for sure thank you so much sis,I’ve learnt so many things throughout your book,Kimenifunza mengi san na sasa naweza kusema nipo tayr kuyaface maisha haya mapya..I encourage you to keep writing such books as there are few people who are willing kuandika kitabu kinachomuongoza mtu katika kuelekea chuoni,Honestly am grateful for this and may God keep blessing you in everything you do..love you Eunice❤️Thanks again

Share Your Thoughts With Me

Translate »