Pata majibu ya maswali yote uliyonayo kuhusu maisha ya chuo na changamoto zake

man writing on a notebook
Maisha ya Chuo

Vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 5000/= tu, bonyeza hapa)


Hongera kwa kufika chuo tena, sehemu yenye uhuru na maamuzi unayoyafanya mwenyewe. Hakuna kitu kizuri kama hicho kwenye maisha, kuwa huru. Katika yote chuo, leo ningependa kukuambia vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo, vya kuviangalia kwa jicho la tofauti maana vina umuhimu kwenye maisha yako ya chuo.

Vitu vyenyewe ni:

Kitu cha 1: Urafiki utakaouchagua

Kuna msemo unasema “nionyeshe marafiki zako watano, nami nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani”, lakini pia watu husema, marafiki utakaowatengeneza chuo unaweza kudumu nao mpaka milele”, inawezekana ni kweli au sio kweli lakini ninakubaliana nao. Chuoni ni sehemu ambako nimetengeneza urafiki, tena wa kweli. Kuwa makini na kuchagua marafiki wako hasa sasa. Watu utakaowapata chuo wanaweza kukusababisha ufanikiwe au usifanikiwe kwenye maisha kwahiyo kuwa makini na chaguzi yako.

Pia Soma : Urafiki chuoni

Kitu cha 2: Masomo yako

Kuna watu wanasema GPA haina umuhimu, inawezekana ni kweli au si kweli, lakini kumbuka sababu kuu iliyokupeleka chuo ni kusoma, kwahivyo kuwa makini na masomo yako, ni heri kuona GPA haina umuhimu ukiwa nayo nzuri, kuliko usipokuwa nayo nzuri. Mimi nimepata cheti changu kuna muda nikikiangalia natamani niongeze point 0.1 tu ili nibadilishe class kabisa. Pambana na masomo utoke na GPA nzuri.

Kitu cha 3: Matumizi ya hela

Hivi karibuni nimepiga mahesabu ya hela nilizokuwa nazipata nikiwa chuoni, na nikagundua kuwa kama ningekuwa mtumiaji mzuri ningekuwa hata bilionea (au hata milionea basi au hata nina hela kidogo), lakini sikuwa na huo ufahamu au hata sikupewa ushauri basi toka naanza chuo. Lakini sitaki wewe upitie njia hiyohiyo, maana unaweza ukakosa hata nauli ya kusambazia hiyo barua ya kuombea kazi ukimaliza chuo.

Unaweza ukawa na matumizi mazuri ya hela ukiwa chuoni kwa:

-Kuwa na budget ya matumizi ya hela zako (hili nitaliongelea kwenye post zijazo)

-Kufungua biashara ambazo zitakuingizia kipato (saloon na biashara ya chakula ni biashara maarufu sana maeneo ya chuo)

– Kukaa na marafiki zako sehemu moja ili kusave hela

-Kufungua savings account au fixed account kwaajili ya pesa zako. Saving account usiiiguse kabisa utahifadhi tu hela, na fixed itakusaidia kuongeza hela baada ya kuiacha kwa muda.

-Kuweka bill (mimi sikuweka bill, ila walioweka bill wanasema iliwapunguzia gharama za maisha)

Soma zaidi kuhusu kuwa na matumizi mazuri ya pesa hapa.

Kitu cha 4: Afya yako

Kuwa makini na afya yako labda ningeweka kama kitu cha kwanza kwasababu chuoni unapitia/utapitia vingi sana vitakavyokuletea msongo wa mawazo kwenye maisha yako hapo chuo, kumbuka unadili na masomo lakini wakati huohuo kuna familia inakuzunguka, mahusiano, drama za marafiki, lakini siku nyingine unakuwa tu umechoka, kuwa makini na afya yako, kwasababu hakuna umuhimu wa wewe kuugua au kupata matatizo eti kisa unasoma sana, na hata hivyo ukiugua hauwezi hata kusoma. Hivyo kuwa makini na afya yako, kimwili, kihisia, kiroho, kijamii na kisaikolojia.

Unaweza kufanya mambo yafuatayo katika kukusaidia kuwa makini na afya yako:

-Kufanya mazoezi

-Kunywa maji, kula vizuri,kupumzika muda wa kutosha( masaa nane)

-Kutoka nje ya mazingira ya chuo, kutembelea vivutio,beach nk

-Kukutana na marafiki, hakikisha una mtu hata mmoja unaemuamini kushirikiana naye unapopitia matatizo.

Soma hapa kuhusu jinsi ya kujali afya yako ya akili chuoni.

Kitu cha 5: Image yako

Kuwa makini sana na image yako unapokuwa chuoni. Siri moja katika maisha ni kwamba hakuna watu wapya( zaidi ya waliozaliwa), hao uliotoka nao primary wengine mnakutana chuo au mtakutana ofisini au uliokutana nao chuo watakutana ofisini na watu uliosoma nao primary, kwahiyo kuwa makini na image yako unayoiweka mbele za watu.

Hapa simaanishi uigize maisha ya watu ambayo siyo yako, na simaanishi ubadilishe maisha yako ili uonekane perfect, namaanisha maisha yenye taarifa mbaya, au image mbaya ambayo watu wataipata kuhusu wewe.

Na hivyo ni vitu vitano vya kuzingatia unapokuwa chuo. Ila kikubwa zaidi ya vyote, ni usimuache Mungu, alikusaidia huku chini, atakusaidia na chuo pia.

(Kupata dondoo hizi na nyingine nyingi, pata kitabu cha Your Guide to University Life, kinachokusaidia kupata majibu ya maswali na kila jambo unaloweza kupitia kama mwanachuo, kwenye kitabu hiki utapata ushauri kutoka kwa waliomalia chuo kuhusiana na maswala ya pesa na biashara, urafiki, supp, carry, disco, mahusiano, migomo, mambo ya kufanya ukipata skendo chuo, jinsi ya kudili na walimu wasumbufu, ushauri wa mitindo, jinsi ya kujiandaa na maisha ya mtaani ukiwa chuo na mada nyingine kedekede, kukipata kitabu hicho kwa Tsh 15000/= tu, bonyeza hapa)

Eunice

17 Comments

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป