Hongera kwa kufika chuo tena, sehemu yenye uhuru na maamuzi unayoyafanya mwenyewe. Hakuna kitu kizuri kama hicho kwenye maisha, kuwa huru. Katika yote chuo, leo ningependa kukuambia vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo, vya kuviangalia kwa jicho la tofauti maana vina umuhimu kwenye maisha yako ya chuo.

Vitu vyenyewe ni:

Kitu cha 1: Urafiki utakaouchagua

Kuna msemo unasema “nionyeshe marafiki zako watano, nami nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani”, lakini pia watu husema, marafiki utakaowatengeneza chuo unaweza kudumu nao mpaka milele”, inawezekana ni kweli au sio kweli lakini ninakubaliana nao. Chuoni ni sehemu ambako nimetengeneza urafiki, tena wa kweli. Kuwa makini na kuchagua marafiki wako hasa sasa. Watu utakaowapata chuo wanaweza kukusababisha ufanikiwe au usifanikiwe kwenye maisha kwahiyo kuwa makini na chaguzi yako.

Pia Soma : Urafiki chuoni

Kitu cha 2: Masomo yako

Kuna watu wanasema GPA haina umuhimu, inawezekana ni kweli au si kweli, lakini kumbuka sababu kuu iliyokupeleka chuo ni kusoma, kwahivyo kuwa makini na masomo yako, ni heri kuona GPA haina umuhimu ukiwa nayo nzuri, kuliko usipokuwa nayo nzuri. Mimi nimepata cheti changu kuna muda nikikiangalia natamani niongeze point 0.1 tu ili nibadilishe class kabisa. Pambana na masomo utoke na GPA nzuri.

Kitu cha 3: Matumizi ya hela

Hivi karibuni nimepiga mahesabu ya hela nilizokuwa nazipata nikiwa chuoni, na nikagundua kuwa kama ningekuwa mtumiaji mzuri ningekuwa hata bilionea (au hata milionea basi au hata nina hela kidogo), lakini sikuwa na huo ufahamu au hata sikupewa ushauri basi toka naanza chuo. Lakini sitaki wewe upitie njia hiyohiyo, maana unaweza ukakosa hata nauli ya kusambazia hiyo barua ya kuombea kazi ukimaliza chuo.

Unaweza ukawa na matumizi mazuri ya hela ukiwa chuoni kwa:

-Kuwa na budget ya matumizi ya hela zako (hili nitaliongelea kwenye post zijazo)

-Kufungua biashara ambazo zitakuingizia kipato (saloon na biashara ya chakula ni biashara maarufu sana maeneo ya chuo)

– Kukaa na marafiki zako sehemu moja ili kusave hela

-Kufungua savings account au fixed account kwaajili ya pesa zako. Saving account usiiiguse kabisa utahifadhi tu hela, na fixed itakusaidia kuongeza hela baada ya kuiacha kwa muda.

-Kuweka bill (mimi sikuweka bill, ila walioweka bill wanasema iliwapunguzia gharama za maisha)

Soma zaidi kuhusu kuwa na matumizi mazuri ya pesa hapa.

Kitu cha 4: Afya yako

Kuwa makini na afya yako labda ningeweka kama kitu cha kwanza kwasababu chuoni unapitia/utapitia vingi sana vitakavyokuletea msongo wa mawazo kwenye maisha yako hapo chuo, kumbuka unadili na masomo lakini wakati huohuo kuna familia inakuzunguka, mahusiano, drama za marafiki, lakini siku nyingine unakuwa tu umechoka, kuwa makini na afya yako, kwasababu hakuna umuhimu wa wewe kuugua au kupata matatizo eti kisa unasoma sana, na hata hivyo ukiugua hauwezi hata kusoma. Hivyo kuwa makini na afya yako, kimwili, kihisia, kiroho, kijamii na kisaikolojia.

Unaweza kufanya mambo yafuatayo katika kukusaidia kuwa makini na afya yako:

-Kufanya mazoezi

-Kunywa maji, kula vizuri,kupumzika muda wa kutosha( masaa nane)

-Kutoka nje ya mazingira ya chuo, kutembelea vivutio,beach nk

-Kukutana na marafiki, hakikisha una mtu hata mmoja unaemuamini kushirikiana naye unapopitia matatizo.

Soma hapa kuhusu jinsi ya kujali afya yako ya akili chuoni.

Kitu cha 5: Image yako

Kuwa makini sana na image yako unapokuwa chuoni. Siri moja katika maisha ni kwamba hakuna watu wapya( zaidi ya waliozaliwa), hao uliotoka nao primary wengine mnakutana chuo au mtakutana ofisini au uliokutana nao chuo watakutana ofisini na watu uliosoma nao primary, kwahiyo kuwa makini na image yako unayoiweka mbele za watu.

Hapa simaanishi uigize maisha ya watu ambayo siyo yako, na simaanishi ubadilishe maisha yako ili uonekane perfect, namaanisha maisha yenye taarifa mbaya, au image mbaya ambayo watu wataipata kuhusu wewe.

Na hivyo ni vitu vitano vya kuzingatia unapokuwa chuo. Ila kikubwa zaidi ya vyote, ni usimuache Mungu, alikusaidia huku chini, atakusaidia na chuo pia.

(bonyeza hapa kufollow akaunti ya Maisha ya Chuo Instagram, akaunti hii inashare dondoo na ushauri unaomsaidia mwanachuo kukabiliana na changamoto za maisha ya chuo)

Eunice

You May Also Like

17 thoughts on “Vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo

 1. Praygod

  I’m in love with your work?

  1. Eunice Tossy

   Thank you Praygod.. Glad to have you here?

 2. Pascal

  how come i didnt hear this from you?! luk now it’s too late hhhha

  1. Eunice Tossy

   Ha ha! Jameni.. Am doooh!

  2. Eunice Tossy

   I was learning back them

 3. Pascal

  I love this blog, keep it up sis

  1. Eunice Tossy

   Thank you my young.. Thank you so much!

 4. Stephen Liondo

  I really admire the wisdom you have. I can tell that you will one day make a great woman in history. Keep it up. May God bless you.

 5. Eunice Tossy

  Thank you so much Stephen..

  That means a lot brother. Amen?

 6. Mailz

  Am happy to be here

 7. Mailz

  Am happy to be here

  1. Eunice Tossy

   Am happy to have you Mailz???

 8. Mpaji

  Fixed account mfano account ta bank ipi?

  1. Eunice Tossy

   Bank zote nadhani unauwezo wa kuweka fixed account..

   Ninachoweza kukushauri nenda kaulizie process za bank tofauti uangalie pia kiwango wanachoongeza ukiweka fixed halafu ufanye uamuzi baada ya kuona inayokufaa kutokana na research utakayofanya

 9. Makala 6 za Kiswahili ulizozipenda sana kwenye mwaka 2019 - Eunice Tossy

  […] 1- Vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo […]

 10. Aloyce Ackley

  I really appreciate what your doing, your guiding us better for the future goals in uni. I cant wait to see your new posts everytime en i wish god graces upon u to keep u healthie en strong enough to keep on sharing ur knowledge

  1. Eunice Tossy

   Thank you Aloyce.. means a lot to see that you appreciate. Thank you so much.
   Amen and amen.

Share Your Thoughts With Me

Translate ยป